Kwanini TPDC wanalipwa mshahara mkubwa kiasi hiki?

Kudadeti, walimu wanalala njaa tu huku sekta zingine wanalalia dollar
 
Wakati nipo pale Staff hasa wa Idara ya Explorations walikuwa wanabadilishia mabegi Airport,yaani mfanyakazi anatoka safari ya kikazi mfano Norway na Dubai,anatua na Emirates saa 9 mchana ana check out,Mkewe anakuwa nje pale kamletea Begi lingine la nguo anabadilisha,anachukua nguo hizo alizoletewa,ana-check in kisha anageuza na Emirates hiyohiyo saa 11 jioni kwenda Calgary Canada huko au kokote kwenye kazi nyingine za Shirika,ndio maana pale Wafanyakazi walikuwa wanachukua VISA za mwaka mzimamzima kuepusha usumbufu
 
Itakuwa na yeye mwalimu anatumia jukwaa kutaka mabadiliko maana kuacha kazi anaogopa .same to me kipindi jobless niliilaumu sana serikali now shavu kimyaaa hata kutetea vijana wenzangu mtihani

Cc @mwifa
Daahh, ndio maana wasaka vyeo wakishavipata wananyamaza[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3].

Usiache kutusemea jobless mkuu
 
walitaka kuondolewa kwenye chimbo la asali...!! kuna mwana wangu kasoma petrolium aisee hana mchongo akija kuotea hapo ni balaaa
 
walitaka kuondolewa kwenye chimbo la asali...!! kuna mwana wangu kasoma petrolium aisee hana mchongo akija kuotea hapo ni balaaa
Kama ana Upper Second mwambie anitafute nimuunganishie akaanze hata kujitolea TPDC au PURA maana Mkurugenzi Mkuu wa PURA Eng.Sangweni ni mshkaji wangu anaweza akamsaidia,na uzuri pale ukipata nafasi ya kujitolea kisha nafasi zikaja kutangazwa official unachukuliwa kirahisi,na wao huwa wanatangaza wenyewe hawapitii PSRS
 
aisee bhasi ntakuunga nae mkuu yeye kaenda kusoma nje kwa sasa ila ntamtonyaaa
 
Hizi propaganda sometimes muwe mnaacha. TPDC kwenye hii sector ya oil and gas ndio shirika ambalo wana mishahara ya hovyo kuliko mashirika yote. Huyo jamaa yako kakuingiza mkenge na wewe ulivyo huna akili plus wivu unakuja kuanzisha thread hapa. NARUDIA TPDC MISHAHARA YAO NI POOR SANA.
 

Me nikabaki kimya sikua na nguvu ya kujibu… NAKIU ha mkono
 

Mzee wa ikulu upoo?? Be patient mkuu
 
Hakika nifanikiwa kuingia Ikulu kwa njia yoyote ile 2030, lazima nikuteue kuwa Waziri Mkuu, au kama utakosa vigezo vya kielimu, basi nitakuteua kuwa Waziri wangu wa Elimu.

Yaani wewe ni Mgogo wa kwanza nchini kuwa na tabia kama za Marehemu Edward Moringe Sokoine. Wagogo wenzako wengine waliobakia, akili zote zimehamia tumboni.
 
Huu ni wizi umewekwa na vigogo wa CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…