KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Haiwezi kuwa AWAMU YA SITA. Kwa vigezo vipi?Rais Mama Samia Suluhu Hassan nitakuwa wa mwisho Kukuamini kuwa tupo Awamu ya Sita kama unavyotulazimisha.
Ninachojua tu Generalist na naamini hata wale Waliobarikiwa vyema Akili ni kwamba tupo bado Awamu ya Tano ya Muhula wake wa Pili ( wa mwisho).
Rais Mama Samia Suluhu Hassan nitakubaliana nawe kuwa tupo Awamu ya Sita pale tu ukichukua Fomu na Kugombea Urais na ukashinda kuanzia mwaka 2025.
Rais wa Awamu ya Tano alikuwa ni Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na Wewe kuwa Makamu wake na alipofariki Kikatiba ukaapishwa Wewe kuendelea ndani ya Awamu hii kstika Muhula wake wa mwisho.
Nasikitika tu kuona kuna waliomuamini.
Mkuu, haya ni matokeo ya kufanya mambo pasipokufuata taratibu, mama anaendeleza mle mle kwenye njia alizoziasisi mtangulizi wake.
Kwa hiyo mama na yeye sasa anatambua kwamba akijitangazia AWAMU YA SITA, hakuna atakayepingwa, kwa sababu yeye ndiyo rais!
Lakini hata akitangaza, historia itabaki kuwa vile vile, kwamba yeye anaendeleza awamu ya tano baada ya bosi wake kutoikamilisha awamu yao.