Kwanini sisikii kesi za Wagombea Ubunge upinzani kudai kuibiwa ushindi?

Kwanini sisikii kesi za Wagombea Ubunge upinzani kudai kuibiwa ushindi?

Inawezekana wapinzani wanajua kuwa wakikata rufaa watatoa mwanya wa wagombea wao wachache kupewa ushindi wa mezani ili kuhalalisha uchaguzi mzima na kuleta mpasuko kwenye vyama vyao. Hamna kitu kinachopiganiwa sasa kama kupata wapinzani wachache kutoka vyama vinavyoeleweka bungeni.

Amandla...
Kwa nini CCM watake wapinzani bungrni ikiwa uchaguzi huwa ni waushindani. Na kama ni ushindani basi hata wapinzani kuna siku wanaweza kukwaa Viti vyote?

Au vyma vingi maana yake asipatikane ambaye wanaweza kushinda zaidi ya 90℅ hata kama wananchi wameamua.

Huoni hii sio democrasia
 
Kesi ya tumbili. Kama mahakimu wamepewa teuzi promotion ikiwemo ujaji kwa kuwashughulikia na kuwafunga wapinzani ili kumfurahisha malaika mkuu hio si kesi ya nyani na gendere kula mahindi shambani
 
Matokeo ndio hayana Sifa au uchaguzi. Je wapinzani hawa kuwa na uwezo wa kuforecast na kuamua kutoshiriki ili hiki kinachofanyika sasa (kutokudai hali kama wameonewa) kisifanyike ili wahamishie mashambulizi huko ICC na EU, US
Kushiriki uchaguzi huu kumefanya tuyafahamu mengi juu ya wizi uliotokea, kwa mdano Mimi, nimekuwa msimamizi wa uchaguzi huu ni wizi ulivyofanyika nimeona kwa macho yangu. Haukuwa uchaguzi nilikuwa ni upumbavu tu.
 
Kama hawakupewa mkuu sasa mahakamani so wanashinda asubuhi tu.

Kuna nini aisee
Nilisikia mkuu akimwambia AG wakati anamwapisha kuwa hatarajii kuona serikali inashidwa kesi mahakamani. Nami nikabaki najiuliza ni agizo ama. Nawasihii wabunge na madiwani walio shidwa hata kwa goli la mkono kutokwaenda mahakanani. Sauti ya mkuu ni amri,lejea alipo mwambia sipika Ndungai kuwa washughulikie huko bungeni wakija huku serikali itawashughurikia. Nadhani uliona alicho kifanya Ndugai
 
Zaidi nasikia uchaguzi umeisha tufanye yajayo.

Miaka iliyopita watu walikuwa wanakwenda mahakamani kudai haki zao zilizopokonywa na wengine walishinda.

Je,
Hawana ushahidi?
Wamrkubali yaishe?
Hawajaibiwa Bali wamepigwa kisawasawa?
Wanatishwa?
Wanatafakari kilichotokea?
Wanajiandaa kuunga Mkono juhudi?

None of the above?
Kwa sababu mahakama hazipo huru.
Zinafuata maelekezo ya Meko.
 
Mkuu tutumie hisia.
Sio kwamba AG alikuwa anapewa changamoto atumie weledi wake wa kisheria.

Mfano nimewahi kuwa mahala kila kesi kampuni inashindwa. ILa walipoamua kuwa na wanasheria sirias na kutafuta watu sirias hakuna aliyrkuwa anatoboa na kupewa fidia labda uhurumiwe tu.
 
Kwa sababu mahakama hazipo huru.
Zinafuata maelekezo ya Meko.
Kuna kaushahidi kidogo kukoleza hoja.
Maana Melo angrkuwa ananyea beseni keko na jf ingerudi ile ya Kenya kama kungrkuwa na unachosrma
 
Zaidi nasikia uchaguzi umeisha tufanye yajayo.

Miaka iliyopita watu walikuwa wanakwenda mahakamani kudai haki zao zilizopokonywa na wengine walishinda.

