Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

Haiwezi kuwa AWAMU YA SITA. Kwa vigezo vipi?

Mkuu, haya ni matokeo ya kufanya mambo pasipokufuata taratibu, mama anaendeleza mle mle kwenye njia alizoziasisi mtangulizi wake.

Kwa hiyo mama na yeye sasa anatambua kwamba akijitangazia AWAMU YA SITA, hakuna atakayepingwa, kwa sababu yeye ndiyo rais!

Lakini hata akitangaza, historia itabaki kuwa vile vile, kwamba yeye anaendeleza awamu ya tano baada ya bosi wake kutoikamilisha awamu yao.
 
Aende kwa wananchi, wamchague.

Hiyo itakuwa ni awamu yake bila ya kelele zozote.
 
Aende kwa wananchi, wamchague.

Hiyo itakuwa ni awamu yake bila ya kelele zozote.
Hii ni awamu yake. Kelele zinazopigwa hazibadili hilo. 2025 kuna uwezekano mkubwa akachaguliwa tena kumalizia awamu yake ya sita kwa kipindi cha mwisho kama chama kitampitisha.

Kama hii si awamu ya 6, ikitokea akapitishwa na chama akaanza awamu ya 6 yenye vipindi viwili, basi tupo naye for the next 14 years.
 
Si kweli mnapotoshana awaamu inaambatana na Rais mpya awamu sio kikatiba ni mapendekezo ya chama
 
Awamu ni Raisi😂😂 Raisi akifa na awamu inaisha na hii ni kisheria maana awamu ni ya Raisi sio makamu. Hivyo hii ni awamu ya kwanza ya awamu ya 6 na anaweza kuhombea tena kisheria kwa muhula mmoja.
 
Kwani awamu unaihesabu vp?NI kwa miaka? Au ?
Kama NI miaka je awamu Mona ina jumla ya miaka mingap? Labda wewe ndio utueleweshe kwa Nini unasema NI awamu ya tano muhula was pili
Basi hebu ona hizo awamu zilizo
pita
Nyerere miaka 20+
Mwinyi miaa 10
Mkapa 10
Jk miaka 10
Magu 5
Haya sisi tusiojua awamu tuambie awamu ina miaka mingapi?
 
Eeenh Heee,
Hii ni awamu yake. Kelele zinazopigwa hazibadili hilo.

Mkuu, hii tabia ya mabavu mtaachana nayo lini? Tumia akili zaidi kuliko kulazimisha watu.

Hiyo habari ya "2025 yeye kugombea na kuchaguliwa kwa kipindi chake cha mwisho" umeitoa wapi?
Ndivyo katiba inavyosema?
 
Eeenh Heee,


Mkuu, hii tabia ya mabavu mtaachana nayo lini? Tumia akili zaidi kuliko kulazimisha watu.

Hiyo habari ya "2025 yeye kugombea na kuchaguliwa kwa kipindi chake cha mwisho" umeitoa wapi?
Ndivyo katiba inavyosema?
Boss sio mabavu ni uhalisia.

Ndiyo... katiba imetoa vipindi viwili vya miaka 5. Ccm wakavibatiza jina awamu. SSH akigombea 2025 anamalizia kipindi chake au awamu kama ccm wanavyoziita, katiba haimruhusu zaidi ya 2030.

Ila kama hii ni still awamu ya 5 kama unavyotaka na si awamu yake, basi inamaana ana vipindi vingine vya miaka 5 mara mbili vya awamu mpya.2025/30 - 2030/35. Hapa ataongoza kinyume na katiba inavyotaka miaka 10.

JPM lets say angefariki 2 years before uchaguzi basi hicho kipindi cha miaka 2 kisingekuwa awamu ya sita bali ya tano. Lakini 3 yrs na kuendelea ni awamu mpya.
 
Ila kama hii ni still awamu ya 5 kama unavyotaka na si awamu yake,
Nielewe, siyo kama ninavyotaka mimi; lakini hujaweka vigezo vyovyote vinavyoonyesha kuwa ni awamu ya sita.
Kama nilivyoandika hapo juu, kama anataka awe na awamu yake, aende kwa wananchi wampigie kura na aunde serikali yake ya awamu ya sita.
Huu uliopo sasa ni mwendelezo wa awamu ya tano.
 
Kalamu 1

"Ila kama hii ni still awamu ya 5 kama unavyotaka na si awamu yake, basi inamaana ana vipindi vingine vya miaka 5 mara mbili vya awamu mpya.2025/30 - 2030/35. Hapa ataongoza kinyume na katiba inavyotaka miaka 10."


Sentensi nimeandika imekamilika usiipunguze kubadili maana.
 
Mimi sioni tatizo na hili, endapo kama ana ridhaa ya wananchi hapo 2025 na miaka mingine mitano baada ya hapo!

Maadam katiba iko kimya juu ya hilo, wewe unaona tatizo?

'Caviet' ni hiyo moja tu, kutimiza matakwa ya wananchi - yaani wampigie kura 2025 na hiyo mitano ya kumaliza awamu hiyo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sababu kubwa ni hii
 
Tupo pamoja katika hili mkuu.

Wananchi ndo kila kitu.
 
Znz wana katiba yao ambayo ni tofauti na ya kwetu. Sijui kwanini unafananisha ila ni kwamba, Hayati JPM alishinda uchaguzi wa mwaka 2020 ili kukamilisha muhula wake wa pili wa awamu ya tano. Akahudumu kwenye muhula wa pili kwa miezi michache.

Katiba inasema, Makamu wake aapishwe kumalizia ngwe iliyobaki, na zaidi inasema kama kipindi kilichobaki ni chini ya miaka mitatu, Makamu huyo hatahesabiwa kuwa amehudumu kipindi kimoja cha awamu hiyo.

2020 angeshinda Lisu au CCM ingempitisha mtu tofauti na JPM, hapo tungekuwa tumeanza awamu ya 6.

Hivyo, Samia anamalizia muhula wa pili ulioachwa na JPM kwa uchaguzi wa 2020. Yeye ni raisi wa 6 wa JMT yenye mihula mitano mpaka sasa, ndo kusema, awamu ya tano imeshikwa na maraisi wawili.

Ni kama katika hali ya kawaida kuendelea kung'ang'ania kuwa Edward Lowasa ni waziri mkuu mstaafu, alistaafu lini?
 
Pengine tuzumzie awamu baada ya vyama vingi na uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia. Awamu inaweza kuwa ni kichwa au muda kutegemea na uchaguzi au anayeingia ofisi kuu.

Mtu yule yule anaporudi ofisini baada ya uchaguzi mkuu, awamu haibadiliki. Awamu inaweza kuwa ya miaka 5 au 10 kutegemeana na uchaguzi.

Raisi mteule, baada ya kuapishwa kikatiba, anapaswa kumteua waziri mkuu ndani ya siku zilizotajwa, waziri mkuu mteuliwa ataapishwa na raisi. Raisi atalihutubia bunge ishara ya kulifungua rasmi bunge.

Kuna tamko lolote kuhusu kwanini Majaliwa anaendelea kwa uteuzi ule ule wa JPM na kiapo kile kile cha JPM?

Waziri mkuu akifa, baraza linakuwa limekufa, vipi akifa Raisi, baraza aliloliteua linabaki?

Samia ni raisi wa 6 wa JMT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…