Kwanini Ujenzi wa Ulaya (Ukraine) hawaweki lenta?

Kwanini Ujenzi wa Ulaya (Ukraine) hawaweki lenta?

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
Hizi ni baadhi ya picha za majengo mbalimbali mitaani kutoka uwanja wa Vita uko ukraine.

Kinachoshangaza hata majengo ya serikali (magorofa Hadi nyumba za Kawaida) Nayo hayana beams Wala columns.

Mafundi, Wahandisi, wataalamu wa majengo na wanaJf hebu tufahamishane.

Imekaaje Hii[emoji848]
JamiiForums-1381373539.jpg
IMG_20220802_143102.jpg
IMG_20220802_142739.jpg
IMG_20220704_085304.jpg
IMG_20220802_143027.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na nyumba zao ni nzuri na Imara wenyewe wanashangaa nyumba na ghorofa nyingi za Africa zinajengwa kwa kiwango duni.Me huwa napenda sana ujenzi wao kwakweli nyumba zina miaka lakini zipo strong na nzuri labda ziharibiwe na vita kama hivo,,,,compare zetu chek magorofa ya NHC upanga na kkoo,posta huko Yan watu wana subiri mpaka serikali iwapakie rangi haha wakati wanalipa kodi kidogo hatar sana yan wanashindwa kujichangisha kweli,,,pic ikipigwa kuonesha magorofa ya Dar utasema mbele yasogelee karibu uone![emoji23][emoji23]
 
Sahii kabisa,
Bado najiuliza uimara ukoje ukzngatia hawafungi lenta?

Ina Maana wazungu hawajui umuhimu wa lenta au vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Same kwa Russia, ghorofa ya floors hadi tano haina columns wala beams na ndivyo wanavyojenga. Utakachoona ni beams za tofali and that's it, nyumba zao zipo imara sana. They're very precise wakati wa ujenzi, lakini pia soil structure yao inawapa favor huenda na wanatumia matofali yaliyokuwa compressed, nadhani hata bongo kuna sehemu wanatumia, kama yale ya kuchoma.
 
Bongo hata mikoan wanakotumia za kuchoma, bado lenta wanafunga.

Kibongo bongo mkandarasi ajenge ghorofa bila beam Wala columns za zege sidhan kama anaweza kueleweka.

Imekua Kama mazoea kufunga ring beams kwa kila jengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahandisi wa majengo njoni hapa mtupe maelezo! Inawezekana kabisa rinta ikawa si takwa la lazima kwa kila nyumba. Mimi inavyoona, kama matofali yako compressed / yameshindiliwa vya kutosha, halafu foundation/ msingi uwe imara sana, halafu nyumba ipande juu digrii 90 na siyo 89.99999 au 90.0000001 sioni sababu kwa nini nyumba isiwe imara hata kama itapanda ghorofa 10. Lakini pia nyumba za ulaya mara nyingi floor moja na nyingine hazitenganishwi kwa jamvi la zege ambalo ni zito sana. Zinatenganishwa na mbao ngumu ambazo siyo nzito sana!
 
Ngoja waje kukupa muongozo...
Nadhani hata hao wahandisi wetu wanashangaa na hawana majibu ya uhakika!! Kumbukeni kuwa watu wa mwanzo kabisa walianza kujenga mnara wa babeli kwa kutumia matofali ya kuchoma tu, hapakuwepo na mambo ya zege wala rinta na mnara ulipanda juu sana na kama Mungu asingewachafulia lugha kitu kingepanda hadi mawinguni bila rinta!!
 
lakini pia soil structure yao inawapa favor
Hilo la ugumu wa ardhi ya Ulaya unabahatisha tu, si kweli.

Afrika ndio the oldest and hardest land mass among all of earth's geological formations. Na baadae, wakati Pangea inavunjika vipande na mabara yanatambaa ( tectonic plate drifting) Afrika ilibakia pale pale kwa miaka milioni 200. (John Reader: Africa, Biography of the Continent.)

Ndio maana hata kilimo kilishindikana: changarawe, jiwe, jua kali na dongo gumu na kavu.

Kwenye ujenzi ardhi yetu inapaswa kutupa advantage. Hatujui tu kujenga.

Mimi nimekulia kwenye nyumba ya mkoloni, ya ghorofa, haina nondo, mkanda, jamvi wala zege. Imejengwa kwa beam za mbao unene futi moja. Haikuwahi kuwa na nyufa, mtitio, mchwa, mvujo, kamwe.

0ebb920c8af4c46296be8cf8b11cb8f9f6b6d853.jpg
 
Ok ok ok, ni hivi

Ukifanya structural analysis utagundua kwa nyumba za floor moja kushuka chini, uzito huwa si mkubwa hivyo uzito huo unaweza bebwa na kuta tu na kunakua hakuna haja ya nguzo/column,

Kwa nini tunaweka beam/lenta na column
1. Kuongeza robustness/tightness/ ukazo wa nyumba
2. Taarifa za ardhi/ geotechnical reports za mazingira yetu huwa hazipo hivyo tunaweka lenta kwa ajili ya tahadhari zinazoweza jitokeza.
3. Kwa upande wa floor kuanzia moja, ujenzi wetu tunatumia zaidi floor slab ya zege tofauti na ulaya/USA wanaprefer zaidi mbao kwa partitions. Hivyo uzito ni mkubwa lkn ht wao wanaweka nguzo za bricks sio kwamba hawaweki kbs.

Ila kwa majengo ya zaidi ya floor mbili kutokua na beam sina jibu,

By: nile house designs.
 
Back
Top Bottom