Je,
Hawana ushahidi?
Wamrkubali yaishe?
Hawajaibiwa Bali wamepigwa kisawasawa?
Wanatishwa?
Wanatafakari kilichotokea?
Wanajiandaa kuunga Mkono juhudi?

None of the above?

Hakuna hata mmoja hapo. sababu ni KUTOKUAMINI MAHAKAMA YENYEWE. Kesi wapi wakati uchaguzi wote ulikuwa wa wizi na kupagwa! Yaani kama ni kesi ni kila jimbo Tanzania!. Vilevile Kesi zinachukua muda mrefu hadi miaka 4 sasa mhula wa miaka mitano kesi miaka 4!!!. Tanzania hakuna demokrasia tena tusiangalie upinzania hili ni jambo la nchi
 
Kwa nini CCM watake wapinzani bungrni ikiwa uchaguzi huwa ni waushindani. Na kama ni ushindani basi hata wapinzani kuna siku wanaweza kukwaa Viti vyote?

Au vyma vingi maana yake asipatikane ambaye wanaweza kushinda zaidi ya 90℅ hata kama wananchi wameamua.

Huoni hii sio democrasia
Kinachoangaliwa ni namna huo ushindi ulivyopatikana. Hata mwalimu akisema mtoto wake amekuwa wa kwanza darasani halafu akakataa kurudisha makaratasi ya mitihani. Na hii baada ya wanafunzi wengine wote walivyoshuhudia alivyo mpa majibu mtoto wake na kuwanyang'anya wengine makaratasi yao kabla ya muda. Hakuna atakayeamini kuwa anasema kweli.

Amandla...
 
Hakukuwa na uchaguzi, sasa utaenda kufungua kesi gani mahakamani?
 
Kinachoangaliwa ni namna huo ushindi ulivyopatikana. Hata mwalimu akisema mtoto wake amekuwa wa kwanza darasani halafu akakataa kurudisha makaratasi ya mitihani. Na hii baada ya wanafunzi wengine wote walivyoshuhudia alivyo mpa majibu mtoto wake na kuwanyang'anya wengine makaratasi yao kabla ya muda. Hakuna atakayeamini kuwa anasema kweli.

Amandla...
Mkuu umeandika kama wale maphilosopher wa kigiriki BC
 
Hivi ghararama ya kufungua kesi ya uchaguzi bei gani
 
Hakuna hata mmoja hapo. sababu ni KUTOKUAMINI MAHAKAMA YENYEWE. Kesi wapi wakati uchaguzi wote ulikuwa wa wizi na kupagwa! Yaani kama ni kesi ni kila jimbo Tanzania!. Vilevile Kesi zinachukua muda mrefu hadi miaka 4 sasa mhula wa miaka mitano kesi miaka 4!!!. Tanzania hakuna demokrasia tena tusiangalie upinzania hili ni jambo la nchi
Vipi Mzungu akitupotezea kwa sababu hata hivyo hatugombani na kuna nchi nyingi zinamatatizo kama yetu ILS yao yameiva hadi wanatwangana. EU, ICC na US wakaamua kujishughulisha na kesi ngumu.

Watafanyaje maana Mahakama hawaiamini.
 
Kwa nini unawataka waende mahakamani badala ya kuishauti serikali yako ilete tume huru ya uchaguzi??
Tumegundua kwa hoja za wadau kuwa tatizo sio tu tume Bali bali wanaituhumu Mahakama pia.

Nilitegemea njia ya kuidhibiti tume isiyohuru hasa kwa uchaguzi wa wabunge ni mahakamani. Time ikiwa hivi hivi na tuhuma za kutokuwa guru tumewahi kuna wabungr wa upinzani wanashinda kesi na kutinga mjengoni.

Au tatizo ni kificho. Halijulikani ni tume au Mahakama au dola au mtawala au Ccm au wapinzani mwenyewe wanazingua
 
Ushindi analilia Trump, sisi tumekubali ili CCM ilete maendeleo.
 
Back
Top Bottom