Kwanini somo la Civics ndilo pekee ambalo haliundiwi combination "A" level katika masomo saba ya msingi Kidato cha Nne?

Kwanini somo la Civics ndilo pekee ambalo haliundiwi combination "A" level katika masomo saba ya msingi Kidato cha Nne?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Kwanini somo la Civics ndilo pekee ambalo haliundiwi combination "A" level katika masomo yale saba ya msingi kidato cha nne? What's the logic? Aren't they diplomats?

images (5).jpg


Wale wanaopata As za somo hili la Civics katika matokeo ya Kidato cha Nne wakiwekewa mkazo stahiki si ndio watafaa kuja kuwa wanadiplomasia wazuri wa Tanzania hapo baadae kama ambavyo tunaamini kuwa wanaofaulu vizuri Biology ndio watakuwa madaktari wazuri? Au wanaofaulu vema Physics watakuja kuwa engineers wazuri wa Tanzania hapo baadae?

Unakuta mwanafunzi wa kidato cha nne anakuchambulia vena masuala ya ECOWAS, ECOMOG, SADC, Structure nzima ya UN kama ambavyo mwanafunzi wa Biology anavyokuchambulia digestion system ya mwanadamu.

Ukijaribu kufanya utafiti wa haraka haraka tu kutoka kwa hawa walimu wanaotufundishia wadogo zetu ambao ndio taifa la kesho unaweza ukagundua suala hili mara moja.

Mwalimu wa History atakwambia alisoma HGK, HGL, HGE, HKL

Mwalimu wa Geography atakwambia alisoma EGM

Mwalimu wa Kiswahili atakwambia alisomea HKL

Mwalimu wa Biology atakwambia alisomea PCB

images (6).jpg


Kwanini hawa vipanga wa Civics hawapewi attention inayotakiwa kama hao wa HGL na HGK? Kwanini kusiwe na combination ya HCL (History, Civics na Language) au HCK (History Civics na Kiswahili)?

Kuna mtoto mmoja wa shangazi yangu alimaliza chuo mwaka 2017 alisomea Accountancy UDSM.

Huyu dogo katika ufaulu wake wa kidato cha nne alipataga As mbili moja ya english na nyingine ya Civics pamoja na Cs saba.

Ingawa amesomea uhasibu ila yeye ukimkuta ameingia kwenye internet au anasoma vitabu basi ni vya siasa za kimataifa tu (SADC, AU, UN) na sio taaluma yake ya uhasibu kwa maana anakwambia hana interest nayo kabisa ingawa "A" level alisoma combinations ya ECA.

Kwanini Tanzania isianze kusuka wanadiplomasia kuanzia wanaofaulu vema somo la Civis kidato cha nne?

Mbona somo la computer linasomwa na wanafunzi wote huko vyuoni lakini wale wa ICT na Computer Science wanalisoma kwa undani zaidi? Kwanini Civics lisisomwe na wanafunzi wote lakini kuwe na combination ya wabobezi watakaolisoma kwa undani zaidi?

NJE YA MADA KIDOGO: Kwanini hutokea mtaalamu wa fani nyingine (sheria, uhasibu, mhitimu wa form four tu) anakuwa wanasiasa mzuri na bora kuliko yule aliyesomea "Political Science"? Sababu ni nini?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kuna sehemu tunafeli kama taifa ndio maana wazi kama kina Mbowe na Lissu eti ndio wanasiasa simply watu hawajui elimu ya uraia vema
 
Ukitaka iwe na combination means alie muuguzi hatojua uraia (civics) hivohivo na kwa mwalimu.

Maana ya kuwekwa civcs bila comb yoyote means isomwe kwa wote na ni lazima sio ombi au hiari kama unavyojichagulia hizo EGM, HKL, HGE, n.k

Na ndio maana O level inaitwa civics ni lazima isomwe na wote ila
A level inaitwa general study hiyo ni kwa wote sio ombi au hiari.
 
Somo la uraia NI somo linalohusu raia na wajibu wao pamoja na haki zao
Maarifa unayopata Katika Hilo somo i hayajengi taaluma au hayamuandai mlengwa kuwa professional Katika eneo fulani
Bali Kama raia ufahamu wajibu wako NI Nini na haki zako NI zipi
na general knowledge ya Mambo mbalimbali Kama usalama nk

Masomo mengine yanaandaa wataalamu mfano madaktari, ma engineer, walimu, wahasibu, wachumi nk
 
Hata ukisoma definition NI
The study of the rights and duties of citizenship

Ndio Mana hata mwalimu wa biology anaweza kufundisha civics
Au mwalimu wa somo lolote
 
Somo la uraia NI somo linalohusu raia na wajibu wao pamoja na haki zao
Maarifa unayopata Katika Hilo somo i hayajengi taaluma au hayamuandai mlengwa kuwa professional Katika eneo fulani
Bali Kama raia ufahamu wajibu wako NI Nini na haki zako NI zipi
na general knowledge ya Mambo mbalimbali Kama usalama nk
Mbona kuna masuala ya kimataifa ndani ya somo la civics hautaki kuyaongelea?...
 
Mbona kuna masuala ya kimataifa ndani ya somo la civics hautaki kuyaongelea?...
Ukisoma vizuri nimeweka not
Siwezi kutaja topics zoote za civics lakini masuala yote hayo ya diplomasia bado ni masuala ya raia na haki zao
NI somo linalokupa uelewa mpana zaidi Katika masuala yote yanayomhusu raia
 
Ukisoma vizuri nimeweka not
Siwezi kutaja topics zoote za civics lakini masuala yote hayo ya diplomasia bado NI masuala ya raia na haki zao
Unapozungumzia raia na haki zao ni kama unaongelea "local issues" tu mkuu...
 
Kwani unaposema masuala ya kidplomasia unaweza kuwakwepa raia?
Bado tunazungumzia mahusiano ya raia kimataifa
Na Kama NI mahusiano basi haki na wajibu was raia upo pale pale
 
Kweli hii ingekuwa inatutengenezea hata watendaji na maafisa tawala. Baadae wanasoma Bachelor of leadership and diplomacy inapendeza kweli.
 
Somo la uraia NI somo linalohusu raia na wajibu wao pamoja na haki zao
Maarifa unayopata Katika Hilo somo i hayajengi taaluma au hayamuandai mlengwa kuwa professional Katika eneo fulani
Bali Kama raia ufahamu wajibu wako NI Nini na haki zako NI zipi
na general knowledge ya Mambo mbalimbali Kama usalama nk
If that's the case, kuna haja gani ya kufanya mitihani ya civics na kuweka madaraja ya A mpaka F?
 
Local issues?
Mahusiano ya kimataifa yanaweza kuwa managed vip Kama watu was mataifa hayo hawajui haki na wajibu wao
HAKUNA haja ya kubisha Rudi kwenye definition ya civics
Hakuna definition moja ya civics kama alivyokukaririsha mwalimu wako mkuu. Tatizo lako unakariri sana maisha ndio maana swali moja likipindwa kidogo darasa zima wana-fail
 
Back
Top Bottom