Kwanini Ujenzi wa Ulaya (Ukraine) hawaweki lenta?

Kwanini Ujenzi wa Ulaya (Ukraine) hawaweki lenta?

Kibongo bongo inawezekana ujenge jengo la kawaida au ghorofa usiweke lenta?

Sent using Jamii Forums mobile app
Zipo nyingi Sana mkuu, japo kwa ghorofa naona badala ya beam ya zege inatumika chuma ambayo ukiwa nje haionekani kabisa. Na slab inabebwa na hiyo steel beam. Mfano tembelea majengo mengi ya viwanda vyenye angalau floor 1, utaona hii kitu imetumika Sana. Pia inasaidia kupunguza gharama kuliko zege.
 
Kuna nyumba nikipata nafasi ntapiga picha niweke hapa ..ya ghorofa moja lakini Haina nguzo....wamelaza tofali na msingi wametumia mawe...
 
Huku kwetu kujenga ghorofa bila column inawezekana vizuri bila shida, Ila tofali yako iwe ya uhakika. Ila sijawahi kuona slab bila beam, hiyo ni kitu kipya kwangu.
Pia lenta sio lazima Sana kwenye jengo hasa hizi nyumba za floor moja. Cha muhimu msingi wako uwe mzuri na udongo usiwe mkorofi.
Sasa wale wanaokomalia linta la nondo 4 kwa kijumba Cha chumba sebule
 
Nilipofika Ulaya kwa mara ya kwanza nilifanya kazi kwenye construction sites. Nilishangaa kweli kweli wanamimina zege leo kesho wanaondoa mbao zilizoshikilia zege.
Watakua wanatumia cement Kali sana
 
Back
Top Bottom