Uchaguzi 2020 Kwanini Tusimchague John Pombe Magufuli !? Una sababu embu tuwekee hapa!

Uchaguzi 2020 Kwanini Tusimchague John Pombe Magufuli !? Una sababu embu tuwekee hapa!

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Kwa upande wangu mimi ni kuzuia mambo ya siasa mikutano ya hadhara na kukubali kuwapokea mashehe wa uamsho kutoka Zanzibar waletwe huku Tanganyika, hivi mheshimiwa hawezi kujua mambo ya uwongo na mzigo huu sasa umeiangukia Tanzania nzima,waislamu walio wengi wanaikataa CCM mwaka huu kwa dude hili tu la kuwafunga mashehe ,WaZanzibari wanawaita Mashehe wetu.

Kuna Viongozi wa CCM - Zanzibar waliwambia mashehe hawa mtaenda kunyea ndoo,viongozi wa ngazi za juu kabisa katika serikali kufika kutamka hayo kwa mambo ya kesi za kubambikia leo hii,malipo yapo njiani ccm wengi wakihudhuria mikutano ya viongozi hawa wa dini na wakiwakubali kwelikweli.

Leo mnarudi kuwaomba kura waZenji ,mmewakosea kubwa ni kuwa mmeshindwa kuwafikisha miaka saba ,sababu kubwa inajulikana mmewafunga kisiasa kuliko kiuhalisia wa sababu mnazowabambikizia ambazo mmeshindwa kuleta ushahidi.
Hii ni sababu ya kura yangu kutoelekea CCM naipeleka kule walikoniahidi siku ya kushinda tu basi mashehe wapo huru !
 
Kura za kuwakomboa mashehe ni kombora kubwa sana litakalowasambaratisha CCM ,kama makombora haya yakirushwa Tanga,Zanzibar Dar, Mtwara Kigoma Mwanza yaani Tanzania nzima likitumika kombora hili kwa usahihi,wananchi kueleimishwa vilivyo bila ya kujali dini zao.mbona CCM watasikilizia matangazo ya ushindi kutoka vyumbani mwao na presha juu juu.
 
1. Ni mkatili, mbaguzi, muuaji na mwenye roho ya chuki na kisasi kikubwa

Mf. Alivyowafanyia Ben Saanane, Tundu Lissu, Erick Kabendera na Mama yake, Msanii Idriss na wengineo wengi

2. Ameharibu uchumi kwa maamuzi yake ya kijinga

Mf. Kuingilia soko la korosho kulikopelekea biashara ya zao hili kufa

mf2. Anesababisha kupanda vibaya kwa bei ya sukari kutoka 1800 mpaka 2800/3000 kutokana na maamuzi yake ya hovyo ya kuzuia uagizwaji wa sukari kwa chuki zake dhidi ya wafanyabiashara

3. Ameharibu uchumi. Watu wengi wamefunga biashara kwa manyanyaso ya TRA na wengi wamepoteza kazi kutokana na makampuni yao kufunga biashara Tanzania

Mf. Rhino cement na mengineyo mengi bila kusahau Kampuni na maduka ya kubadirisha fedha

4. Amesababisha umasikini mkubwa kwa wakulima wa mananasi na mazao mengine kutokana na kuharibu mahusiano ya kimataifa mf na kenya ambapo wafanyabiashara na kampuni za kule ndo zilikuwa zinakuja Tanzania kununua mazao mengi

5. Ni muonevu na mpendeleaji mkubwa. Alifukuza kazi maelfu ya watumishi kwa vyeti feki huku akiwaacha kabudi na Makonda ambao hawakuwa na vyeti
 
Mimi km Mtanzania Mzalendo nitamchagua Rais Magufuli
 
Wewe km umejenga barabarani mlaumu baba ako kwa kukwepa gharama za kuchorewa ramani na manspaa
Ameninyima ajira mpaka sasa miaka 4 ,amobomoa nyumba ya home ,alafu anatutishia maendeleo
 
Ameharibu mifumo mingi ya nchi na utaratibu alioleta yeye umeleta hasaea badala ya faida. Mf. Mifuko ya pension
 
Kitendo cha kununua madiwani na wabunge wa vyama vingine kwa kodi ya watanzania, fedha ambazo ingetumika kuimarisha huduma zingine za jamii ni dhihaka na dharau makubwa kwa watanzania. Inatosha sisi wananchi kupata ghadhabu ya kukataa mtu huyo.

Lakini pia kitendo cha kukiri waziwazi kwamba maeneo ambayo madiwani na wabunge si wa chama chake alihakikisha hawapati huduma ya maji, barabara wala umeme wa REA kinatosha kutomchagua. Unachaguaje ubaguzi wa namna hii? Kiongozi anayetishia kunyima watu maji ni muuaji kwa sababu maji ni uhai.

Worse enough, kiongozi huyo aliamua nafasi zote za uteuzi ndani ya serikali, seckretariats na Tume mbalimbali inaenda kanda yake tuu ...Sasa maofisini hakukaliki kwa sabahu wafanyakazi nao wanaona ubaguzi wanaofanyiwa kisa umetoka kanda isiyopendwa. Ufanisi umepungua, hao wanaopendelewa nao wanajiona miungu watu maofisini, ni vitisho kila kukicha. Wanaojiona wanaakili zaidi ndo maana ya kupewa teuzi. Uonevu wa namna hii ni lazima kuumaliza tukipata nafasi adimu kama hii ya kura.
 
Ww na watanzania wapi? Huna mandate ya kuwasemea watanzania.
Na watanzania wana haki ya kuchagua wanae mtaka. Usiwasemee na kuwalisha maneno.
Watanzania ni kuanzia Wananchi wawili wa kitanzania.

Hiyo Mandate anayo ya kunijumuisha pia mie.
Nitamchagua John P.Magufuli kama rais Mzalendo na Nchi yake.
 
Back
Top Bottom