Kwanini transaction fee kati ya mabenki na mitandao ya simu ni kubwa sana?

Kwanini transaction fee kati ya mabenki na mitandao ya simu ni kubwa sana?

Balaa kabisaa. Na ndio unakuta huna jinsi paymentninabid ifanyike kwa bank. Na ni mida mibovu hakuna huduma wakat huo.
Maana kwa mfano haya makato ya 6500, hiyo ni bora ukatoa kwa wakala kisha ukaenda kutuma kwa wakala wa bank, makato hata hayakaribii hiyo oesa wanayokukata ukifanya direct mobile-bank deposit.
Sio bora. Fanya mahesabu yako vizuri. Ukitoa kwa wakala hio 270,000 unakatwa kiasi gani?
 
Una uhakika?
What do you know??
Screenshot_20250416_193240_Samsung Internet.jpg
 
Ya Mix by yas iko wapi?
Screenshot_20250416_193556_Samsung Internet.jpg

Utagundua hazina tofauti sana tena kwa Mixx by Yas kidogo zime drop japo kwa refference hiyo ya kutuma pesa, hawajaweka column ya kutoa but you can tell such a correlation based on withdrawal charges uki compare na Tigo. Mambo ni yale yale tu Tigo ndio Yas hata sijui una complicate kitu gani
 
Kodi ni ndogo hela nyingi ni makato yao, uwe unasoma mchanganuo. Hao ndio wanyonyaji aliowakataa baba wa Taifa, ubepari ni unyama ndg. Wanavuna bila kupanda na ili kuwapofusha serikali kila shughuli ya serikali wao ni wafadhili hasa CRDB. CRDB ni majambazi
Leta mchanganuo mkuu.
 
Sasa si uweke huo mkeka mbona unafanya mambo yawe magumu ndugu?
Sina huo mkeka. Nataka uhakika tu, ili na mie nijue urahisi uko wapi? Mana mie mdau mkuwa sn wa kuhamisha pesa from simu to bank and vise-verse
Nataka uhakika ili inisaidid kupunguza gharama inapobidi, mie nilikuwa najua kote gharama sawa
 
View attachment 3306593
Utagundua hazina tofauti sana tena kwa Mixx by Yas kidogo zime drop japo kwa refference hiyo ya kutuma pesa, hawajaweka column ya kutoa but you can tell such a correlation based on withdrawal charges uki compare na Tigo. Mambo ni yale yale tu Tigo ndio Yas hata sijui una complicate kitu gani
Shukraan sn
 
Mtihani kweli Mimi Pana siku Ruaha ndani ndani huko ukitaka ATM ili ukatwe elf tatu kutoa hela ni lazima uende Mahenge mjini kwenda na kurudi nauli ni elf 20 kwa boda au elf 7 kwa mshikaki sawa na elf 14,nikicheck gharama za boda na kuhamisha kwa simu tofauti ni elf 3 nikawa sina jinsi kuhamisha kwenye simu network yenyewe niliifata juu ya mlima kule mtandao ni mmoja tu halotel halopesa kupanda mlima nusu saa,kwenda na kurudi kwenye ATM Mahenge masaa matatu.
Kwa uharaka wa pesa nikawa sina option ya kuchoma zaidi ya elf 20 ili kupata pesa kwa process mbili.
Yaani kuhamisha pesa toka bank kwenda simu wakalamba,
Kutoa pesa kwa wakala wakalamba elf sita.
Watumishi wa vijijini wanapata sana tabu kwenye ishu za miamala.
Sasa hivi kuna Selcom Pesa hauna haja ya kwenda mbali kuna mawakala wa Selcom kila kona, na makato ni madogo sanaaaa. Pakua hapo kisha utanipa feedback Selcom Pesa. Makato madogo kuliko!
 
Ni ngumu sana kuwaelewa, na hawajawahi tolea ufafanuzi hata siku moja!
Wale wachuni nguli huwezi sikia wakiongelea hizi mambo kwa kuwa yule tozo master anajuamadokezo anayoandikaga
 
Nilidownload app ya nmb nikawa natuma pesa kwenda mitandao ya simu nikawa naona ni rahisi sana kuliko kwenda bank
Siku nikaona nifuatilie makato yakoje aseeeeeh sikuamini nilichokiona
Toka wakat huo nilijiapia sitofanya huo muamala tena nitakuwa naenda bank natoa kupitia ATM kisha naweka kwenye line yangu kisha natuma
 
Kiukweli kwa muda niliokaa na app ya nmb mobile nikawa nafuatilia kilamiamala kwenye akaunt yangu.
Nilichogundua ni heri utunze pesa kwenye line za simu kuliko benki yaan wana vimiamala vya ajabuajabu tena wanakukata bila kukuliza

Mfano niliangalia salio nikawa na sh 80,000 siku kadhaa mbele nikannua muda wa amaongezi wa sh 15,000 kuchungulia salio nikakuta zimo sh 41,918 kiukweli nilishangaa sana
Kudownload statement nakuta vimakato vya ajabh ambavyo hata sikuvielewa tena sasa ni kwa kiingereza

Wanaboa sana hawa bank
 
Back
Top Bottom