Kwanini Tanzania Walimu wenye Masters hawatambuliwi kimasilahi?

Unafahamu utoshelevu wa elimu Mkuu? Elimu inayotosha ni Ipi?
Soma Katiba ya Taifa lako vizuri.
 
Wakati work out-put yao ni ile ile
Work output yao haiwezi kuwa ile ile. Binafsi naamini elimu degree ya kwanza ngazi ya ualimu (kwa zama hizi) haitoshi kutoa elimu bora shule za sekondari. Miaka ya hivi karibuni nimeshangaa wanafunzi wanakuja first year vyuoni na wamefaulu division one hadi two lakini ukiangalia performance yao ile semester ya kwanza unapata walakini kama hawa watoto walipata maarifa sahihi ya kuwawezesha kuwa na sifa.za chuo kikuu. Hawajui kujenga hoja, hawajui kujisomea vitabu, wengine hawajui kabisa hata kunyoosha mwandiko achilia mbali kujenga hoja kwa lugha ya kiingereza.

Japo kuwa na elimu ya masters haiwezi kuwa sifa pekee ya kufundisha sekondari miaka hii, lakini nahisi utitiri wa waalimu wengi wenye degree unalazimisha, walau kwa mazingira ya sasa, umuhimu wa walimu wenye viwango vya juu zaidi ili kunusuru kiwango cha elimu kinachotolewa huko sekondari.
 
Nadhani serikali inapaswa kuharakisha uhamisho wa walimu wenye sifa ili kwenda kutumikia elimu yao sehemu husika

Kusoma sio kwaajili ya maslahi yao bali ni kwaajili ya kuitumikia elimu

Kuhusu uhaba wa walimu kutolewe wito kuvutia wanafunzi kusoma zaidi ualimh wa sayansi maana masomo ya sanaa na biashara tunao wengi sana
 
Upo sahihi 🙏🏼
 
Elimu haijawahi tosha mkuu...Tafuta nafasi ukasome.
 
Mzee una Masters? Kama ulifaulu zaidi ya 3.8GPA degree, na ukapata 4.0 GPA masters wewe ni hot cake... omba kuhamia kwenye vyuo.
Mimi Ni mdau wa Elimu tu natoa maoni yangu juu ya kuuboresha ualimu na Elimu...am free activist
 
Mzee una Masters? Kama ulifaulu zaidi ya 3.8GPA degree, na ukapata 4.0 GPA masters wewe ni hot cake... omba kuhamia kwenye vyuo.
Vyuoni nako si kwamba ukishakuwa na 3.8 basi automatically unakuwa mwalimu wa chuo kikuu. Kuna mchakato, lazima kazi itangazwe, utumishi wasimamie interview process, wataaply kibao wakati nafasi zipo mbili au moja. Na pia hoja kuu ni kwamba walimu wenye masters watambuliwe sekondari hata kama hawana gpa 3.8.
 
Kwasasa vyuoni ajira ni kuanzia master Ila before walikuwa wanachukua first degree then baada ya miaka miwili unasomeshwa masters na chuo na ukipata chin ya GPA Yao. Basi kibarua kinaishia hapo.
Otherwise upo sahihi Sana mkuu kwa hoja ya Walimu wenye Masters watambuliwe
 
Huko vyuoni nafasi ni nyingi sana.. anaweza omba kuhamia na akapata... na kwa kada za Assistant Lecturer watu si wengi kama unavyosema maana nafasi huwa re-advertised mara nyingi maana kupata watu wa vigezo hivyo si mchezo ndugu.
 
Hata ukiwa na PhD wataangalia GPA ya 3.8 undergraduate. Vyuoni wanaajiri kuanzia tutorial assistants (degree moja but uwe na 3.8 gpa), assistant lecturer ( masters but uwe na 3.8 undergrad na 4.0 masters), na PhDs (vigezo ni vile vile). Anyway nina walakini na vigezo hivyo lakini kwa sasa hali ndivyo ilivyo.

Hoja yako kuu na ambayo naiunga mkono ni kwamba hakuna sababu ya kutotambua walimu wa masters degree kimaslahi. Kuna viujinga vingi vinaendelea sekondarini kuanzia kiwango cha maarifa yanayotolewa na yanavyotolewa na mojawapo ya sababu za ujinga huo ni kulazimisha walimu kubaki na degree moja. Utadhani degree moja ya miaka ya 1960s ni sawa na degree moja ya 2020s.
 
Huko vyuoni nafasi ni nyingi sana.. anaweza omba kuhamia na akapata... na kwa kada za Assistant Lecturer watu si wengi kama unavyosema maana nafasi huwa re-advertised mara nyingi maana kupata watu wa vigezo hivyo si mchezo ndugu.
Yeah upo sahihi. Sio wengi wana Masters level degree na kuwa na sifa za kiGPA. But dont think pia kama vyuoni kuna nafasi bwerere kwamba ukishakuwa na sifa za assitant lecturer basi utapata nafasi automatically.
 
Maslai ya mwalimu yanatakiwa kupimwa kwa ufanisi wa kazi siyo karatasi za vyuoni ... kwa akili hizi wasomi wa tz ni wapumbavu sana.... yani wanawaza maslai kwa kutumia karatasi za darasani badala ya ufanisi kazini
 
Maslai ya mwalimu yanatakiwa kupimwa kwa ufanisi wa kazi siyo karatasi za vyuoni ... kwa akili hizi wasomi wa tz ni wapumbavu sana.... yani wanawaza maslai kwa kutumia karatasi za darasani badala ya ufanisi kazini
Mbona unapaniki Sana upo sawa kweli.. jitathimin kama upo sawa..vitu Kama stress huwa vinaongeza jazba kwenye vitu vidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…