Kwanini Sokoine ndio Waziri Mkuu anayeenziwa kuliko wote Tanzania?

aka2030

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
2,657
Reaction score
3,679
Hakuwa waziri mkuu wa kwanza, Ila cha ajabu ndio waziri mkuu anayeenziwa kuliko wote hebu tazama,
1. Uwanja wa sokoine mbeya
2. Sokoine University of agriculture
3. Sokoine road Arusha/Dar es salaam
4. Sokoine secondary
5. Sokoine regional refferal hospital lindi
6. kituo cha afya sokoine Singida
7. Sokoine house Tamisemi dodoma

Hayo ni baadhi tu. Yaani ameenziwa kuzidi hata baadhi ya Marais na mawaziri wakuu.
 
Kwasababu ndiye waziri mkuu wa kwanza kufa.
 
Sababu alifariki akiwa madarakani tena ghafla kwa ajali ya gari, na pili uongozi wake unaweza ukaufananisha fananisha na uongozi wa JPM !!
 
Sokoine Memorial High School - Pale alipopatia ajali imejengwa shule kubwa ya serikali ya advanced. Mambo mengine ni nyota ya mtu haya yote yamefanyika wakati hayupo. Viongozi wengine wamepeana majina wakiwa hai kama Soko Kuu la Ndugai.
 
Alikuwa kama jiwe, alikuwa anawachukia wenye nacho na kupora mali zao na kuwapa kesi za uhujumu uchumi
Mungu sio Athumani naye akafa kabla hajafanya uonevu zaidi
Ama kweli Wazuri hawafi
 
Nadhani Vitu Vingi Vya Maana vilianzishwa au kujengwa katika kipindi akiwa Waziri Mkuu..na kwa Heshima ikabidi viitwe jina lake...siku hizi siasa zimekua nyingi...na viongozi walioko madarakani Wana wivu sana...wanapenda wavume wao tuu...any attempt kumheshimisha mwanasiasa mwingine inakua nongwa kwa sababu Viongozi wote wenye maamuzi ya juu bado Wana political ambitions zao, as a result juniors wote ambao kimsingi ndio hupendekeza majina ya kuita Taasisi au mtaa Fulani wanakua waoga kupendekeza jina la mtu ambaye hana nguvu tena kisiasa....kwa mfano...can you imagine Makamba apendekeze mradi wowote mkubwa ulioko kwenye Taasisi anayoiongoza uitwe Pinda au Magufuli?!....NEVER....Lakini yuko tayari ata kuita mitungi ya gas ..SAMIA CARE CYLINDERS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…