mkuu point zako ni halisi kabisa ndiyo wanasayansi waliunda hesabu kulingana na patterns walizoziona sahihi.
pia ni swa, kuna confirmation bias hatari katika mjadala wowote nakubaliana na hilo ni onyo zuri.
lakini pointi hizo hazifiki tatizo la msingi na hapa ndipo tutakapoingia.
Umesema ninaonyesha theories zilizofanikiwa tu na hilo ni haki.
lakini angalia hoja yangu kwa makini sionkwamba hesabu zote zinafanya kazi hoja yangu ni tofauti kabisa:
namaanisha hivi mkuu
Ibn Unuq
Kwa nini akili ya binadamu inaweza kuunda hesabu yoyote inayofanana na muundo wa ulimwengu hata mara moja?
Hata kama theories nyingi zimetupwa bado kuna theories zilizofanikiwa. Na swali ni hilo kwa nini zipo kabisa?
mfano rahisi chukulia napiga risasi gizani mara elfu na moja inapiga shabaha palepale swali si kwa nini nyingine zilipotea.
Swali ni kwa nini moja ilifika kama sikuwa na dira yoyote ?
Akili ya binadamu ina dira fulani inayoifanya igundua patterns za ulimwengu dira hiyo inatoka wapi?"
pa kuhusu equetions kurekebishwa angalia kinachoendelea pale zinapoboreshwa:
Newton aligundua gravity Einstein aliboresha lakini Einstein hakusema Newton alikosea kabisa alisema Newton alikuwa sahihi kwa kiwango fulani na yeye akaenda mbali zaidi.
Hii inamaanisha akili ya binadamu inazidi kukaribia ukweli wa ulimwengu polepole lakini inakaribia na ina dira inayoiwezesha.
Kuzidi kukaribia ukweli kunamaanisha ukweli huo upo unangoja kugundulika.
ukweli unaongoja kugundulika uliwekwa na nani?
oia kuhusu unataka nikwambie Mungu ni nini basi acha nikwambie maana nimesharudia mara kwa mara siongei kuhusu Mungu wa dini fulani wala siongei mtu anayekaa mawinguni ana ndevu hapana.
kama ulivyosema hujui pia na kweli akili ya binadamu haina uwezo wa kujua gitu vingi mfano binadamu hawezi kuelewa 4th dimension lakini anaona parten na anajua ipo
mimi naona pattern inayonielekeza, na pattern hiyo inaelekeza kwenye Akili Kubwa kuliko yote.
Sijui kila kitu kuhusu akili hiyo lakini naona alama zake kila mahali Kitu hicho chenye uwezo wa kuweka kanuni, mpangilio, na akili nacho ni Supernatural Intelligence akili Kubwa.
Sisi wengine tunaita Mungu. Unaweza kukiita jina lolote lakini swali ni kama kipo sio jina lake.