Physicist mkubwa Eugene Wigner aliandika makala maarufu sana aliita
"The Unreasonable Effectiveness of Mathematics in the Natural Sciences."
Alisema waziwazi na maneno yake ni haya kwa muhtasari:
"Ni ajabu isiyoeleweka kwa nini hesabu zilizoundwa bila kujali ulimwengu wa kimwili zinafanya kazi vizuri sana kueleza ulimwengu huo. Hakuna maelezo ya kawaida ya hili."
huyu ni mwanasayansi mkubwa anayeheshimika kwa mchango wake kwenye physics.
Swali kama ulimwengu ni bahati tu kwa nini unafuata hesabu za akili ya binadamu kwa usahihi huu?
Hesabu ni kitu kinachoishi akilini. Hakuna mtu aliyeona namba 7 ikitembelea barabarani. Hakuna aliyegusa equation kwa mkono.
Lakini ulimwengu wa kimwili mwamba, maji, nyota unafuata hesabu hizo kwa usahihi wa kushangaza.
hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuna uhusiano wa ajabu kati ya ulimwengu wa akili na ulimwengu wa kimwili.
Uhusiano huo unatoka wapi kama akili na ulimwengu vilitokea kwa bahati tena kwa muda tofauti
Mwaka 1846 mwanasayansi Urbain Le Verrier alitumia hesabu za mvutano (gravity) kuonyesha kwamba kuna sayari isiyoonekana inayovuruga mzunguko wa Uranus. kwa kutumia hesabu pekeyake akaonyesha kabisa ipo wapi angani.
Baadaye, mwanasayansi Johann Galle akaangalia kwa darubini sehemu hiyo na kweli sayari hiyo ikapatikana karibu kabisa na hapo ilipoonyeshwa. Sayari hiyo mpya ikaitwa Neptune
Newton alitoa theory yake ya gravity miaka ya 1687. Mwaka 1969 hesabu zake zikatumika kuwapeleka binadamu kwenye mwezi, na mpaka sasa hesabu zake zinatumika kurusha roketi angani
theory of relativity ya Einstein iliandikwa mwaka 1905 na 1915. Sasa hivi miaka 100 baadae hesabu zake ndo msingi wa GPS
miaka 1000 kabla ya satelite, Al-battani alitumia hesabu ili kujua dunia inatumia siku gapi kuzunguka Jua. Al-Battani akaja na jibu akasema:
Mwaka una siku 365, Masaa 5, Dakika 46 na sekunde24
nakuwekea video fupi kutoka kwenye documentary fulani ili uone kwa ufupi alivyofanya na kupata jibu hilo
View attachment 3573435
Leo kwa kuchunguza kwa Satelite tunaona dunia inatumia Siku 365, Masaa 5, Dakika 48 na sekunde 47
( Al-battani alikua nyuma kwa dakika 2 tu )
Paul dirac aliandika equation yake na hesabu zake zikamfanya agundue ulimwenguni kuna anti-particle. Wkati huo ilikua haiwezi kuthibitishwa kwa namna yoyote kwasababu tecnolojia ilikua chini. leo baada ya miaka 100 sasa tuna tecnolojia ya kisasa anti-particle tunaiona kila siku maabara.
Galileo Galilei alisema
“Mathematics is the language in which God has written the universe.”
NASA walikuja kuthibitisha hili walipokua wakituma golden disc wakajiuliza swali
je tukikutana na aliens leo tutatumia lugha gani kuwasiliana nao ?
wakasema ni hesabu, obviously kiumbe yeyote mwenye akili mahali popote ulimwenguni anajua 1 + 1 ni 2
Kuna uwezekano mbili tu wa kueleza hili:
Uwezekano wa kwanza ni bahati ya kushangaza sana kwamba akili iliyotokana na evolution inaweza kuelewa ulimwengu wa quantum, cosmos, na hesabu za abstract bahati ambayo haina maelezo.
Uwezekano wa pili akili na ulimwengu vina chanzo kimoja. Vimeundwa na kitu kimoja. Kwa hiyo vinafanana kama vitu viwili vilivyotengenezwa na fundi mmoja vinavyofanana.
Wigner mwenyewe alisema uwezekano wa kwanza hauridhishi akili.
Kama ulimwengu ni bahati tu akili ni bahati tu hesabu ni bahati tu basi bahati hiyo imefanya kitu ambacho hakuna bahati nyingine inaweza kufanya
Imeunda akili inayoweza kuuelewa ulimwengu ambao haikuhitajika kuuelewa.
Hilo linahitaji maelezo. Na maelezo rahisi zaidi ya kimantiki ni moja kulikuwa na akili kubwa kabla ambayo iliunda akili ndogo na ulimwengu na kuzifanya zifanane.
Stephen Hawkins Ambae ni Mwanasayansi maarufu ambae pia alikua Atheist, kwenye moja ya maandiko yake alijiuliza hivi:
"What is it that breathes fire into the equations and makes a universe for them to describe?"