Kwanini Ulimwengu unafuata hesabu zilizotoka akilini mwa Binadamu? Vita kali dhidi ya Atheists Ep3

Prof Phraoh AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
1,269
Reaction score
2,311
‎Physicist mkubwa Eugene Wigner aliandika makala maarufu sana aliita
‎
‎"The Unreasonable Effectiveness of Mathematics in the Natural Sciences."
‎
‎Alisema waziwazi na maneno yake ni haya kwa muhtasari:
‎"Ni ajabu isiyoeleweka kwa nini hesabu zilizoundwa bila kujali ulimwengu wa kimwili zinafanya kazi vizuri sana kueleza ulimwengu huo. Hakuna maelezo ya kawaida ya hili."
‎huyu ni mwanasayansi mkubwa anayeheshimika kwa mchango wake kwenye physics.
‎
‎Swali kama ulimwengu ni bahati tu kwa nini unafuata hesabu za akili ya binadamu kwa usahihi huu?
‎
‎Hesabu ni kitu kinachoishi akilini. Hakuna mtu aliyeona namba 7 ikitembelea barabarani. Hakuna aliyegusa equation kwa mkono.
‎Lakini ulimwengu wa kimwili mwamba, maji, nyota unafuata hesabu hizo kwa usahihi wa kushangaza.
‎hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuna uhusiano wa ajabu kati ya ulimwengu wa akili na ulimwengu wa kimwili.
‎Uhusiano huo unatoka wapi kama akili na ulimwengu vilitokea kwa bahati tena kwa muda tofauti
‎
‎Mwaka 1846 mwanasayansi Urbain Le Verrier alitumia hesabu za mvutano (gravity) kuonyesha kwamba kuna sayari isiyoonekana inayovuruga mzunguko wa Uranus. kwa kutumia hesabu pekeyake akaonyesha kabisa ipo wapi angani.
‎Baadaye, mwanasayansi Johann Galle akaangalia kwa darubini sehemu hiyo na kweli sayari hiyo ikapatikana karibu kabisa na hapo ilipoonyeshwa. Sayari hiyo mpya ikaitwa Neptune
‎
‎Newton alitoa theory yake ya gravity miaka ya 1687. Mwaka 1969 hesabu zake zikatumika kuwapeleka binadamu kwenye mwezi, na mpaka sasa hesabu zake zinatumika kurusha roketi angani
‎
‎theory of relativity ya Einstein iliandikwa mwaka 1905 na 1915. Sasa hivi miaka 100 baadae hesabu zake ndo msingi wa GPS
‎
‎miaka 1000 kabla ya satelite, Al-battani alitumia hesabu ili kujua dunia inatumia siku gapi kuzunguka Jua. Al-Battani akaja na jibu akasema:
‎Mwaka una siku 365, Masaa 5, Dakika 46 na sekunde24
‎
‎nakuwekea video fupi kutoka kwenye documentary fulani ili uone kwa ufupi alivyofanya na kupata jibu hilo

