Kwanini sisikii kesi za Wagombea Ubunge upinzani kudai kuibiwa ushindi?

Kwanini sisikii kesi za Wagombea Ubunge upinzani kudai kuibiwa ushindi?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Zaidi nasikia uchaguzi umeisha tufanye yajayo.

Miaka iliyopita watu walikuwa wanakwenda mahakamani kudai haki zao zilizopokonywa na wengine walishinda.

Je,
Hawana ushahidi?
Wamekubali yaishe?
Hawajaibiwa Bali wamepigwa kisawasawa?
Wanatishwa?
Wanatafakari kilichotokea?
Wanajiandaa kuunga Mkono juhudi?

None of the above?
 
Sheria inatumika kupinga matokeo ya uchaguzi ila huu hata sifa ya kuitwa uchaguzi hauna.
Matokeo ndio hayana Sifa au uchaguzi. Je wapinzani hawa kuwa na uwezo wa kuforecast na kuamua kutoshiriki ili hiki kinachofanyika sasa (kutokudai hali kama wameonewa) kisifanyike ili wahamishie mashambulizi huko ICC na EU, US
 
Wapinzani wametafakari mengi, japo fomu za matokeo hawana/hawakupewa sababu ilitungwa sheria ya uchaguzi inayosema fomu za matokeo kupewa sio lazima, lakini pia hata huko mahakamani hawana uhakika kama haki itatendeka, kwasababu NEC na mahakama wote ni waajiriwa wa CCM.
 
Kuna ule wimbo wa Zuchu alikuwa anaimba "wapinzani watetereke mama", ndio kutetereka huko sasa
 
Mahakama hizihizi ambazo ni chumba cha pili cha magufuli? Acha Ulaya watusaidie jamani
Huoni wakienda na wakafigisiwa itawaongezea walaya Nyama katika kutubana huku na kuwadhibitishia kuwa mihimili yote haikoromi.

Sasa bila hili huoni kama ni propaganda tu za kulialia
 
Wapinzani wametafakari mengi, japo fomu za matokeo hawana/hawakupewa sababu ilitungwa sheria ya uchaguzi inayosema fomu za matokeo kupewa sio lazima, lakini pia hata huko mahakamani hawana uhakika kama haki itatendeka, kwasababu NEC na mahakama wote ni waajiriwa wa CCM.
Inawezekana wapinzani wanajua kuwa wakikata rufaa watatoa mwanya wa wagombea wao wachache kupewa ushindi wa mezani ili kuhalalisha uchaguzi mzima na kuleta mpasuko kwenye vyama vyao. Hamna kitu kinachopiganiwa sasa kama kupata wapinzani wachache kutoka vyama vinavyoeleweka bungeni.

Amandla...
 
Uzuri hata hao kina Bashiru Ally huko CCM nao wako kimya maana roho inamuuma sana japo haongei. Ashawahi kusema Tanzania uchaguzi ni kituko. Hapo alipo amekosa hata jina la kuupa huu uchaguzi. Akisema ni kituko atakuwa ameupamba sana
Bora akae kimya tu
 
Back
Top Bottom