Uchaguzi 2020 Kwanini Tume ya Taifa ya Uchaguzi imjibie tuhuma Mgombea?

Uchaguzi 2020 Kwanini Tume ya Taifa ya Uchaguzi imjibie tuhuma Mgombea?

Ndicho ambacho mgombea wa urais kupitia Chadema amekuwa akisisitiza kinyume na yule anayesema yeye kwake katiba sio kiaumbele.
JPM anafanya maendeleo hiyo ipo wazi ila madaraka na nguvu kubwa aliyonayo inapunguza uwazi na ufanisi. Hata ushauri hapokei, ndio maana kunabmaswala huwa ana prive total failure. Mf sakata la korosgo last year
Tatizo wengi ukizungumzia katiba mpya, haki na uhuru wanaona unataka kuleta fujo.
CCM wananufaika na hii katiba ya sasa, why bother..!!.yes ,ukubwa wa madaraka unamfanya achemke kwenye baadhi ya mambo kama hilo la korosho.chombo ambacho nacho kingesaidia kumuweka sawa ni bunge.nalo ndio hivyo halieleweki.kuanzia spika na wabunge tawala wote dhaifu.katiba mpya ni muhimu sana.
 
Kuwa na akili basi hata baadhi ya masaa mkuu.
Hujui kwamba sheria ndio mgongo wa maendeleo? Hiyo kodi inayokusanywa kwaajili ya maendeleo haikusanywi kwa mujibu wa sheria?
Huo mshahara unaolipwa ofisi unayoifanyia kazi ambayo ndio chachu ya maendeleo yako haulipwi kwa mujibu wa sheria?
Hiyo nyumba uliyopanga au uliyojenga haulipwi Kodi kwa mujibu wa sheria?
Ndiomana sishangai wanaosema wanaccm akili zimelala kwasababu mambo mengine ya wazi kabisa lakini wao wataoppose.
mijitu km hyo ndo mtaji wa ccm
 
Namba 4 sheria na taratibu haziruhusu?
Ndio, kufanya kampeni kwa niaba ya muhusika. Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi sidhani kama ni sawa
Sizungumzii kumsupport. Kinachosemwa ni mfano TAL alitakiwa kwenda sehemu A siku X kwa mujibu wa ratiba ya tume, badala yake Mbowe anaenda eneo hilo kuchukua nafasi ya muhusika moja kwa moja
 
Yes,ndio kulikuwa na jambo la mabadiliko ya katiba n.k,lingeshughulikiwa hili maana yake na tume huru ya uchaguzi ingepatikana,pia ingewezekana Rais kupunguziwa nguvu kwenye baadhi ya maamuzi na machaguzi,na uteuzi wa vyombo kama NEC, kwahiyo sasa katiba mpya ni suala la msingi si tu kwa upinzani, bali kwa watanzania wote. vinginevyo ndio kama hivi yan...

Nadhani utakuwa umepata majibu ya maswali yako.
wakati Jiwe kasema wazi swala la katiba kwake halipo ndiyo maana amesubiriwa kwenye sanduku la kura tuone kama atachomoka
 
Hivi akina Kibatala hawawezi kupeleka hoja mahakamani kwa hati ya dharura ya kuomba mkurugenzi huyu aondoelewe katika nafasi hiyo kabla ya siku ya uchaguzi? Najiuliza tu, kama inawezekana kisheria.

Wakuu mimi si mtaalamu sana wa sheria lakini najaribu kujiuliza maswali machache.

1. Kwanini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Kupitia mkurugenzi wake) inajaribu kujibu na kukanusha tuhuma kwa mgombea fulani. Si ilipaswa yeye mwenyewe au waenezi wa chama kama akina polelepole wafanye hiyo kazi?.

2. Je, Mkurugenzi anavosema mgombea A anapotosha umma na kuwadhihaki wengine, je hiyo kauli yake kuwa kuna watu watapeleka madini nje kwake haoni kama ni tuhuma pia.

Na hii imesemwa na mgombea anaye mtetea, haoni kama ni kitu kilekile anachokataza upande wa pili?

3. Anavosema watanzania wanataka A,B,C, hawataki E,F,G ni lini alikaa na watanzania wakamwambia hayo. Je anaweza kuthibitisha hayo mahakamani.

4. Je, uvunjaji wa taratibu unaofanywa na baadhi ya wagombea ubunge, mfano anayetoka nje ya jimbo lake kumnadi mgombea urais wa chama chake (kazi iliyopaswa kuwa ya mgombea mwenza) hayo haoni kama ni ukiukwaji wa taratibu?

Nawasilisha
 
Tanzania hakuna tume ya taifa ya uchaguzi bali kuna tume ya taifa ya upendeleo
 
Lissu ni mwanasherai kila sehemu anadhani ni mahakamani. Anazua kesi! MWambieni atoe ahadi za maendeleo. Rais gani anaahidi kurekebisha sheria, kwani yeye ni Bunge?
Kwani Magufuli anaposema amefuta kodi 99 kwenye kilimo yeye ni Bunge?
 
Lissu ni mwanasherai kila sehemu anadhani ni mahakamani. Anazua kesi! MWambieni atoe ahadi za maendeleo. Rais gani anaahidi kurekebisha sheria, kwani yeye ni Bunge?

Wewe una tatizo la kisaikolojia, hivi ahadi za maendeleo ni zipi? kwani kurekebisha sheria siyo ahadi ya maendeleo?
 
Msimamizi wa Sheria na kanuni za uchaguzi anazivunja sheria na kanuni mwenyewe sijui tukashitaki kwa nani ?[emoji23][emoji23]
 
Waache waingie kumi na name ya icc naona shetani ashawasogeza karibu kutaka kuisaidia CCM
 
Mkurugenzi wa tume. Anasoma makaratasi aliondikiwa na Polepole.
Anajibu hoja za Lissu kupitia NEC.?!

Imenikumbusha barua za kuunga juhudi, wapinzani waliokua wananunuliwa kama kuku za kitoeo sokoni.

Uchaguzi huu lazima tupasuane matumbo tulane maini wenyewe kwa wenyewe.
#sasabasi.
 
Back
Top Bottom