Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

Kwanini tunalazimishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa tupo Awamu ya Sita wakati Kiuhalisia bado tupo Muhula wa Pili wa Awamu ya Tano?

Awamu ni mtu anayeongoza. Samia ni Rais wa sita na awamu ya sita. Awamu hutokana na idadi ya marais walioongoza. Mfano magufuli awamu zote za miaka yake kumi ingeitwa awamu ya Tano kwasababu yeye alikuwa Rais wa tano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok, now mnakiri hilo neno "awamu" halipo kisheria, so mambo ya katiba hapa hayana nafasi.
 
Wengine tulikuwepo wakati neno awamu lilipoanza kutumika mwaka 1985.

Halina mantiki!!
 
Ujione mjinga itoshe kusema hivyo kama hata hili linakushinda kulielewa
Mataga ni Zero brain na ni Low Thinkers wengi wao, Type hii ya watu ni wengi wako sisiem na ndo mtaji kwa ccm kuitawala hii nchi...
 
Kuendeleza alipoishia anamaanisha kufuata ilani ya CCM na miongozo ya Chama, hamaanishi mtindo wa uongozi.

Mfano: JPM alinunua ndege cash na ilani ilimuelekeza kununua ndege ila mtindo wa kutumia cash huo ni wake, Pengine mwingine angekopa.
How comes mtu atumie ilani ile ile ya mwenzake halafu useme awamu ni tofauti? msilazimishe haya mambo.
 
Awamu nane za marais Zanzibar


JinaMuda wa UtawalaChama
Sheikh Abeid Amani Karume12 Januari 19647 Aprili 1972ASP
Skeikh Mwinyi Aboud Jumbe11 Aprili 197230 Januari 1984ASP, 1977 CCM
Ali Hassan Mwinyi30 Januari 198424 Oktoba 1985CCM
Idris Abdul Wakil24 Oktoba 198525 Oktoba 1990CCM
Salmin Amour25 Oktoba 19908 Novemba 2000CCM
Amani Abeid Karume8 Novemba 20002010CCM
Ali Mohamed Shein3 Novemba 20102020CCM
Hussein Ali Mwinyi3 Novemba 2020
Mkuu ungeyaacha tu haya masukuna. Yaendelee na ujinga wao.
 
Move on ndugu!

Kubali matokea Rais Tuliye naye si yule aliyetwaliwa.

Hii ni Awamu ya Sita.

Ninachojua ni Rais wa Awamu ya Tano anayemalizia Muhula wa Pili wa Mtangulizi wake Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Tatizo lenu mnasumbuliwa na Upumbavu mwingi halafu hampendi Kuchambua na Kuchanganua Mambo ( Masuala )

Nitakubali Samia ni Rais wa Awamu ya Sita pale tu akipitishwa Kugombea na CCM na Kupigiwa Kura na Wananchi na Kushinda pia.

Mnajiita Wasomi wakati hamna Maarifa.
 
Ni wachache sana wenye uwezo wa kuelewa bandiko hili lililowasilishwa kwa akili nyingi.
. Tatizo sijui waafrika akili yetu mpaka wazungu watuekeze. Haiitaji elimu ya sekondari Kujua Rais wetu SSH ni rais wa sita ndani ya Awamu ya tano. Ila kwa mara ya kwanza Tanzania itaongaozwa na marais wawili ndani ya awamu moja
 
Ni wachache sana wenye uwezo wa kuelewa bandiko hili lililowasilishwa kwa akili nyingi.
. Tatizo sijui waafrika akili yetu mpaka wazungu watuekeze. Haiitaji elimu ya sekondari Kujua Rais wetu SSH ni rais wa sita ndani ya Awamu ya tano. Ila kwa mara ya kwanza Tanzania itaongaozwa na marais wawili ndani ya awamu moja
 
Popoma Gentamicin,Mzukulu,Clever right,All Rounder katika ubora na umbumbumbu uliotukuka.
Rais wa Zanzibar wa sasa Dr Hussein Mwinyi ni Rais wa awamu ya nane kule Zanzibar. Sasa jiulize hao marais nane wa awamu zote nane walifanya uchaguzi ndio ikaanza kuhesabiwa upya au.....!!.

Simple logic ni kuwa anapoingia madarakani Rais mwengine unaanza kuhesabiwa awamu mpya rejea mfano wa Zanzibar
Popoma alipie hizi ID..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajui hata maana ya awamu hawa wasukuma naona wana jambo lao sirini dhidi ya serikali hii.
Mkuu masuala ya ukabila achana nayo. Wasukuma, Wasukuma. Pambana na maisha yako dogo. Nchi hii tukiamua kuzungumzia ukabila, hakuna kabila litashaini nchi hii zaidi ya Wasukuma. Mimi ni Mhaya na sipendi huo upumbavu wako wa ukabila. Au wewe ni Mkenya unataka kutugombanisha Watanzani? Hapa umechemka!
 
Kuwa raisi wa JMT Kuna njia mbili kulingana na katiba.

1. Kupigiwa kura
2. Kuchukua nafasi kupitia Makamo wa raisi na wote walioorodheshwa na katiba pale raisi anaposhindwa kutimiza wajibu kutokana na kifo au ugonjwa.

Njia zote hizo zinahalalisha kuwa amiri jeshi mkuu.

Kwann unafikiri neno awamu lazima uwe umechaguliwa? Katiba imekuelekeza hivyo?

Acha Kudanganya Watu njia pekee tena ya Kikatiba ndani ya CCM ni ile tu ya Rais Kupigiwa Kura.

Logically tu kwakuwa Mama Samia alikuwa Makamu wa Rais aliyepigiwa Kura kwa Awamu ya Tano Hayati Dkt. Magufuli akiapa Yeye Kikatiba hawi Rais wa Awamu ya Sita bali anaimalizia ile iliyokuwa ya Boss wake.

Hivi kwanini Jambo dogo tu hili linawashindeni Kuling'amua tena Kimantiki kabisa? Ubongoni mwenu kumejaa Takataka ngumu tu au?
 
Napata wasiwasi huenda kweli ccm wakatawala miaka mingine 100 ,kama wasomi ,sijui watoto wa mjini mnaopata mitandao akili ndio hizi? Je wa kijijini?. Yani hata awamu hamjui ni kitu gani?propaganda za TOT na nyie mmezikubali awamu ndio nini? Ziko kwenye katiba? Kama mdau alivyouliza angeshinda membe 2020 ingekuwa awamu ya ngapi? Mazoea ya ccm kuwapa mara is wake miaka 10 mmekariri ndio awamu?
 
Pole sana kwa uelewa mdogo.. Mlishakariri kuwa awamu moja basi ni lazima iwe MIAKA 10.. Angalia hapo MWINYI katawala mwaka mmoja tu 1984 had 1985 ikaitwa AWAMU ya tatu na JUMBE alichukua nafasi ya marehem KARUME 1972 ikaitwa AWAMU ya pili.. Hivyo kabla hujapost ujinga TAFAKARI KWANZA

Another Cretin.
 
Back
Top Bottom