Nipo Muhimbili hapa...idadi kubwa ya wagonjwa na wapendwa wao ni wamama ... ni kwamba men hawaumwi!?
No wonder men ndo sababu tunakufa fasta hatuna muda wa kupokea tiba
Pamoja kuzingatia aina huduma itolewayo kwenye vituo vya afya, bado tafiti zimeonyesha kuwa jinsi(mwanamke au mwanaume) imekuwa ni moja ya sababu ya utofauti wa mahudhurio kwenye vituo vya afya.
Wanawake wanao mwitikio mkubwa wa kwenda kituo cha afya kwa dalili yoyote anayojisikia au kutokuwa sawa.
Utofauti huu huweza kutokana na:
1: Matarajio kutoka kwenye huduma
Kuna huduma maalumu kwa makundi maalumu ya huduma husika. Hii huweza kuwaleta watu husika kwa wingi. Mfano: huduma za mpango wa uzazi. Hapa mwanamke ndiye mnufaika zaidi kwa mantiki ya mwanaume. Kulingana na malezi ya jamii na tamaduni, wababa hujihusiaha kwa uchache. Nso maana hapa kuna wamama hujiunga na huduma hii hata kwa siri bila kuhuaisha wenzi wao.
2: Malezi
Malezi yetu humjenga kijana wa kiume kuwa mkakamavu/musculinity. Hii humjenha kisaikolojia kutokuwa mwepesi kutoa ishara au kujongea kwa kila kiyu hasi kinachotokea kwenye mwili wake.
2: Unyanyapaa
Unaweza kuwa kwa huduma inavyotolewa inamwonyesha kila anaenda pale hospitalini ni kama anaonyesha unyoge wake/kwa tafsiri ya mwanaume au misingi ya jinsi huduma inavyotolewa huweza kumtweza kifikra mwanaume.
Pia kwenye baadhi ya huduma husika kama kliniki za watoto, ambapo baba huona kama ni jukumu la mama zaidi.
3: Tamaduni
Kwa tamaduni zetu, zinamtaka mwanaume asiwe mtu wa kuonyesha kulalamika kwa sababu ndogondogo. Hii hupelekea hata upande wa ugonjwa kuchukuliwa kiwepesi mpaka dalili zinapokuwa kubwa.
4: Utafutaji/kipato
Baba nso mtafutaji mkuu wa familia/social reaponsibility. Huwa kwenye harakati nyingi za kutafuta kipato , hivyo akibadili ratiba vitu hukwama/husimama pia.
5: Umri
Pia kuna magonjwa yanaathiri zaidi kulingana na jinsi. Mfano: maambukizi ya njia ya mkojo yapo zaidi kwa watoto wa kike. Wakari umri wa kati, watoto wa kike ni wahanga wa kupungukiwa damu sababu ya hedhi pia kuwa ni wahanga wa magonjwa ya ngono, umri mkubwa kuambatana na madhira yake kama menstrual syndrome na kansa aina mbalimbali kutokana na mabadiliko makubwa ya vichocheo/homoni mwilini.
Hizi ni baadhi tu ya sababu zinazofanya mahudhurio ya wamama kwenye vituo vya afua kuwa juu zaidi ya wanaume