Kitu ambacho wewe hujui ni kwamba wakati wewe na wenzio mnatafuta namna gani ya kuibomoa Tz, kuna watu na vyombo vinajifunza namna bora ya kuilinda tz na watu wake. Taifa linagharamia kusomesha watanzania namna bora ya kuilinda Tz, tena wanapelekwa kusoma ndani na nje ya nchi za Afrika, Asia, Europe na Marekani. Kabla hujafikiria namna ya kuiangamiza tz au serikali iliyoko madarakani fikiria kwanza hilo.
Mfano, watanzania na vyombo vya dola wanajua kuwa wakoloni walikuwa wanasali pale kwenye kanisa la St. Peter Oyster bay na kuleee St. Joseph (forodhani). Tunajua kuwa wakoloni walipoondoka kurudi kwao waliwaacha maaskofu nyuma na wapo hadi leo kwa namna ileile. Hatujawahi kusikia maaskofu wakiwaomba radhi watanzania kwa kusalisha wakoloni waliokuwa wanaibagaza nchi yetu. Hivyo, hata leo kama nikisikia kanisa linatoa matamko ya kuipinga serikali ya watanzania sishangai. Matamko kama hayo yalipaswa kuwa mengi sana wakati wa ukoloni kupinga wakoloni kuiba mali zetu kwa nguvu na kupeleka kwao.
Kuna wakati nasikia bunge la ulaya linajadili maswala ya nchi za Afrika; huwa nacheka sana, maana bunge la ulaya ni lilelile lililo kaa kule Berlin, Ujerumani chini uongozi wa Bismarck kujadili namna ya kuigawana Afrika na kuitawala kwa nguvu. Ni watu hawahawa sasa wanajiita bunge la Ulaya. Wana mawazo na akili zilezile za babu zao walikutana kwenye Berlin conference kupanga namna ya kulikata kwenye vipande vya hovyohovyo na kutawala.