Kwanini Ujenzi wa Ulaya (Ukraine) hawaweki lenta?

Kwanini Ujenzi wa Ulaya (Ukraine) hawaweki lenta?

Hapa nmekupata,
Ila za kule Ukraine hata zikibomoka hatuoni hata pande la chuma limeanguka.

Ni totally Hakuna beams

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea matufali ya aina gani, kama matufali ni mepesi basi hiyo frame ya mlango au dirisha inatosha kubeba uzito haina haja ya lintel. Kama Matufali ya kuchonga kwenye mawe ni mepesi sana. Vili vile hizi nyumba za zamani frme zake za milango na madirisha ni heavy duty na zinadumu muda mrefu sana kwa hiyo hazihitaji lintel.
 
Bongo hata mikoan wanakotumia za kuchoma, bado lenta wanafunga.

Kibongo bongo mkandarasi ajenge ghorofa bila beam Wala columns za zege sidhan kama anaweza kueleweka.

Imekua Kama mazoea kufunga ring beams kwa kila jengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilienda zanzibar kipindi flani nikakuta nyumba ina rinta 3, chini, levo ya dirisha, na juu baada ya dirisha
 
Jibi ni wao hujenga kuta mbili kitaalam mjengo huo huitwa CAVITY WALLS
na katikati ya zile kuta huwekwa waya ambao hauonekani unaitwa Tie. Umbo lake kama tai ya shingo
Nilidhani cavity wall ni kwasababu ya baridi maanake pale katikati wanaweza insulating materials
 
Siyo Ukrain tu, hata huku Tanzania vijijini wanajenga nyumba bila lenta ya simenti.

Wanaweka ubao sehemu ya dirisha au mlango na ujenzi unaendelea.

Tena ukiwa umeandaa madirisha na frame za milango ukazijengelea, nyumba inakuwa imara tu.

Na ndio maana hata ukitumia nondo moja kwenye lenta nyumba inakuwa imara tu. Cha msingi weka simenti
kali tu!
 
Makombora yaliyolipuka Dar hayakugusa nyimba ila mtikisiko tu nyumba zilivunjika na lenta zake.
Hizi ni baadhi ya picha za majengo mbalimbali mitaani kutoka uwanja wa Vita uko ukraine.

Kinachoshangaza hata majengo ya serikali (magorofa Hadi nyumba za Kawaida) Nayo hayana beams Wala columns.

Mafundi, Wahandisi, wataalamu wa majengo na wanaJf hebu tufahamishane.

Imekaaje Hii[emoji848]View attachment 2323447View attachment 2323452View attachment 2323454View attachment 2323455View attachment 2323457

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli kwamba hizi ni nyumba za kizamani,
Hili jengo Ni la ubalozi wa Canada nchini Ukraine,

Hii picha imepigwa haina hata mwezi ktk ya Hii Vita, jengo Lina Hadi kiyoyozi[emoji116] View attachment 2323931

Sent using Jamii Forums mobile app
Aina ya tofali na upana wa ukuta?
Sio ukreine tu hata huko kwa malkia
Picha kwa hisani ya google earth.

Halafu mbona wabongo hawapendi ujenzi wa aina hii zaidi naona ni kujitwisha mizigo ya mifuko ya saruji na ndoo za rangi kupendezesha ukuta?
Screenshot_20220817-110006.png
Screenshot_20220817-105640.png
 
Nadhani hata hao wahandisi wetu wanashangaa na hawana majibu ya uhakika!! Kumbukeni kuwa watu wa mwanzo kabisa walianza kujenga mnara wa babeli kwa kutumia matofali ya kuchoma tu, hapakuwepo na mambo ya zege wala rinta na mnara ulipanda juu sana na kama Mungu asingewachafulia lugha kitu kingepanda hadi mawinguni bila rinta!!
Daaa nimecheka sana.
 
Bongo hata mikoan wanakotumia za kuchoma, bado lenta wanafunga.

Kibongo bongo mkandarasi ajenge ghorofa bila beam Wala columns za zege sidhan kama anaweza kueleweka.

Imekua Kama mazoea kufunga ring beams kwa kila jengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa columns , inawezeka kuziacha Kutokana na design.
Ila kwenye beem hapo , labda floor sio ya concrete.

Watakua wa natumia vyuma + mbao.
 
Mzee wangu alijenga nyumba mwaka 1988 bila Renta tena kwa tofari mbichi but mpaka leo hii ipo!!na imeenda hewani tu vizuri,sema imepitwa na wakati kwenye upauaji.
Nyumba hii mzee ataiacha nna uhakika.

Nikirudi kwenye mada yako,nyumba ya kawaida inaweza tu ikajengwa bila renta Ila ukaiwekea virenta Fulani madirishani na milangoni na ikawa vizuri Sana tuu,sema ujenzi wa Sasa si kwa ajili ya kuishi,watu wanajenga ili wapate umaarufu na sifa.(vijana wanajenga kwa kushindana aisee)
 
Kabisa,
Ujue Kuna Hadi nyumba za makuti na udongo zimejengwa miaka ya 80 ila mpk leo zipo strong.
 
Bongo hata mikoan wanakotumia za kuchoma, bado lenta wanafunga.

Kibongo bongo mkandarasi ajenge ghorofa bila beam Wala columns za zege sidhan kama anaweza kueleweka.

Imekua Kama mazoea kufunga ring beams kwa kila jengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huku kwetu kujenga ghorofa bila column inawezekana vizuri bila shida, Ila tofali yako iwe ya uhakika. Ila sijawahi kuona slab bila beam, hiyo ni kitu kipya kwangu.
Pia lenta sio lazima Sana kwenye jengo hasa hizi nyumba za floor moja. Cha muhimu msingi wako uwe mzuri na udongo usiwe mkorofi.
 
Sasa eng kwanini hujafanya utafiti kujua mbona wenzetu wanajenga
Sio kila kitu mfundishwe darasani ubunifu mwngine mnaweza kuongezea wenyewe ni maoni tu lakn [emoji3]
Wazo zuri sana hili, Ila nyumba/jengo la utafiti waje waanze kujenga ya kwako na uishi mwenyewe tuone Kama utakubali.
Kwa ufupi huku kwetu hata Kama unayo idea mpya huwa ni vigum Sana kupata mfuko wa kusapoti hiyo utafiti wako.
 
Back
Top Bottom