Kwanini TISS wapo msibani kwa Marehemu Mhagama, na kwa kujificha?

Kwanini TISS wapo msibani kwa Marehemu Mhagama, na kwa kujificha?

Kitu ambacho wewe hujui ni kwamba wakati wewe na wenzio mnatafuta namna gani ya kuibomoa Tz, kuna watu na vyombo vinajifunza namna bora ya kuilinda tz na watu wake. Taifa linagharamia kusomesha watanzania namna bora ya kuilinda Tz, tena wanapelekwa kusoma ndani na nje ya nchi za Afrika, Asia, Europe na Marekani. Kabla hujafikiria namna ya kuiangamiza tz au serikali iliyoko madarakani fikiria kwanza hilo.​

Mfano, watanzania na vyombo vya dola wanajua kuwa wakoloni walikuwa wanasali pale kwenye kanisa la St. Peter Oyster bay na kuleee St. Joseph (forodhani). Tunajua kuwa wakoloni walipoondoka kurudi kwao waliwaacha maaskofu nyuma na wapo hadi leo kwa namna ileile. Hatujawahi kusikia maaskofu wakiwaomba radhi watanzania kwa kusalisha wakoloni waliokuwa wanaibagaza nchi yetu. Hivyo, hata leo kama nikisikia kanisa linatoa matamko ya kuipinga serikali ya watanzania sishangai. Matamko kama hayo yalipaswa kuwa mengi sana wakati wa ukoloni kupinga wakoloni kuiba mali zetu kwa nguvu na kupeleka kwao.

Kuna wakati nasikia bunge la ulaya linajadili maswala ya nchi za Afrika; huwa nacheka sana, maana bunge la ulaya ni lilelile lililo kaa kule Berlin, Ujerumani chini uongozi wa Bismarck kujadili namna ya kuigawana Afrika na kuitawala kwa nguvu. Ni watu hawahawa sasa wanajiita bunge la Ulaya. Wana mawazo na akili zilezile za babu zao walikutana kwenye Berlin conference kupanga namna ya kulikata kwenye vipande vya hovyohovyo na kutawala.
Unachanganya madesa sana...

Sina tatizo na nchi kulindwa kwa nguvu zote...

Nina tatizo na wewe kuchanganya vitu viwili tofauti kabisa "NCHI" na "SERIKALI". Ni wazi kuwa huna ufahamu na uelewa wa mambo haya

NAOMBA NIKUINGIZE SHULE KIDOGO YA SOMO LA URAIA​

Serikali ni nini?
👉🏻👉🏻Ni kikundi kidogo tu cha watu kilichopewa nguvu na mamlaka kusimamia uendeshaji wa shughuli za nchi au taifa kupitia chaguzi za kidemokrasia zilizo huru, haki na wazi. Serikali hutekeleza majukumu yake ktk nchi/taifa kwa kutumia taasisi mbalimbali za kiserikali; mfano ulinzi na usalama (polisi, JWTZ, TISS nk), huduma ya nishati ya umeme (TANESCO), ujenzi na kulinda miundombinu ya barabara (TANROADS & TARURA), huduma ya elimu (Wizara ya Elimu), huduma za kiafya (wizara ya afya) nk

Serikali hupataje madaraka na mamlaka hayo?

👉🏻👉🏻Kimsingi serikali ni wananchi na wamekasimu kazi hii kwa kundi hili dogo. Na kwa hiyo, serikali hupata mamlaka toka kwa wananchi (Soma katiba ya JMT Ibara ya 8) na wananchi hawahawa wanaweza kuiondoa au kuchukua mamlaka yao toka kwa serikali wakati wowote iwapo wanaona haikidhi malengo na matarajio yao...

👉🏻👉🏻"Serikali" huja na kuondoka lakini "nchi" au "Taifa" huwepo na kudumu milele. Nchi ndiyo inayolindwa kwa nguvu zote na wenye jukumu hilo sio serikali bali wananchi wenyewe kupitia utaratibu waliojiwekea. Sometimes hukasimu mamlaka ya ulinzi wa nchi na taifa lao kwa chombo kinachoitwa "serikali". Na serikali inaposhindwa kufanya kazi yake sawasawa na matarajio ya wananchi, basi serikali inaweza kufurushwa madarakani wakati wowote...!!.

👉🏻👉🏻Kwa hiyo, literally, kuna aina mbili za serikali ambazo ni;

A: SERIKALI YENYE RIDHAA YA WANANCHI:
👉🏻👉Hii ni serikali iliyopewa mamlaka na wananchi wenyewe kupitia uchaguzi huru, wa haki na ulio wazi. Hii tunaweza kuiita "serikali ya kidemokrasia".
👉🏻👉🏻Serikali ta namna hii ni halali kabisa na kwa kweli hulindwa na kuenziwa kwa wivu mkubwa na wananchi kwa kuwa inakuwa pale kwa maslahi ya "nchi" kwa ujumla
👉🏻👉🏻Serikali zilizoingia kwa njia za kidemokrasia wakati mwingine on the way, hubadilika na kuwaasi wananchi na kugeuka kuwa serikali za kudikteta.
👉🏻👉🏻Ikifikia hatua ya kuwaasi wananchi, basi serikali hii hugeuka kuwa adui wa wananchi na hupingwa na kukataliwa kwa njia zozote...!!

