Kwanini tunachukiana makazini? Yani shida inakuwa nini?

Wajapani zaidi ya 30 upo nao kwenye Oil rig kwa muda mrefu unaanza kazi mpaka mkataba unaisha mkuu usijue kuwa watu wana chuki kaa na Wazulu wachache tu kwenye meli utajua tabia zao..
 
Katika taasisi zote nilizowahi kufanya kazi, watu wake wote wanafanana kitabia. Nadhani hii ni common African behavior. Wafanyakazi wenzio hawatakaa wapende mabadiliko chanya katika hali yako ya kimaisha, iwe ni kiuchumi, kiimani, kijamii nk.

Unaweza ukakuta daraja fulani la wafanyakazi ambalo linapokea kiwango sawa cha mshahara au gape la mshahara ni dogo tena ni kutokana na uzoefu. Sasa itokee umeamua kuchagua maisha ya kutokula bata zisizo na maana (pombe na wanawake) ukaamua kutumia hela yako kuboresha hali yako ya kimaisha kwa kufanya vitu vya maana (kununua assets au shughuli yakukuongezea kipato) chuki, fitina, visa na vitendo vya kishirikina utakavyokutana navyo kama humtegemei Mungu na hujasimama kiimani nakwambia huwezi toboa hapo kazini.

Na jinsi binadamu walivyo wa ajabu, wanaweza wakakusaka kote huko kisirisiri ila wakikushindwa kuna siku tu watakwambia kabisa jinsi lifestyle yako inavyowanyongorota, iwe kwa bahati mbaya au makusudi.

Nadhani hii hulka huenda ndio sababu kuu iliyomfanya shetani akachagua mizizi wa Uchawi Mweusi (Black Magic) aichimbie Afrika.
 
Mkuu namba namba yako pm umenigusa sana boss
 
Ushamba tuu na ulimbukeni,kipindi nafanya kazi kampuni flani nilihamia Dodoma ,nikakutana na jamaa mmoja alikuwa ni mtu mwenye chuki kwa watu wengi!Siku Moja aliingia Cha kike,tumefanya mchongo nae alivyomjinga akaenda kunichoma kwa bosi kwamba nimeuza kitu kwa flani-----Bosi akamfuata huyo mtu,Bahati Nzuri bosi alikuwa muelewa akamuuliza jamaa vizuri Jamaa akataja tuliomuuzia!Kwa Bahati sana huyo mtu aliomba namba ya simu ili akiishiwa tumletee Tena mzigo.Bosi kupiga namba ni ya yule mnoko.Duuh ilikuwa mtiti ofisini.Wewe unawasema wenzio kumbe na wewe umo!Bonge la Aibu Ina maana hata Mimi Boss wako ukikutana na mabosi wangu utakuja kusema mapungufu yangu .
 
Sio wanawake tu hata wanaume pia wanakua na chukiii......ukiwa smart katika kazi zako ukipendwa Na maboss Na ukiwa Na Nyota kalii Na ukiwa smart kuwazidi wanafeel inferior Na kuanza kukuonea wivu mwishowe chuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…