‎
‎Leo kwa kuchunguza kwa Satelite tunaona dunia inatumia Siku 365, Masaa 5, Dakika 48 na sekunde 47
‎
‎( Al-battani alikua nyuma kwa dakika 2 tu )
‎
‎
‎Paul dirac aliandika equation yake na hesabu zake zikamfanya agundue ulimwenguni kuna anti-particle. Wkati huo ilikua haiwezi kuthibitishwa kwa namna yoyote kwasababu tecnolojia ilikua chini. leo baada ya miaka 100 sasa tuna tecnolojia ya kisasa anti-particle tunaiona kila siku maabara.
‎
‎Galileo Galilei alisema
‎ “Mathematics is the language in which God has written the universe.”
‎
‎NASA walikuja kuthibitisha hili walipokua wakituma golden disc wakajiuliza swali
‎ je tukikutana na aliens leo tutatumia lugha gani kuwasiliana nao ?
‎wakasema ni hesabu, obviously kiumbe yeyote mwenye akili mahali popote ulimwenguni anajua 1 + 1 ni 2
‎
‎
‎Kuna uwezekano mbili tu wa kueleza hili:
‎Uwezekano wa kwanza ni bahati ya kushangaza sana kwamba akili iliyotokana na evolution inaweza kuelewa ulimwengu wa quantum, cosmos, na hesabu za abstract bahati ambayo haina maelezo.
‎Uwezekano wa pili akili na ulimwengu vina chanzo kimoja. Vimeundwa na kitu kimoja. Kwa hiyo vinafanana kama vitu viwili vilivyotengenezwa na fundi mmoja vinavyofanana.
‎Wigner mwenyewe alisema uwezekano wa kwanza hauridhishi akili.
‎
‎Kama ulimwengu ni bahati tu akili ni bahati tu hesabu ni bahati tu basi bahati hiyo imefanya kitu ambacho hakuna bahati nyingine inaweza kufanya
‎Imeunda akili inayoweza kuuelewa ulimwengu ambao haikuhitajika kuuelewa.
‎Hilo linahitaji maelezo. Na maelezo rahisi zaidi ya kimantiki ni moja kulikuwa na akili kubwa kabla ambayo iliunda akili ndogo na ulimwengu na kuzifanya zifanane.
‎
‎Stephen Hawkins Ambae ni Mwanasayansi maarufu ambae pia alikua Atheist, kwenye moja ya maandiko yake alijiuliza hivi:
‎
‎"What is it that breathes fire into the equations and makes a universe for them to describe?"
‎
 
Jibu rahisi ni evolution, binadamu wameanza kuelewa hesabu za Ulimwengu 1700s, huku nyuma miaka 10,000 BC walikuwa cavemen tu, ancestors wa binadamu kwa zaidi ya miaka milioni tano walikuwa hawajuhi hata moto au kutumia nyenzo kama za chuma n.k

Hawa wanasayansi wanaofikiri Kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya akili ya mwanadamu na scientific laws zinazo governe ulimwengi ni creationists wanaoamini binadamu wameumbwa na binadamu wa kwanza alikuwa Adamu, hawaamini evolution.
 
Jibu rahisi ni evolution, binadamu wameanza kuelewa hesabu za Ulimwengu 1700s, huku nyuma miaka 10,000 BC walikuwa cavemen tu
evolution sio jibu kabisa kwasababu akili inge evolve kujilinda, kutafuta chakula etc

kwanini akili inaelewa quantum physics, inaelewa black holes galaxies, ime evolve vipi kuelewa kwa undani vitu kama hivi
 
Mbona hata kwenye vitabu vya mungu anaelezea kuhusu ulimwengu unavyoweza kutoa majibu kuhusu hesabu au ulitaka kitabu cha m.mungu kikufundishe logarithm ndio uamini Soma huu mstari kwenye moja ya kitabu cha m.mungu

" Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili za uwezo wetu tukautoa mwanga usiku ukawa kiza na mchana tukauweka mwanga ili kwenye huo mchana mtafute riziki fadhila itokayo kwa mungu wenu na mpate kujua idadi ya miaka na hesabu" Israel Aya 12
Hata huyo al battali pengine uelewa wa hesabu za siku kwenye mwaka kwa kufata kanuni hizo hizo
 
Huwezi kuipangia evolution process iishie wapi kama vile ambavyo hukuipangia ianzie wapi, pia binadamu sio lengo, pinnacle, end result au center ya evelution, binadamu sio hata center ya universe, ni mojawapo tu kati ya mabilioni ya viumbe waliokuwa shaped na evolution.
 
