Kwanini sisi wapare hatujui football?

Kwanini sisi wapare hatujui football?

Mussa Msangi (Marehemu)

Kocha Mziray (Marehemu)
 
Toka nizaliwe sijawahi kuona au kusikia mcheza mpira mkubwa Tanzania ligi kuu ni mpare kwanini?
Naomba serikali ifanye utafiti.
Mussa msangi alikuwa anaupiga mwingi sana labda ulikuwa hujazaliwa!
 
Wapo bana
1.SEKILOJO
2.GAdiel
3.Mussa Msangi
Nadhani na Zawadi Mauya mana pale ndungu kuna ukoo wa Mauya
Akija jukwaaji Uncle Karigo atatutajia wengine
 
mtoto wa 2000 atajuaje hayo. kuna mada humu zikianzishwa unapata kujua umri wa mtu. wengi vijanjaro vimeanza kushabikia mpira 2010 wc ya SA. ukimuambia gwiji sekilojo chambua atatumbua macho.
Sekilojo chambua,gula joshua,noah kilimanjaro na gadiel michael mbaga
 
Toka nizaliwe sijawahi kuona au kusikia mcheza mpira mkubwa Tanzania ligi kuu ni mpare kwanini?
Naomba serikali ifanye utafiti.
ni kwasababu ninyi ni wafupi, labda mkacheze na vistuli wenzenu (in mchaga's voice).
 
Moto anatakiwa apate muda wa kutosha kuwa huru acheze sana mpira ili awe fundi

Wazazi wengi upareni mtoto ni kazi kazi full under control. Usipofanya kazi za familia unaweza usile

Pwani watoto hawapewi sana kazi na wazazi wao. Mtoto anatafutwa ili ale.
Hivyo anakuwa na muda wa kutosha kujifunza mpira na mengineyo.

Ndio maana vijana wa kiume wa pwani wanna vipaji sana vya nje ya masomo. Na wanafanikiwa sana

Hata mabinti wa pwani ni mafundi KWA vile ukiachana na mafunzo ya unyago,hawabanwi sana katika ukuaji wao
Kweli kabisa vijana wa pwani wana muda mwingi wa kufanya mambo nje ya shule, muziki, mpira na sanaa mbalimbali wanazoona wanafit na wengi hutobolea hukohuko
 
Hahaha, na kweli sijawahi sikia mchome, mbaga, mndeme. Ila nadhani hata wachaga na wamasai ni wachache, mara chache sana kusikia Lymo, mushi, saitoti, Mollel... Nadhani kaskazini na mpira kidogo ni changamoto.
Gadiel Michael Mbaga
 
Back
Top Bottom