Kwanini tarehe ya Pasaka hubadilika?

Kwanini tarehe ya Pasaka hubadilika?

Hakuna mwezi ulioongezwa Mkuu!
It was Just a pinch of changing the day..
Kutoka Julian Calenda kwenye Gregory ni kama wiki kadhaa tu zilikuwa skipped not kuongezwa
Unataka kuniambia kalenda ya sasa ya kiyahudi ni sawa na ya zamani ?
 
UKo sawa kabisa Na hilo sipingi..
Lakini nichosema kulikuwa na haja gani ya Kubadili jina Kutoka Paska kuwa Easter?

Kama Mungu aliamuru Ifanyike Tarehe anayotaka Yeye Then kwanini Walibadilisha??
Kwani Easter maana yake ni nini?
 
Passover (Paska) ni Kumbukumbu Ya Mikate isiyotiwa chachu na Divai na ilisherekewa kama Kumbukumbu ya ukombozi kutoka Misri kwenda kanaani..

Easter ni Kumbukumbu siku ya Kufa na kufufuka kwa yesu..

Mkuu hizi siku ni Mbili tofauti tusipindishe kwa wale wasiojua
Bro, Easter haihusiani na pasaka na haipo katika Biblia. Binafsi sijui ilipotokea na wala sijuagi maana yake labda unifundishe leo kiongozi. Ila nifahamucho, tunakumbuka Ukombozi pitia "damu ya mwana kondoo". Kama ambavyo damu ya Mwanakondoo iliwaokoa wana wa Israel toka utumwani Misri, ndivyo nayo damu ya mwana kondoo wa Mungu imetuokoa na kututuoa utumwani. Mengine siyajui na sitaki kuyajua. Hata ukinifundisha, nitayaachia hapa hapa JF. 😀😃😄😁😆
 
Great Thinkers; Leo nina swali ama muono wa hizi sikukuu za Kiblblia.

Tuanze na kitabu cha Kutoka 12: 1 Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia,
2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.
3 Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;
4 na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.


Mwaka huu tumesheherekea Pasaka mnamo kuanzia tarehe 29 Machi hadi 01 April. Mwaka 2023 Pasaka ilianza tarehe 07 April hadi 09 April.
Kuna kitu hakipo sawa kama endapo tutatumia akili zetu vizuri tutaweza kung'amua kuwa Wazungu wameingiza upagani kwenye Neno la Mungu.

Nini Mtazamo wako kwenye shifting dates za Pasaka.
Unatumia Calendar gani?
 
Oooh..kuna sehemu niliona kama Nissan ni mwezi march kumbe ni mwezi wa kwanza..ahsante Mkuu
NIssan ni mwezi wa kwanza wa kiyahudi na March ni mwezi wa Tatu wa Kirumi,
ni kama mtu aseme mwezi wa Shabani ni mwezi February..

Sio sawa kwa sababu February ni mwezi wa kirumi na Shabani ni mwezi wa Kiarabu (Kiislamu)
 
Mkuu wanaleta Loggical fallacies kwenye Facts inayoonekana 😅😅
Mkuu, unajua msingi wa mada ni ku-attack ukristo. Obvious dhidi ya dini nyingine ikiwemo na uislamu.

Sasa mfano, Idd el fitri chanzo chake ni kipi? Na je kama haipo kwenye quran, ina uharamu wowote kwa waislamu?
 
NIssan ni mwezi wa kwanza wa kiyahudi na March ni mwezi wa Tatu wa Kirumi,
ni kama mtu aseme mwezi wa Shabani ni mwezi February..

Sio sawa kwa sababu February ni mwezi wa kirumi na Shabani ni mwezi wa Kiarabu (Kiislamu)
Na hawa wa orthodox nao imekaaje maana wana tarehe zao pia za pasaka na Christmas , nao ni wakatoliki
Screenshot_20240401-092728_Samsung Internet.jpg
Screenshot_20240401-092754_Samsung Internet.jpg
 
Pasaka ni agizo. Kuabudu Jumapili ni kukumbuka siku aliyofufuka kwake Yesu ni sawa tuabudu katika mwanzo mpya wa siku baada ya kuishinda mauti. Kusheherekea kuzaliwa kwa Kristo ni Agizo la malaika "Furaha kuu kwa ulimwengu, kwani leo amezaliwa Yesu aliye mkombozi wa ulimwengu" Luke 2:10.