Huwezi kuipangia evolution process iishie wapi kama vile ambavyo hukuipangia ianzie wapi, pia binadamu sio lengo, pinnacle, end result au center ya evelution, binadamu sio hata center ya universe, ni mojawapo tu kati ya mabilioni ya viumbe waliokuwa shaped na evolution
‎Evolution inaweza kueleza kwa nini akili yetu inajua kuepuka simba, kutafuta chakula, kujenga makazi mambo ya maisha ya kila siku.
‎Lakini evolution haielezi kwa nini akili yetu inaweza kuelewa quantum mechanics ulimwengu mdogo sana ambao hatuuoni, hatuugusi, hauna uhusiano wowote na kuishi au kufa.
‎haielezi kwa nini tunaweza kuelewa black holes umbali wa miaka bilioni ya mwanga ambao hauna uhusiano wowote na survival yetu.
‎haielezi kwa nini hesabu za abstract zilizoundwa kwa mchezo wa kiakili tu zinafanana na muundo wa ulimwengu ambao evolution haikutuandalia kuuelewa.
‎Evolution ilitengeneza akili ya kuishi si akili ya kuelewa cosmos. Lakini akili hiyo hiyo inaweza kuelewa cosmos. Kwa nini?

Uta evolve vipi kwa kitu ambacho hauna uhusiani nacho hata kidogo, wantama na binadamu tuna evolve kutokana na mazingira yanayotuzinguka tu Yoda
 
Mbona hata kwenye vitabu vya mungu anaelezea kuhusu ulimwengu unavyoweza kutoa majibu kuhusu hesabu au ulitaka kitabu cha m.mungu kikufundishe logarithm ndio uamini Soma huu mstari kwenye moja ya kitabu cha m.mungu

" Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili za uwezo wetu tukautoa mwanga usiku ukawa kiza na mchana tukauweka mwanga ili kwenye huo mchana mtafute riziki fadhila itokayo kwa mungu wenu na mpate kujua idadi ya miaka na hesabu" Israel Aya 12
Hata huyo al battali pengine uelewa wa hesabu za siku kwenye mwaka kwa kufata kanuni hizo hizo
sijaelewa upo upande gani ?
 
‎Evolution inaweza kueleza kwa nini akili yetu inajua kuepuka simba, kutafuta chakula, kujenga makazi mambo ya maisha ya kila siku.
‎Lakini evolution haielezi kwa nini akili yetu inaweza kuelewa quantum mechanics ulimwengu mdogo sana ambao hatuuoni, hatuugusi, hauna uhusiano wowote na kuishi au kufa.
‎haielezi kwa nini tunaweza kuelewa black holes umbali wa miaka bilioni ya mwanga ambao hauna uhusiano wowote na survival yetu.
‎haielezi kwa nini hesabu za abstract zilizoundwa kwa mchezo wa kiakili tu zinafanana na muundo wa ulimwengu ambao evolution haikutuandalia kuuelewa.
‎Evolution ilitengeneza akili ya kuishi si akili ya kuelewa cosmos. Lakini akili hiyo hiyo inaweza kuelewa cosmos. Kwa nini?

Uta evolve vipi kwa kitu ambacho hauna uhusiani nacho hata kidogo, wantama na binadamu tuna evolve kutokana na mazingira yanayotuzinguka tu Yoda
 
Attachments

  • Screenshot_20260416-093800~2.jpg
    Screenshot_20260416-093800~2.jpg
    201.1 KB · Views: 30
  • Screenshot_20260416-093813~2.jpg
    Screenshot_20260416-093813~2.jpg
    218.1 KB · Views: 22
  • Screenshot_20260416-093835~3.jpg
    Screenshot_20260416-093835~3.jpg
    223.1 KB · Views: 26
  • Screenshot_20260416-093917~2.jpg
    Screenshot_20260416-093917~2.jpg
    262.3 KB · Views: 28
okay ngoja tuanzie nyuma kidogo, ili uelewe nilichokua nikikwambia. Conciousness imetoka wapi na ubongo umewezaje kuwa compatible na mazingira kiasi cha kuweza ku evolve kutokana na mazingira.

pendekezo: tumia maneno yako badala ya screenshot za gemini ai kwasababu nina uhakika haina mtiririko mzima wa mada zimeanzia wapi.
ningeomba utafute fact zako huko kisha uje uniambie hapa kwa maneno yako badala ya kuja na screenshot uliyoibeba na kuja kuibandika

pia kwenye post yangu nimetoa mifano kadhaa, yote ukiangalia ina muelekeo mmoja: mtu alifanya calculation zake kichwani na kwenye karatasi, bila yeye kujua zitatumika wapi lakini baadae zinatumika kwenye ulimwengu wa uhalisia, kurusha roketi, satellite na kadhalika
 