B: SERIKALI ISIYOTOKANA NA RIDHAA YA WANANCHI:
👉🏻👉🏻Hii ni aina ya serikali ambayo imepata madaraka na mamlaka kidola ya kutawala nchi na wananchi kwa kutumia maguvu pasipo ridhaa ya wananchi kupitia uchaguzi huru, wazi, wa kuaminika na ulio wa haki
👉🏻👉🏻Wakati mwingine huingia kwa chaguzi za kilaghai (manipulated elections) na wao hujitetea kuwa "tumechaguliwa na wananchi" kupitia uchaguzi huru..!!
👉🏻👉🏻Tabia ya serikali za namna hii mara nyingi ni kutawala kwa maguvu, viongozi wake ni wezi, mafisadi, wabinafsi, hawapendi nchi na wananchi bali hujipenda wao tu.
👉🏻👉🏻Aidha, viongozi chini ya serikali ya namna hii mara nyingi sana huwa na tabia ya dharau kwa wananchi, kiburi na lugha chafu za kibabe kama tu unavyoiona hii ya Tanzania chini ya CCM inayoongozwa na Bi Chura Kiziwi a.k.a Idd Amin Mama a.k.a Bi Kizimkazi.

SERIKALI YA KIDIKTETA HUFANYWAJE?​

💪🏻💪🏻Hupingwa na kupigwa vita vya ndani na nje ya nchi kwa nguvu zote. Hili huwa lina gharama kubwa ikiwemo kugharimu hata maisha ya watu kama ilivyotokea MO29 na yanayoendelea kutokea.

💪🏻💪🏻Sababu kuu ni moja tu, kwamba, serikali zisizotokana na ridhaa ya wananchi kokote duniani hutumia nguvu kujilinda zenyewe (sio nchi) ikiwemo kuteka, kutesa, kupoteza na kuua kila mtu wanayehisi ni tishio (threat) dhidi yake awe ndani ya serikali yenyewe au nje ya serikali. Wao husema na kujitetea kusema "ni kwa maslahi mapana ya taifa na nchi" lakini ukweli ni kuwa ni kwa maslahi ya viongozi binafsi wa serikali hii ya kishenzi. Hata kifo cha huyu Jenista Mhagama ni matokeo ya kuwa na serikali ya namna hii...!!

KWA HIYO WITH ALL DUE RESPECT:​

👉🏻👉🏻Usitetee haya mambo kwa kuliingiza kanisa Katoliki kwenye ushenzi wa hawa watu.

👉🏻👉🏻Acha kuleta mambo ya historia uchwara za Berlin Conference kwenye mambo ya leo yanayoonekana na kutendwa na watu tunaowaona waziwazi, wengine ndugu zetu na jirani zetu kabisa

👉🏻👉🏻Na Kumbuka kuwa;

1. SERIKALI na NCHI/TAIFA ni vitu viwili tofauti in the context of operational japo zina uhusiano na kukutana mahali

2. SERIKALI huja na kuondoka lakini NCHI/TAIFA lipo na linadumu vizazi hata vizazi

3. Wakati huja SERIKALI NZURI zenye kukubalika na wananchi wote lakini wakati mwingine huja ndani ya nchi SERIKALI MBAYA kabisa zenye tabia ya kishetani 100% kama ilivyo hii ya Bi Samia Suluhu Hassan

4. Kuipinga na kuikataa serikali si kosa la jinai. Ni shughuli halali ya kidemokrasia

5. Serikali inaweza kuwekwa na kuondolewa na wananchi wenyewe wakati wowote.

KUMBUKA HILI: Tumeweka miaka mitano mitano serikali ya kidemokrasia kukaa madarakani kabla ya uchaguzi mwingine only if mambo yanaenda sawasawa. Serikali inapozingua, wananchi hatulazimiki kusubiri miaka mitano..
 
Huenda alikuwa Mwenzao! Na you never know huenda ndio wamem terminate. Nchi hii ni ngumu sana.
 
Ba- orange
Mama Kodi
Hawa watu wajiandae, ni kupelekwa kuzimu, sasa wazubae waone.
Huyo bibi wa kigeni si aende hata huko kwao halisi, yuko anazubaa na uteuzi wa tume fake hajui ni mtego. Lol
Wewe mpumbavu huyo Mama Kodi na bibi wa kigeni ni kina nani?
 
Kwamba TISS hawageukani? Bas ndo hivyo Kipenyo kaondoshwa mapema mchezoni, hatutaki vikwazo sie.
Bado Inno na mama kodi. Tumalize mchezo.

Kwamba TISS hawageukani? Bas ndo hivyo Kipenyo kaondoshwa mapema mchezoni, hatutaki vikwazo sie.
Bado Inno na mama kodi. Tumalize mchezo.
Mama Kodi ni nani tena msaada tafadhali
 
Haya mambo ya kujua siri kuu ni hatari sana! Kama unashiriki/shirikishwa siri na wenye siri kuu wakiona utakuja kutoa siri lazima uondolewe tu. Sipendagi kushiri/kushirikishwa mambo ya siri hata kama nitalipwa. Mambo ya siri ni sawa na mambo ya kichawi tu, wachawi wana siri zao, ukitoa wanakushughulikia hata kama hujato ila wanahisi utatoa, wanakufutilia mbali. Kazi za siri ni nyingi ndio maana wengine huapa kuwa hawatatoa siri
Inaitwa kufuta nyayo
 
Back
Top Bottom