Kwanini sisikii kesi za Wagombea Ubunge upinzani kudai kuibiwa ushindi?

Hii nayo ni pointi, wamewaacha wajikaange kwa mafuta yao wenyewe.
 
Tangy lini ,kesi ya mbuzi ikaamuliwa na fisi na ukapatikana uwanja tambarare?wa kuzungumzia kesi hiyo?
 
Mkuu, kwa mazingila yale, hata ukirudiwa uchaguzi mara10,matokeo yatakuwa hayo hayo. WE ULIONA WAPI MTU ANAKUTWA NA KURA AMBAZO ZISHAPIGWA TAYARI NJE YA KITUO, lakini hachukuliwi hatua yoyote?
Sasa unapelekaje kesi ya wizi kwa mwizi kwa mfano.
 
Bila kuwa na nakala ya matokeo kutoka vituo vya kumpigia kura utakuwa na ushahidi gani?
 
You are a genius
 
Kwa uxhaguzi upi chief. Ni uchaguzi mzima uliharibiwa na CCM
 
Kura zote zilizopigwa zikikuwa halali,maana hata amabae hakwenda kupiga kura ALIPIGA KURA tena alimpigia magufuli ba genge lake.hapo mahakama itaamuaje!!
 
Kushiriki uchaguzi huu kumefanya tuyafahamu mengi juu ya wizi uliotokea, kwa mdano Mimi, nimekuwa msimamizi wa uchaguzi huu ni wizi ulivyofanyika nimeona kwa macho yangu. Haukuwa uchaguzi nilikuwa ni upumbavu tu.
Wametudharau sana, yani tukio la mara moja kila baada ya miaka mitano kutokea ndio wamekuja kuligeuza la hovyo kabisa, wakaliondolea thamani yake yote.
 
Maandalizi ya wizi yalipangwa
Nakala za matokeo hawakupatiwa
Mahakamani wanaendaje?Kila kituo mnacho ,wizi hudanyika Kila uchaguzi Ila safari hii mmetia aibu.
Kama huku kusini SIsiem sijui wapi mlishinda
 
Kesi ya nyani ....
 
Wakienda mahakamani watawatafutia mahakimu ujaji.ukimnyongea mpinani unapanda cheo.
 
Tushasema hakukuwa na uchaguzi Tanzania yalikuwa maigizo. Usifanye watu wajinga.
 
Huko tunduru imebidi mkurugenzi awabadilishe vituo watendaji Kata karibia wote .wanaogopa kurudi Toka waliondoka siku uchaguzi hawajarudi .wamegoma kurudi walikoshiriki uharifu waliiba Sana na kuyangaza walioshindwa.
Si kwa watu hawajui wameibaje Ila washiriki wa wizi wamekimbia adhabu ya waliowaibia.
Wake ambao waliwekeza Mali zao zimeteketea.kuna haja ya waliowashawishi kuiba wawalibe.
 
Mkuu kama ingekuwa ukishinda Mahakamani, basi unapewa Ubunge, nadhani zingefunguliwa kesi nyingi, na kwa mambo yalivyokuwa wazi sana, nina imani CCM wangepoteza majimbo mengi.
Lakini, ukishinda Mahakamani, utakutana tena naTume hii hii, Wakurugenzi walewale, Polisi hawahawa! Yatajirudia yale yale ya uchaguzi wa marudio, akina Waitara "walivyoshinda kwa kishindo", na kumpoteza mtoto Aguilina bila sababu!
 
Mkuu unaishi Tanzania hii hii tunayoishi?!Kwa nini unataka kesi ya Tumbili ipelekwe kwa Ngedere?Yaani kwa nini unataka kesi ya mwizi wa kura ipelekwe kwa msimamizi mkuu wa wizi wa kura?Unaelewa kuwa vyombo vya sheria pamoja na polisi ndiyo walikuwa wasimamizi wakuu wa wizi wa kura na waliokamatwa na kura fake walikuwa ni wasimamizi wasaidizi wa wizi wa kura?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…