Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

Ilani ya uchaguzi ni ileile ya awamu ya tano. Samia hana ilani ya uchaguzi mpya. Hivyo, Samia ni Rais wa sita lakini awamu ni ya tano. Umeandika vema.

Nafurahi Kueleweka nawe Genius hapa.
 
Kuendeleza alipoishia anamaanisha kufuata ilani ya CCM na miongozo ya Chama, hamaanishi mtindo wa uongozi.

Mfano: JPM alinunua ndege cash na ilani ilimuelekeza kununua ndege ila mtindo wa kutumia cash huo ni wake, Pengine mwingine angekopa.
Sasa alipoishia ni vipaumbele a Ilani ya awamu ya tano vilikuwa vinamuelekeza yeye kufanya hayo..je huyo Samia ni Ilani Gani anatumia..Kama Sio hiohio ya awamu ya tano ya kuanzia mwaka 2020-2025!?..vitu vingine huko so open ..Ila watu mnajitia upofu aisee..Samia ni Rais wa Sita katika awamu ya tano..akitokea akafariki ..Mpango atakuwa Rais wa Saba katika awamu ya tano still.ndio maana hata ukisoma katiba kwa kuielewa hii utaona dhana hii ipo katika kipengele cha Rais wa naman ya Samia na muda alioupata Urais na Kama anafaa kugombea tena ama la...soma iko kipengele
 
Duh..aisee kweli we ni andazi tena lile la kuchemsha
 
Awamu ni nn?

Sasa kama tu neno Awamu hulijui je, utaweza kweli Kujadili huu Uzi ambao unahitaji mno utulivu wa Akili katika Kuukabili ili mwisho wa Siku nawe usionekane ni Mpumbavu tu kama Wengine?
 

Genius Members kama Wewe si wengi.
 
Sasa unalazimishwa ama ndio ukweli wenyewe! Au umekariri urais miaka 10 ndio awamu inaisha!
Awamu ni Rais na sio miaka mkuu hebu jiongeze basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
So akitokea akafariki..ghafla..Mpango atakuwa Rais wa Saba katika awamu ya Saba sio!?
Ujinga mtupu ..Yani majitu nmnakomaa kwa kitu ambacho kipo wazi ..awamu Gani inakuwa na miaka minne..ama Tisa!?
 
Mzee..hivi mnasomaga katiba kama.kitabu cha hadithi ama gazeti!? ..embu Rudi tena kasome katiba vyema kipengele cha endapo Rais atafia madarakani na namna ya kumsimika Makamu wake kuwa Rais ndipo utaelewa usiyojua..
 
( i ) Abeid Aman Karume, ( ii ) Abeid Jumbe, ( iii ) Idrissa Abdul Wakili, ( iv ) Ali Hassan Mwinyi, ( v ) Salmin Amour, ( vi ) Aman Abeid Karume, ( vii ) Dr Mohammed Shein, ( viii ) Dr Hussein Ali Mwinyi.
 
Kwa faida ya wote maamuma...term za Rais ziko wazi kikatiba ..ukisoma anatuhusiwa kugombea term Moja..kwa kipindi cha miaka mitano..Kisha kipindi kingine cha pili cha miaka mitano..hii ndio kusema kwamba..JPM alikuwa katika kipindi chake cha pili cha miaka mitano...Mama Samia yeye karithi kipindi hiki cha pili ndio maana kwa kulitambua hilo.katiba inampa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano mbele..mara baada ya kumaliza ngwe ya Hayati....so mama Samia yeye ni Rais wa Sita katika awamu ya tano.

Na hiyo 2025 akigombea..akashindwa uchaguzi..aliyeshinda atakuwa Rais wa Saba katika awamu ya Sita...2030 ikitokea mama Samia atagombea tena na kushinda atakuwa Rais wa nane katika awamu ya Sita (kwa kuzingatia Ilani ya chama chake..na katiba )
 

Huyu mama mutake musitake ndio raisi wetu, na ikiwezekana kile kipengele cha kumtaka akamilishe 5years/mihula miwili kifutwe kabisa. Huyu Mama aongoze miaka15 mpaka 30.
 
Wewe usiye maamuma, tuambie kwanini Dr. Mwinyi kule Zenji ni Rais wa awamu ya nane?
 
Kwahio Samia ni Rais wa sita wa awamu ya tano?
 
NI AWAMU YA SITA KWA KUWA MAMA ANARUHUSIWA NA KATIBA KUGOMBEA MIAKA MINGINE MITANO TU!
NB: Kama sisi darasa la saba tumeelewa, wewe msomi ulikuwa unasomea ujinga?
 
Swali ambalo anatakiwa kujiuliza ni kuwa iwapo jpm angekuwa amesafiri au yuko kwenye matibabu ya muda mrefu automatically anayeongoza nchi ni yeye, je angesimama kwenye jukwaa na kusema hii ni serikali ya awamu ya sita? Then jpm akirudi anasema ni serikali ya awamu ya 5. Awamu za serikali zinatokana na UCHAGUZI sasa hapa hakuna uchaguzi mwingine uliofanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…