Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

Yapo mabadiliko makubwa ya yanayoashiria tupo awamu nyingine mkuu! Nakumbuka awamu ya tano Bashiru na mwenzake Chakubanga walikuwa wanaogopeka na kuheshimika kama simba wa porini ila ssa hivi wanapigana vikumbo na wakina Lusinde hata salamu hawapewi! Kweli zama Zimebadilika.
Bashiru na Polepole walimnunua Silinde kwa vipande vya fedha leo wanamuuliza maswali ya Nyongeza hahahaaa

Hii awamu ya 6 kweli

SSH mikumi tena atake asitake
 
Pole sana kwa uelewa mdogo.. Mlishakariri kuwa awamu moja basi ni lazima iwe MIAKA 10.. Angalia hapo MWINYI katawala mwaka mmoja tu 1984 had 1985 ikaitwa AWAMU ya tatu na JUMBE alichukua nafasi ya marehem KARUME 1972 ikaitwa AWAMU ya pili.. Hivyo kabla hujapost ujinga TAFAKARI KWANZA

Another Dunce.
 
We ni kilaza,hivi aufahamu kuwa kuna uchaguzi kila miaka mitano je kama magufuli angeshindwa na lisu tungesema lisu anaendeza awamu ya tano.

Hapo nafikiri aujaelewa,hebu fikiria kama membe angechukua fomu na magufuli kutokupitishwa alafu membe awe rais ingekuwa ni hawamu ya tano tena?.

Kwa ufupi hawamu ni vichwa vya marais ndio maana kila hawamu kunakuwa na rais bila kujali muda alioudumu kwa taarifa yako Samia ni rais wa sita wa tanzania .
Lakini kwa mantiki yako hii maana yake ni kuwa bado tupo awamu ya tano bado....maana JPM "alichaguliwa" kwa kipindi cha pili na akaunda serikali. So far, mama hajavunja serikali aliyoikuta....kafanya tu mabadiliko madogo. Kwa hivyo hoja ya kuwa tupo awamu ya 5 inapata mashiko.

Lakini mimi nafikiri hoja kubwa ni jina la Rais, likibadilika na awamu inabadilika. Sio suala la muda au uchaguzi. Awamu ni kipindi cha urais wa mtu fulani (Rais).
 
Yaani graduates siku hizi sijui ni kukosa kazi au ni kitu gani whether iwe ya 20 au ys 7 au number yoyote that doesn't matter tunachohitaji ni mahospital,shule bora,Barabara,Maji,siasa safi na the likes...hiyo ndio kitu ulete mezani tujadili mambo ya muhula yanahusu nn?akisema ni ya 5 let say itabadili nn kwako?
 
Awamu ya tano kivipi? Hii ni awamu ya sita. Awamu inawakilisha mtu si miaka.

Nyerere awamu ya 1, miaka zaidi ya kumi...
Mwinyi awamu ya 2, miaka kumi
Mkapa awamu ya 3, mikaka kumi
Kikwete awamu ya 4, miaka kumi
JPM awamu ya 5, miaka 5 na miezi miwili
SSH awamu ya 6, haijulikani miaka.......

Still kama awamu ni miaka 10 na si mtu basi Nyerere hajatawala awamu moja hivyo hatukupaswa kuwa awamu ya tano.

Kama hutaki we mbishi tu.

Naamini sasa Elimu ya Tanzania mbovu.
 
Kuwa raisi wa JMT Kuna njia mbili kulingana na katiba.

1. Kupigiwa kura
2. Kuchukua nafasi kupitia Makamo wa raisi na wote walioorodheshwa na katiba pale raisi anaposhindwa kutimiza wajibu kutokana na kifo au ugonjwa.

Njia zote hizo zinahalalisha kuwa amiri jeshi mkuu.

Kwann unafikiri neno awamu lazima uwe umechaguliwa? Katiba imekuelekeza hivyo?
Nimeisoma katiba sijaona panapo define neno "awamu", kama unapajua niambie ni article ngapi? Ilani gani anayoitumia Samia? mwenyewe anakiri anaendelea pale alipoishia mwenzake, kwanini bado anajihusisha na mwendazake, leo kasema asifananishwe na Magufuli wote ni wale wale.
 
mnapoambiwa msikimbie somo la Uraia mnakuwa wabishi..watoto waliozaliwa kichwa chini,wakachungukia matako
 
 
Popoma Gentamicin,Mzukulu,Clever right,All Rounder katika ubora na umbumbumbu uliotukuka.
Rais wa Zanzibar wa sasa Dr Hussein Mwinyi ni Rais wa awamu ya nane kule Zanzibar. Sasa jiulize hao marais nane wa awamu zote nane walifanya uchaguzi ndio ikaanza kuhesabiwa upya au.....!!.

Simple logic ni kuwa anapoingia madarakani Rais mwengine unaanza kuhesabiwa awamu mpya rejea mfano wa Zanzibar
Kweli kaka kule Zenji wameongoza hawa wafuatao!
1.Abeid Amani Karume
2. Aboud Jumbe Mwinyi
3. Alli Hassani Mwinyi
4. Idrisa Abdul Wakili
5. Salmin Amour Juma
6. Amani Abeid Karume
7.Alli Sheini
8. Hussein Alli Mwinyi
Nakila mmoja ana awamu yake bila kujali kaongoza kwa muda gani! Mama Samia yupo sahihi!
 
Nimeisoma katiba sijaona panapo define neno awamu, kama unapajua niambie ni article ngapi? Ilani gani anayoitumia Samia? mwenyewe anakiri anaendelea pale alipoishia mwenzake, kwanini bado anajihusisha na mwendazake, leo kasema asifananishwe na Magufuli wote ni wale wale.
Kuendeleza alipoishia anamaanisha kufuata ilani ya CCM na miongozo ya Chama, hamaanishi mtindo wa uongozi.

Mfano: JPM alinunua ndege cash na ilani ilimuelekeza kununua ndege ila mtindo wa kutumia cash huo ni wake, Pengine mwingine angekopa.
 
Hao wote uliowataja hapo walipigiwa kura, tuambie Samia alipigiwa kura na nani?

Ni bahati mbaya sana kuwa Uzi huu umevamiwa na Kuchangiwa kwa Kukurupuka na the so called Lumpen wengi ila Brainy ( Intelligent ) Members kama Wewe mpo wachache sana hapa Jamiiforums na hata katika Kuchangia huu Uzi wangu.
 
Back
Top Bottom