Kwanini Tanzania Walimu wenye Masters hawatambuliwi kimasilahi?

Kweli network hapa ni not reachable

Sawa kiongozi umeeleweka
 
Nyie mnaosema Maafisa wanaogopa walimu wenye masters watawapora vyeo vyao... Mnitajie wapi huko Afisa elimu wilaya au hata Afisa taaluma amewahi pokonywa cheo na mwalimu mwenye Masters au PhD..?
Serikali karibia zote Duniani zinaajiri mtu na zinalipa mshahara na kutambua elimu kuanzia Certificate mpaka Degree...
Masters ni added advantage ikitokea nafasi fulani inahitaji mtu mwenye Masters ndipo anaangaliwa mtumish mwenye uwezo wa kuimudu nafas hiyo na elimu yake ya masters... Duniani kote Masters ni managerial course inayomuandaa mtu kuwa kiongoz...
 
Masters inaongeza tija gani kwenye kufundisha shule ya msingi na sekondari.

Kwa kada zingine kama madaktari, inaongeza tija kwa kwa maana unaanza kutoa huduma za kibingwa (specialist).

So onyesheni tija kwanza sio makaratasi.
 
Kwetu jambo hili haliko vizuri kabisa. Linawakatisha tamaa vijana wetu.
Mwalimu wa akihitimu master degree anaongezewa vidato viwili tu mf TGTS F1 TO TGTS F3; wakati muundo wa kazi unabaki ule ule.
Huu ni upuuzi kabisa.
Huenda walioko huko juu wanawaogopa hawa vijana wasomi.
 
Masters inaongeza tija gani kwenye kufundisha shule ya msingi na sekondari.

Kwa kada zingine kama madaktari, inaongeza tija kwa kwa maana unaanza kutoa huduma za kibingwa (specialist).

So onyesheni tija kwanza sio makaratasi.
Kwani degree inaongeza tija gani kwenye kufundsha msingi na sek. Tuanzie hapo ili tupate jibu la swali lako
 
Unaongea tu hebu jaribu kujiridhisha na hoja zako usitumie uzoefu kujibu hoja hivi unajua miaka ya nyuma kidogo hapa Tz hata degree yenyewe ilikuwa haitambuliki, usiseme serikali zote Duniani hazitambui Masters si kweli hebu jaribu kugoogle nchi zifuatazo.. Uganda, Kenya, Zimbabwe, Nigeria, south Africa, zambia...huko mtu kuwa mwl ni Kama ilivyo Tz kwa mtu kuwa mhadhri, nafas zinatangazwa na watu Wana wafanyiwa interview na kila Elimu Ina Mshahara wake kasoro tu kwenye hzo nchi certificate haitambuliki
 
Chukua takwimu vyuoni.
Master za Ed pekee zinazidi 3000 kwa mwaka.
Mara miaka 5. Na wanaosoma ni vijana.
Wapo wengi value yao ishashuka.
Vijana watafute njia nyingine ya kutokea maisha
Wakati CPA Kwa Mwaka hazizidi 500, advocates Kwa mwaka 600
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…