Kama sekta binafsi hawawezi, serikali naishauri inunue mabasi madogo na kutoa kuduma bure kwa watalii. Watangaze package tours.
Nimeona mabasi ya bure Asia, unapelekwa kufanya shopping maduka mbali mbali, au unapelekwa mahotelini bure. Itawasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kuuza bidhaa zao kama mabasi yakisimama kwao. Pia inakuwa rahisi kwa mgenu kutembea bila ya kupoteza mda.
Kuna mito ya maji moto (hot spring) Morogoro nimeona, yanaitwa onsen kwa Kijapani. Hii ni biashara kubwa hapa kwa kuwa maji yake ni mazuri kwa afya ya binadamu. Kama sehemu hizo zikizungushiwa hoteli, watapata wateja wengi sana.
Hapo DSM, kama Oysterbay beach ingejengwa vizuri, watalii wengi wangekuja kuota jua hapo. Sio kila mtalii anataka kuona mlima na wanyama.
Ukienda Pattaya, Thailand au Bali, Indonesia, kuna bahari kama Oysterbay. Package tour zao za wiki moja kutoka Japan hazizidi $700 kununua usafiri, hoteli na chakula. Bali na Pattaya wanavuta watalii milioni 15 kwa mwaka kuota jua. Sisi tunavuta milioni 2 tu kwa nchi nzima na tuna vivutio bora zaidi!