Kuhusu "siku na majira ya sherehe", hatusheherei siku wala majira ila "tunasheherekea tukio". Nafikri nami nimechangia kidogo mkuu.
Upo sawa kabisa mkuu.
 
Unataka kuniambia kalenda ya sasa ya kiyahudi ni sawa na ya zamani ?
Hapana sio sawa mkuu..

Calenda ya zamani ya kiyahudi ilikuwa Pure Lunar calendar,Baada ya wayahudi Kuwa utumwani Rumi waliadapt solar calendar..

Kwahyo Calendar yao mpya Ilikuwa na Lunisolar structure..

So kalenda iliikuwa lunisolar ikitaka Matumizi ya Vyote Mwezi na Jua. So Ina miezi 12 ya lunar na miezi miwili au mitatu ya kuadjast solar kama sijasahau sana
 
Mkuu, unajua msingi wa mada ni ku-attack ukristo. Obvious dhidi ya dini nyingine ikiwemo na uislamu.

Sasa mfano, Idd el fitri chanzo chake ni kipi? Na je kama haipo kwenye quran, ina uharamu wowote kwa waislamu?
Ooh bhasi kama Msingi wa Mada ni kuattack watu fulani Sio sawa hata kidogo..
Ila kama ni Njia ga kuelimisha Ni sawa!

Ila Hata waislamu pia na wenyewe wana sherehe nyingi ambazo si Za kidini
Kama maulidu nabbi (Maulidi) ("Kuzaliwa kwa mtume")


Kwenye Uislamu Idd Ilikuwa na chanzo ni Kusherekea baada ya Funga..Ukisoma kwenye Quran

Al-Baqarah aya ya 185

شَهْرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِىٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلْقُرْءَانُ هُدًۭى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٍۢ مِّنَ ٱلْهُدَىٰ وَٱلْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ ٱلشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍۢ فَعِدَّةٌۭ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِكُمُ ٱلْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ ٱلْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا۟ ٱلْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا۟ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

kwa Kingereza

The month of Ramadhan [is that] in which was revealed the Qur’an, a guidance for the people and clear proofs of guidance and criterion. So whoever sights [the new moon of] the month, let him fast it; and whoever is ill or on a journey - then an equal number of other days. Allah intends for you ease and does not intend for you hardship and [wants] for you to complete the period and to glorify Allah for that [to] which He has guided you; and perhaps you will be grateful.


Kiswahili:

"Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu (Kwa kumaliza masiku) kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru."
 
Mwaka huu tumesheherekea Pasaka mnamo kuanzia tarehe 29 Machi hadi 01 April. Mwaka 2023 Pasaka ilianza tarehe 07 April hadi 09 April.
Kuna kitu hakipo sawa kama endapo tutatumia akili zetu vizuri tutaweza kung'amua kuwa Wazungu wameingiza upagani kwenye Neno la Mungu.
Upagani ni nini ?
Upagani upi huo ulioingizwa ?

Kuna tatizo gani na kubadilika badilika kwa tarhe za pasaka, ilihali tukio ni lile lile la ufufuko na ukombozi wa mwanadamu kutoka katika utumwa wa dhambi. Chenye maana ni tarehe siku au tukio ?

Je, Wewe kutokujua siku na tarehe aliozaliwa babu wa babu yako kuna ondoa ukweli/uwepo wa tukio kwamba babu yako alizawaliwa ?
 
Bro, Easter haihusiani na pasaka na haipo katika Biblia. Binafsi sijui ilipotokea na wala sijuagi maana yake labda unifundishe leo kiongozi. Ila nifahamucho, tunakumbuka Ukombozi pitia "damu ya mwana kondoo". Kama ambavyo damu ya Mwanakondoo iliwaokoa wana wa Israel toka utumwani Misri, ndivyo nayo damu ya mwana kondoo wa Mungu imetuokoa na kututuoa utumwani. Mengine siyajui na sitaki kuyajua. Hata ukinifundisha, nitayaachia hapa hapa JF. 😀😃😄😁😆
🤣🤣
KWa uandishi huu Hakika Mkuu wewe Ni msabato🤣🤣
 
Back
Top Bottom