Hakuna jambo kubwa sana unalo jadili hapa mkuu, hii ni hoja dhaifu sana katika kuthibitisha uwepo wa mungu ndio maana hata ni nadra sana kutumika na theists kwenye mijadala. Binadamu kuelewa physics na astrophysics ni kama alivyoelewa mambo mengine yote tu, hakuna kitu cha kipekee sana kuthibitisha hiyo ni ishara ya uumbaji.

Pia hayo mawazo yako ni kwa sababu unawazia katika matrilioni ya galaxies na sayari uhai na viumbe wenye akili wako katika sayari moja tu ya duniani, hujawahi kuwazi labda kumewahi kuwepo au zipo civilizations katika sayari nyingine zenye viumbe wenye sayansi na teknolojia hata mara elfu moja zaidi yetu.

Ukilazimisha sana kwamba ubongo wa binadamu na uelewa wake kuhusu physics sio nasibu bali ni uumbaji wa makusudi utarudishwa kule kule tu kutakiwa ueleze na uthibitishe ni nani aliyemuumba huyo aliyeumba ubongo wa binadamu unaohusiana na sheria za ulimwengu na god of gaps fallacy.

Conscious ni mjadala mwingine kabisa.
 
‎naomba usome kwaa hatua kwasababu nataka kukujibu kwa kina na kwa upole kabisa labda kuna kitu uta toka nacho

umesema hoja ni dhaifu lakini sijaona ukiijibu.
‎kusema ni nadra kutumika si kujibu. mimi nimeitumia kwasababu najua huwezi kujibu
‎Niambie kwa usahihi kwa nini hesabu zilizoundwa akilini zinafanya kazi ulimwengu wa kimwili? Hiyo ndiyo swali. lipe jibu si tathmini yako ya ubora wa swali.
‎
‎Umesema labda kuna civilizations nyingine zenye akili kubwa zaidi.
‎ni sawa ( labda ) lakini mdogowangu Yoda hilo halishughulikii swali langu hata kidogo.
‎Swali langu si je binadamu ni wa kipekee? Swali langu ni hili: ngoja ni highlight
‎
‎Kwa nini kiumbe chochote binadamu, alien, au kingine kinachoundwa na atomu za ulimwengu huu kinaweza kuunda hesabu akilini mwake ambazo zinafanana na muundo wa ulimwengu huo?
‎
‎Hata kama aliens wako wao pia watatumia hesabu hizo hizo. Wigner alizungumza kuhusu hesabu yenyewe si binadamu peke yake nikatoanmfano wa NASA walisema lugha watakayo tumia kuongea na Alisens ni hesabu kwasababu haijalishi mahali popote ulimwengu 1 + 1 = 2.
‎ Aliens wakizigundua hesabu hizo swali bado lipo palepale: kwanini bado zinafanya kazi ?
‎
‎God of Gaps inasema hivi Yoda
‎
‎"sijui kitu fulani kwa hiyo jibu ni Mungu."
‎
‎ Hoja yangu inasema hivi mdogowangu
‎
‎ "naona pattern ya wazi na maelezo ya kimantiki ni kuna akili kubwa nyuma yake."
‎
‎Hizi ni hoja tofauti kabisa. kwaiyo kama unahisi ni God of gaps nenda kajifunze upya Gid of gaps ni nini
‎
‎Mwisho kabisa nisisitize hii umesema hoja yangu ni dhaifu sawa. Sasa nionyeshe udhaifu wake kwa kujibu maswali matatu rahisi tu, ( nitazibhiglit ili uzione vizuri
‎
‎Moja kwa nini hesabu za akili zinafanya kazi ulimwenguni wa kimwili?
‎
‎Mbili kwa nini kuna uzoefu wa ndani consciousness badala ya giza tu?
‎
‎
‎Tatu kama majibu yako ni sijui kwa maswali haya mawili kwa nini sijui ni jibu bora zaidi kuliko jibu langu ?
‎
‎
‎Maswali haya hayajajibiwa na sayansi hadi leo si kwa sababu ya ujinga wangu hata Wigner, Hawking, na Chalmers walikubali hawajui
‎
‎ndo maana post yangu ya kwanza ya kuanzisha mada nilitoa mifano hai na nikawekana maswalinyao kwaiyo Yoda unaweza ukawajibia kwasababu sahivi wenyewe hawapo tena duniani
 
