Kwanini ukienda hospitali idadi kubwa ya wanaotibiwa ni wanawake?

Kwanini ukienda hospitali idadi kubwa ya wanaotibiwa ni wanawake?

Anachokisema mtoa mada kipo, me nililigundua hili nilipompeleka wife kuanza clinic, asee!
Wanaume wanahesabika zahanati nzima wamejaa wanawake, wanaume wengi wamesindikiza watu wao, na waliokuja kutibiwa unawahesabu kwa vidole.
Yaani 5% kwa 95%
Wanawake wana uwakilishi. Mfano anampeleka mtoto na anaowalea. Mwanaume anapoenda anaenda mwenyewe tu
 
Mwanamke anaumwa kila mwezi unategemea idadi iwe sawa na wanaume hospital..
Ile faragha Yao nafikiri ndio chanzo Cha wao kunyemelewa na magonjwa mengi tofauti na wanaume
 
Asilimia kubwa ya sisi wanaume tuna tabia ya kupuuza maradhi tofauti na kina mama ambao wao kila maumivu huchukulia ni kitu serious.
Mimi binafsi mpaka kwenda hospitali ni iwe nimeshikika hasa.

Pengine ndio maana huwa hata kwenye ndoa tunakufa mapema kabla ya wake zetu.
Haya mambo nimegombana sana na mke wangu,yaan yeye akisikia kuumwa kidogo anataka kwenda hospital na atapima kila kitu hata kama miezi miwil katoka kupima vitu hvyo
 
Hata kwenye maombi Kwa akina mwamposa wengi ni wamama
Anachokisema mtoa mada kipo, me nililigundua hili nilipompeleka wife kuanza clinic, asee!
Wanaume wanahesabika zahanati nzima wamejaa wanawake, wanaume wengi wamesindikiza watu wao, na waliokuja kutibiwa unawahesabu kwa vidole.
Yaani 5% kwa 95%
Ataa
 
Nipo Muhimbili hapa...idadi kubwa ya wagonjwa na wapendwa wao ni wamama ... ni kwamba men hawaumwi!?

No wonder men ndo sababu tunakufa fasta hatuna muda wa kupokea tiba
Tushazoea kujikaza KISABUNI.
 
Halafu wagonjwa wengi ni watu masikini sababu ya lishe duni.
Chakula ni dawa
 
Nipo Muhimbili hapa...idadi kubwa ya wagonjwa na wapendwa wao ni wamama ... ni kwamba men hawaumwi!?

No wonder men ndo sababu tunakufa fasta hatuna muda wa kupokea tiba
Wanajali afya zao. Akijisikia ndivyo sivyo anatafuta matibabu wakati sisi tunajidai wanaume mwisho wake tunaondoka mapema kwa ubishi.
 
Kanisani kwetu Kuna utaratibu wa kusoma idadi ya wanaume na wanawake waliohudhuria Ibadan jumapili iliyopita. Jumapili ya Jana wakatutangazia kwamba jumapili iliyopita akina mama walikuwa 344 na akina baba 88 !
Nenda kachukue idadi kama hiyo kwenye matamasha ya wasanii au kwenye banda la mpira au uwanja wa taifa 🤣
 
Watu wanaotoa hoja tunaumwa ila tunajikaza kiume haina ukweli.
Sababu za kweli hizi hapa
1. Wanawake wanapokea magonjwa kirahisi kuliko wanaume . Mfano mwanamke ni rahisi kupata HIV kuliko mwanaume kulingana na maumbile yao
2. Ulaji wao , wanawake wanakula hovyo kuliko wanaume hasa junk food
3. Uzazi na Malezi mwanamke anahusika zaidi ya 95%
4. Magonjwa kama fangasi , magonjwa ya ngozi, kansa ya matiti, kansa ya kizazi yanashambulia zaidi wanawake
5. Wanawake waishi zaidi kuliko wanaume yani ukifanya sensa ya kuhesabu watu wenye zaidi ya miaka 60+ utakuta kundi kubwa la wanawake kuliko wanaume na umri huo ndio magonjwa ya uzeeni .

NB
Ukienda hosptiali kubwa waambie wakuoneshe idara ya Urolojia utakuta wanaume wamejaa
 
Hata kwa kina Mwamposa nako wamejaa wao.Nijuavyo mimi tofauti na Mwanaume Mwanamke ni muoga na kila dalili kwake ni sawa na ugonjwa kamili,atakimbilia kupata ufumbuzi.Lingine kubwa ni la kimaumbile,viungo vya uumbaji alivyonavyo ni sensitive hata aikwepe vipi Hospitali bado kuna kubeba mimba na kuzaa ataenda tu.
 
... matibabu yangu Napata hapo kwa nesi wa duka la madawa!
Nitakapoenda huko mahospitalini itakuwa ndo niagieni'niagieni yenyewe!
🤣
 
Anachokisema mtoa mada kipo, me nililigundua hili nilipompeleka wife kuanza clinic, asee!
Wanaume wanahesabika zahanati nzima wamejaa wanawake, wanaume wengi wamesindikiza watu wao, na waliokuja kutibiwa unawahesabu kwa vidole.
Yaani 5% kwa 95%
mwanaume anaenda zahanati kutibiwa nini? Zahanati ni kwaajili ya watoto,wajawazito,wazee na wanawake kwa ujumla.
 
Mleta mada ameingia wodi ya akina mama na wanaojifungua sijui anatazamia atapata atawapata wanaume humo?
 
Back
Top Bottom