Znz wana katiba yao ambayo ni tofauti na ya kwetu. Sijui kwanini unafananisha ila ni kwamba, Hayati JPM alishinda uchaguzi wa mwaka 2020 ili kukamilisha muhula wake wa pili wa awamu ya tano. Akahudumu kwenye muhula wa pili kwa miezi michache.
Katiba inasema, Makamu wake aapishwe kumalizia ngwe iliyobaki, na zaidi inasema kama kipindi kilichobaki ni chini ya miaka mitatu, Makamu huyo hatahesabiwa kuwa amehudumu kipindi kimoja cha awamu hiyo.
2020 angeshinda Lisu au CCM ingempitisha mtu tofauti na JPM, hapo tungekuwa tumeanza awamu ya 6.
Hivyo, Samia anamalizia muhula wa pili ulioachwa na JPM kwa uchaguzi wa 2020. Yeye ni raisi wa 6 wa JMT yenye mihula mitano mpaka sasa, ndo kusema, awamu ya tano imeshikwa na maraisi wawili.
Ni kama katika hali ya kawaida kuendelea kung'ang'ania kuwa Edward Lowasa ni waziri mkuu mstaafu, alistaafu lini?