huu uzi Atheists wanaupita kimya kama vile wanatoa salamu za mwisho,

ni masaa 5 sasa najadiliana na mtu mmoja ambae ni atheist, tofauti na nyuzi zilizotangulia ambazo kwa kawaida Atheists huzishambulia kwa kasi.

kwa Sisi tunaoamnini uwepo wa Mungu ( Theists )
hii ni alama ya usindi

kuishiwa kwa hoja kwa Atheists na kubaki na jibu la sijui kwa maswali yanayoulizwa huku wakidai wanajua kwa uhakika Hakuna Mungu inathibitisha kuwa wana kisia au wana hisi au wana Amini Hakuna Mungu. Lakini si kwamba wanajua kwa uhakika

wakizidi kukaa kimya ndani ya masaa 48 nitakua na uhakika kua hawana cha kujibu na nitaendelea na episode zinazo fuata hadi pale nitakapo baki mwenyewe kujiongelesha
 
maoni yangu hapa nitaanzia mbali kidogo kwanza kwa kuunganisha MATHS, SCIENCE na TECHNOLOGY, nina hakika kufanya hivi italeta maana zaidi ili kuelezea MATHS na kanuni za ulimwengu.
mathematics.png

SCIENCE, MATHS sio kitu kipya,
Sayansi ni asili ya vitu (jinsi kila kitu kilivyo na jinsi kinavyofanya kazi),
Sayansi na Maths ni harakati za mwanadamu ili kuelewa ulimwengu upoje na unafanya kazi kwa kanuni zipi.

Simply, SAYANSI - ni systematic study of nature (asili), Watu hujifunza na kuchunguza asili ya vitu, na kujiuliza (reasoning, critical thinking, cognition, n.k) kwa majaribio ya kitaalamu kwa nini hiki kipo hivi na sio vile,
Je nikiweka hivi au vile kitakuwaje? so as to understand the natural principles (kanuni za asili) ambazo zinafanya vitu viwe jinsi vilivyo.

TEKNOLOJIA - matumizi ya maarifa ya sayansi ili kurahisisha kazi, kutatua changamoto za kibiashara, kilimo, kiusafiri, kielimu, kiujenzi, kijeshi, kimatibabu, kimawasiliano, ki-uhandisi, n.k.

MATHS.
ili kuelewa hizi Kanuni za ulimwengu, ndo mwanadamu akaja na Mathematics (numbers) ili iwe rahisi kuelezea kanuni (principles) za vitu mbalimbali jinsi vilivyo in nature, na jinsi ulimwengu (universe) ulivyo.

Therefore, Ulimwengu haufati kanuni za binadamu, bali binadamu ndiye anayefata kanuni za ulimwengu.

Sabb, kanuni za ulimwengu zipo tu kiasili, MATHS ni mbinu ya vipimo (measurements) au lugha ya kisayansi iliyosanifiwa na mwanadamu ili kurahisisha kuelewa kanuni mbalimbali zinazoendesha ulimwengu, life, things (matter).

