Kwanini Sweden (Sida) hawakutupa pesa FY2020|21 na badala yake wametupa FY2021|22 mwaka mmoja baadaye?

Nikikumbuka kuwa alikuwa msaidizi lakini mawazo yake ni tofauti na mwenzake basi ndivyo ninavyowafikiria kuwa hata ndani ya ndoa wanawake mipango yao ni tofauti na waume ndani ya nyumba.
 
Tatizo sio kujenga madarasa!Tatizo ni elimu Mbovu isiyo na future hapa nchini!hao vijana wakishasoma wanajiarije kama elimu yenyewe mfu isio na macho??Ona wimbi la vijana wasio na ajira mtaani !!tutafanyaje???
 
magufulia alikuwa anatufundisha kujitegema, lakini watu wanalilia misaada. Unadhani kama China ingetegemea misaada ingekuwa hapo ilipo leo?

Waswahili wanapenda vya bure sana; inainikumbusha ule msemo kuwa "nikienda nje nianrudi na kibaba!"
Uliwahi kumsikia Magufuli akikataa msaada? Kwani nani hajitegemei? Ukipewa msaada utakataa??
 
Tatizo sio kujenga madarasa!Tatizo ni elimu Mbovu isiyo na future hapa nchini!hao vijana wakishasoma wanajiarije kama elimu yenyewe mfu isio na macho??Ona wimbi la vijana wasio na ajira mtaani !!tutafanyaje???
Toa maoni ya kuboresha mkuu
 
Uliwahi kumsikia Magufuli akikataa msaada? Kwani nani hajitegemei? Ukipewa msaada utakataa??
Hili swali niliwahi kulijibu hapa. Kupokea msaada ni kitu kimoja, na kutegemea misaada ni kitu kinginee. Tofautisha hayo mawili. Sasa hivi filimbi ni za kutegemea misaada kuwa tunapata missada kiasi gani, jambo ambalo halitakiwi kufanywa na serikali.
 
Mtegemea cha kupewa hufa masikini.
Hela ni za mwenye hela, akikupa, kukunyima ni hewala tu.
 
Hili swali niliwahi kulijibu hapa. Kupokea msaada ni kitu kimoja, na kutegemea misaada ni kitu kinginee. Tofautisha hayo mawili. Sasa hivi filimbi ni za kutegemea misaada kuwa tunapata missada kiasi gani, jambo ambalo halitakiwi kufanywa na serikali.
Toa mfano wa hiyo filimbi?
 
sasa lkn hii laana ya kuwategemea mabeberu siku moja humu ndani tutakuja kusutana.mkono unaotoa unabarikiwa zaidi ya ule unaopokea.misaada hudumaza uchumi kwani hakuna taifa lolote litoe pesa burebure tu wakati wao wanawakamua kodi wananchi wao.mbona matajiri wa hapa kwetu hawatoi misaada kwa watu maskini.hawa mabeberu ndo kusema wanatupenda sana waafrika mpaka wagawe pesa zao bure tu!nimeamini huo ugonjwa kuja kufutika kwa watanzania it will take another decade.haya yetu macho na masikio.
Tutarajie misaada mingi sana wakati huu wa Samia

Wazungu wanataka haki tu walete pesa na haki ni asili ya Rais wetu

Uchumi utachangamka sooner

Hakika hakuna kama Chief Mkuu Hagaya
 
Safi sana Pacha,

Tuendelee kulivunulia Taifa kazi njema na nzuri za mama Samia,

Nakupongeza sana kwa makala hii ya kisomi sana,

Endelea kumuunga mkono Rais Samia
 
Wewe unajua niwao wametufanya sisi kuwa masikini hata leo?

Wamechukua vyetu vingi sana hivyo sioni shida kuturudishia vyetu

Chapa kazi mkuu Jabali la Siasa
 
Dogo ananiharibia jina

Inabidi nibadili sasa

Anatoa narudi kali mdomoni Kwa Tuhuma ambazo akifinywa vizuri atashindwa kuzisimamia
Nikweli dogo anashida sehemu,

Kiwango chake cha hasira si cha kibinadamu kabisa
 
Hili swali niliwahi kulijibu hapa. Kupokea msaada ni kitu kimoja, na kutegemea misaada ni kitu kinginee. Tofautisha hayo mawili. Sasa hivi filimbi ni za kutegemea misaada kuwa tunapata missada kiasi gani, jambo ambalo halitakiwi kufanywa na serikali.

Tatizo lako ni kauli tu?

Hakuna kipindi ambacho Tanzania haijawahi kutegemea misaada. Hata awamu ya kwanza mambo yalipokuwa magumu sana, muasisi wa juhudi za kujitegemea kwa dhati, Mwalimu JKN, aling’atuka kukwepa dhahama ya kusaini mkataba na IMF ili kuwezesha misaada na mikopo nafuu kutiririka nchini. Alitoa baraka zake kwa mrithi wake, AHM amwage wino kwa kuelewa kuwa bila hivyo nchi ingeangamia.

Awamu ya tano, Lissu alishambuliwa sana kwa kukosa “uzalendo”, kwa kampeni zake Ulaya na Marekani “kuharibu sifa ya nchi” na kuomba inyimwe misaada. Aidha, kila msaada au mkopo wa “mabeberu” ulipopatikana ilikuwa habari muhimu kwenye prime time ya media zetu.

Nilichoona, Magufuli alikuwa akitukuzwa sana kwa kauli zake kali zilizojaa propaganda na ile “misimamo isiyoyumba” ya kuponda mabeberu. Eti “sisi ndio tunatakiwa kuwapa misaada”; “sisi ni matajiri; tunaweza kuwa donor country”! Mtu anadiriki kusema “Magufuli kwenye suala la maendeleo alikuwa na msimamo na uthubutu; anaanzisha miradi ya matrilioni bila kujali hela itatoka wapi”!

That was pure DELUSION! Ni maruweruwe wanayopata baadhi ya watu duni ambao ghafla hujikuta wana dhamana na madaraka yote ya kusimamia na kutumia matrilioni ya hazina ya taifa bila watu wa kuwahoji. Ni mtu wa aina hiyo anaweza kuivimbia hata Marekani na kuitambia kuipa misaada huku bado watoto wake kibao wanasoma chini ya miti.

Naona manazi wa awamu ya sita nao wanaongeza kasi ya maruweruwe yao kama vile sisi wanaotuandikia hizi propaganda uchwara ni mazombie.

Anyway, hii yote ni CCM syndrome ya kutaka kuelekeza Watanzania kwenye ibada za kutukuza viongozi badala ya kufuatilia uwajibikaji na utawala bora. Siku hizi hata chama chao wanakiweka kando mbele ya personality cults.
 
Hapo kuna sacrifice lazima itakuwa imetolewa huwezi kupata hiyo pesa bure bure tu namna hiyo.

Huko tuendako kuna concessions sana kwenye mambo ya demokrasia na haki za binadamu. Hii kamata kamata ya akina Sirro na genge lake lazima ifikie ukomo na uhuni kama ule wa Magufuli kwenye uchaguzi hautakuwepo asilani wala kubambikia watu vyesi feki ili kulinda udikteta ndio unamalizika hivyo.

Itakuwa ni pigo kubwa kwa kile chama kinachopenda kubebwa-bebwa na wale waabudu sanamu kwa ujumla.
 
Ni kweli mkono wa Mungu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Umeandika ukaandika ila CCM na serikali yake tunapokea misaada ila kamwe hatutegemei misaada,


#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…