Kwanini Tanzania tunapata watalii wachache kulinganisha na vivutio tulivyonavyo?

👏👏👏 knowledge ya utalii Tanzania inachukuliwa poa tena sana tu..... Bodi ya Utalii Tanzania M/Kiti ni Judge sidhani kama bodi ya Wanasheria M/Kiti ni Daktari wa binadamu.
 
Siku mkija kujua utalii sio tu kuwa na Simba, swala au tembo wengi ndio mtajua kwanini kwanini utalii tanzania unasua sua...

Kuna nchi Zina Utalii wa Beach tu na zinapata wageni wengi kuliko Tanzania yenye mamilion ya sokwe na Simba...

Jiulize kwanini!!! Siku tukija kufuta huo mtazamo nchi hii itafika mbali.
 
Mwendokasi tu imewashinda
 
Exactly pricing ndio tatizo. ...... na ndio maana tunashishindwa na kuhusu Serengeti wageni wengi wanaokuja TZ wanaenda huko sababu ndio tunayoiyaja. na kuitukuza.
Ukienda Zanzibar, room ya hovyo hovyo kwenye vihoteli vyao utaambiwa laki. Chumba cha short time hapa lodge za bongo unalipa 15 unaondoka Zanzibar unaambiwa 100,000.

Mauritius, Comoro, Seychelles, Reunion na visiwa vingine wanapiga hela kwenye utalii hakuna mfano.

Seychelles njia kuu ya uchumi ni utalii, mandege makubwa makubwa yanatua pale kila siku lakini jirani zake tu Zanzibar wameshindwa.
 
Kuna mzungu mmoja aliwahi kuniuliza mbona chips mayai mtaani ni 2,500 hadi 3,000 lakini Nyerere Airport ni 18,000. Kwa nini kuna tofauti kubwa hivyo na hizi za mtaani ni tamu sana?

Mtu kama huyo mnamjibu vipi?

Ungemjibu kwamba "hayo ni maagizo toka juu". Ova!
 
Kule Quatar kuna maelfu ya watalii wanaenda kumuangalia "salt bae" anavyorusha chumvi kwenye nyama Choma kwa kutumia mkono na kiwiko Chake...

Endeleeni kuamini utalii ni swala, mbuzi, Simba na nyumbu.
 
Wewe unafikiri hizo standard hazipo?? Unajua zamani kulikuwa na state travel services??
He hotel ukiambiwa in nyota 1, 2, 3 ,4, 5 si ndio standard zenyewe??
 
Hatuna viongozi creative katika sekta hiyo period. Tunatumia akili zile zile na njia zile zile.we don't go global, kuna watu tumejitolea kuutangaza utalii bila ubalozi tukasanda. No support hakuna njia mpya za kufanya mambo. No exposure. Tumeridhika
 
Umeng'ata Lamdmark wakati sie tunaona ndio bongeee la hoterrriii
 
Tanzania wanacheza tunatania hatujitangazi hopping that tuna vivutio vya kutosha watakuja tu
Na wakija huduma ni mbovu, mapokezi yanaanzia Airport, kunakuwa na immigration desk kwa watalii wasikae muda mrefu kwenye foleni ya visa. Wakitoka nje wakute wahudumu wanawasubiri kwa tabasamu , usafiri upo wa kuvutia. Wapewe mpangilio wa ratiba.
 
Kuna ujuaji na ukiritimba mwingi sana katika sekta ya utalii. Plus serikali na viongozi wake wanazima ubunifu kwa kuingilia mambo mengi sana na kutokaa na wadau kujua wawasaidie vipi kupiga hatua...
 
Wakiruhusu na SEX TOURISM watapiga dough hatari sana.
Tatizo sex tourism wanakuja wabibi ila wangekiwa wanakuja wadada wakali.... Mbona hata mimi ningekuwapo katika biashara.
 
Mimi usifikiri kwamba entry fee ni jambo baya labda rate, lakini ukiwa uingereza e.g. kuingia Windsor castle ni £10.00 , ukitoka hapo madame tausand napo kiingilio sikumbuki how much lakini ukiwa na family unaiona £100 inakwenda, ukienda museum the same, bus tour na boat nayo ni pesa , hujaenda something like marine park etc , na kujifanya hivyo labda Windsor pekee yake siku imekwisha next day hizo sehemu zingine uzipitie u might need two day , so say three day na ya Windsor, hapo hujazungumzia miji mingine, au viwanja vya mpira kama Emirates wa Arsenal etc na train ticket a day travel ticket all zones £ 12.00 etc , bado kwa sisi waswahili hujaingia maduka ya nguo ,viatu etc na ticket za ndege na kukuongezea na accommodation?? Chakula per person kwenye hizi fast food at minimum £5 say breakfast , £10 lunch na dinner the same. Sasa £10 x 3000= 30,000.00
Kwa dinner .

Ninachoona hatupo creative enough kumfanya mtu atumie na aone muda aliokaa hautoshi ili siku nyingine ajione ali miss kitu , awe na hamu ya kuja tena au a recommend mtu mwingine aje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…