Hivyo, MATHS na Science ni mbinu tu ili kusaidia watu waelewe nature of things na principles which govern life, things (matter) and universe.
 
huu uzi Atheists wanaupita kimya kama vile wanatoa salamu za mwisho,

ni masaa 5 sasa najadiliana na mtu mmoja ambae ni atheist, tofauti na nyuzi zilizotangulia ambazo kwa kawaida Atheists huzishambulia kwa kasi.

kwa Sisi tunaoamnini uwepo wa Mungu ( Theists )
hii ni alama ya usindi

kuishiwa kwa hoja kwa Atheists na kubaki na jibu la sijui kwa maswali yanayoulizwa huku wakidai wanajua kwa uhakika Hakuna Mungu inathibitisha kuwa wana kisia au wana hisi au wana Amini Hakuna Mungu. Lakini si kwamba wanajua kwa uhakika

wakizidi kukaa kimya ndani ya masaa 48 nitakua na uhakika kua hawana cha kujibu na nitaendelea na episode zinazo fuata hadi pale nitakapo baki mwenyewe kujiongelesha
ninaacha shughuli zangu za mihangaiko kwa saa 48 ili kufuatilia uzi huu secretarybird
 
‎naomba usome kwaa hatua kwasababu nataka kukujibu kwa kina na kwa upole kabisa labda kuna kitu uta toka nacho

umesema hoja ni dhaifu lakini sijaona ukiijibu.
‎kusema ni nadra kutumika si kujibu. mimi nimeitumia kwasababu najua huwezi kujibu
‎Niambie kwa usahihi kwa nini hesabu zilizoundwa akilini zinafanya kazi ulimwengu wa kimwili? Hiyo ndiyo swali. lipe jibu si tathmini yako ya ubora wa swali.
‎
‎Umesema labda kuna civilizations nyingine zenye akili kubwa zaidi.
‎ni sawa ( labda ) lakini mdogowangu Yoda hilo halishughulikii swali langu hata kidogo.
‎Swali langu si je binadamu ni wa kipekee? Swali langu ni hili: ngoja ni highlight
‎
‎Kwa nini kiumbe chochote binadamu, alien, au kingine kinachoundwa na atomu za ulimwengu huu kinaweza kuunda hesabu akilini mwake ambazo zinafanana na muundo wa ulimwengu huo?
‎
‎Hata kama aliens wako wao pia watatumia hesabu hizo hizo. Wigner alizungumza kuhusu hesabu yenyewe si binadamu peke yake nikatoanmfano wa NASA walisema lugha watakayo tumia kuongea na Alisens ni hesabu kwasababu haijalishi mahali popote ulimwengu 1 + 1 = 2.
‎ Aliens wakizigundua hesabu hizo swali bado lipo palepale: kwanini bado zinafanya kazi ?
‎
‎God of Gaps inasema hivi Yoda
‎
‎"sijui kitu fulani kwa hiyo jibu ni Mungu."
‎
‎ Hoja yangu inasema hivi mdogowangu
‎
‎ "naona pattern ya wazi na maelezo ya kimantiki ni kuna akili kubwa nyuma yake."
‎
‎Hizi ni hoja tofauti kabisa. kwaiyo kama unahisi ni God of gaps nenda kajifunze upya Gid of gaps ni nini
‎
‎Mwisho kabisa nisisitize hii umesema hoja yangu ni dhaifu sawa. Sasa nionyeshe udhaifu wake kwa kujibu maswali matatu rahisi tu, ( nitazibhiglit ili uzione vizuri
‎
‎Moja kwa nini hesabu za akili zinafanya kazi ulimwenguni wa kimwili?
‎
‎Mbili kwa nini kuna uzoefu wa ndani consciousness badala ya giza tu?
‎
‎
‎Tatu kama majibu yako ni sijui kwa maswali haya mawili kwa nini sijui ni jibu bora zaidi kuliko jibu langu ?
‎
‎
‎Maswali haya hayajajibiwa na sayansi hadi leo si kwa sababu ya ujinga wangu hata Wigner, Hawking, na Chalmers walikubali hawajui
‎
‎ndo maana post yangu ya kwanza ya kuanzisha mada nilitoa mifano hai na nikawekana maswalinyao kwaiyo Yoda unaweza ukawajibia kwasababu sahivi wenyewe hawapo tena duniani
Usiniite mdogo wako
 
Back
Top Bottom