Kwanini umri wa dunia unatofautiana sana na wa binadamu wa kwanza

Kwanini umri wa dunia unatofautiana sana na wa binadamu wa kwanza

temoin

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2025
Posts
311
Reaction score
708
Kwa mujibu wa wanasayansi dunia toka kuumbwa kwake hadi sasa ni takribani miaka billion 4.5 iliyopita,(huo ndo umri halisi wa dunia).

Mwaka 1935 ndani ya mamlaka ya hifadhi ya NGORONGORO katika eneo la olduvai george mwanasayansi Louis leakey na mkewe Mary leakey waligundua fuvu la binadamu wa kale Australopithecus boisei (ZINJATHROPUS) ambaye inasadikika kuwa ndo binadamu wa kwanza kuishi hapa duniani takribani miaka million 3.5 iliyopita. Ukiangalia kwa harakaharaka hapo ni tofauti ya miaka mingi sana.

Hatujui Mungu alikaa mda gani kumuumba binadamu wa kwanza alipomaliza kuiumba dunia ila biblia inatueleza kuwa, siku ile Mungu alipoziumba mbingu na nchi hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipukabado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi.

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mafumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi haï.(mwanzo2:5-7). Haijulikani Adam aliumbwa baada ya mda gani toka kuumbwa kwa ulimwengu ila tu tunajua kuwa Adam aliishi miaka mia tisa na thelathini.

Je, kati ya adam na zinjathropus ni nani binadamu halisi wa kwanza kuishi hapa duniani,Labda tutapata jibu sahihi siku likigundulika fuvu la adam
 
Tafiti bado zinaendelea kufanyika na sisi bado tunaendelea kufuatilia kwa sababu sayansi inakuja na fact pamoja na evidénce ukilinganisha na dini ambayo mara nyingi inaonekana na wéngi kuwa ni vitu vya kufikirika
 
Aisee yani unataka kufananisha mawe na binadamu yanaweza kuwa sawa umri.
Tunaposema umri wa dunia tunatafuta mwamba ambao utakuwa na umri mrefu kuliko mwamba wowote.
Mwamba huu ulipatikana kanada na ndio umetoa uthibitisho tokea mwanzo wa dunia kuwa ndio wenye umri wa dunia.
Kwa nini uwe mwamba uo?.
Sababu ya kusema mwamba una umri wa dunia kuna kitu kinaitwa ukusanyaji wa data kijiolojia katika ulinganishi wa carborn 14 kama walivyo chagua ndio ikapatika umri wa mwamba uo.
Mwamba mkongwe kabisa unaojulikana duniani umepatikana nchini Kanada, katika eneo la Hudson Bay, jimbo la Quebec. Miamba hiyo inakadiriwa kuwa na umri wa takribani 4.28 bilioni ya miaka. Dunia inakadiriwa kuwa na umri wa takriban 4.54 bilioni ya miaka, hivyo miamba hii ni karibu sana na umri wa dunia.

1722045441013.jpg


Upande wa mwanadamu uwezi kulinganisha mwanadamu na umri wa dunia sababu wakati dunia inaelekea kuwa kwenye maisha kulikuwa hakuna mazingira ya daraja pa viumbe ambavyo ni sisi sote vingeweza kustahimili mazingira yale ya mwanzoni.

Someni sana nchi za watu achana na kukalia michezo ya simba na yanga.

SOMA HAPA UFAFANUZI;
Viumbe vya kwanza kuishi duniani kabla ya binadamu vilianza kuwepo mamilioni hadi mabilioni ya miaka iliyopita.

1.Viumbe wa Seli Moja (Microorganisms) – Zaidi ya miaka bilioni 3.5 iliyopita​


  • Bakteria na Archaea: Hawa ndio viumbe wa kwanza kabisa waliotokea. Wanaishi katika mazingira magumu sana (kama kwenye volkano, bahari ya chumvi kali, nk).
  • Cyanobacteria: Aina ya bakteria waliokuwa wa kwanza kufanya photosynthesis, wakaanza kutoa oksijeni katika angahewa (karibu miaka bilioni 2.5 iliyopita).View attachment 3356731

2.Viumbe vya Majini Vya Seli Nyingi – Zaidi ya miaka milioni 600 iliyopita

  • Wakati huu viumbe kama sponji za baharini, meduza, na aina za kwanza za minyoo waliibuka.
  • Wengi wao walikuwa hawana mifupa wala uti wa mgongo.

3. Viumbe wenye Miili Migumu (Cambrian Explosion) – Takriban miaka milioni 540 iliyopita​


  • Kipindi cha Cambrian kilishuhudia mlipuko wa aina nyingi mpya za viumbe.
  • Waliibuka viumbe kama trilobites, moluska, na arthropoda (jamii ya kaa na wadudu).
  • Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa viumbe kuwa na macho, miguu, na mifumo tata ya mwili.

4. Samaki wa Kwanza – Miaka milioni 500–400 iliyopita​


  • Samaki wa kwanza walikuwa na uti wa mgongo (vertebrates).
  • Baadhi walikuwa na taya, wengine hawakuwa nayo.

5. Amphibia na Reptilia – Miaka milioni 370–300 iliyopita​


  • Viumbe vya kwanza kutoka majini hadi nchi kavu (kama amphibians).
  • Kisha wakafuatwa na reptilia kama mababu wa mamba na mijusi.

6. Dinosauri – Miaka milioni 230–65 iliyopita​


  • Walitawala dunia kwa muda mrefu kabla ya kuangamia kutokana na tukio la kimondo (asteroid).
  • Wana uhusiano wa karibu na ndege wa kisasa.

7. Wanyama wa Mifupa ya Mgongo Kama Mamalia – Miaka milioni 200 iliyopita​


  • Baada ya kupotea kwa dinosaurs, mamalia wakaanza kutawala.
  • Primates (wanyama wa jamii ya sokwe) walitokea miaka milioni 60–50 iliyopita.

8. Binadamu wa Awali (Hominins) – Takriban miaka milioni 6 iliyopita​


  • Binadamu wa kisasa (Homo sapiens) waliibuka miaka takriban 300,000 iliyopita.

Mfano Rahisi wa Kuelewa​


Fikiria historia ya dunia kama kalenda ya mwaka mmoja:


  • Dunia ilizaliwa tarehe 1 Januari.
  • Maisha ya kwanza yalionekana karibu Machi.
  • Dinosaurs waliishi karibu Desemba 13–26.
  • Binadamu wa kisasa walitokea sekunde chache kabla ya saa sita usiku tarehe 31 Desemba.
 
Aisee yani unataka kufananisha mawe na binadamu yanaweza kuwa sawa umri.
Tunaposema umri wa dunia tunatafuta mwamba ambao utakuwa na umri mrefu kuliko mwamba wowote.
Mwamba huu ulipatikana kanada na ndio umetoa uthibitisho tokea mwanzo wa dunia kuwa ndio wenye umri wa dunia.
Kwa nini uwe mwamba uo?.
Sababu ya kusema mwamba una umri wa dunia kuna kitu kinaitwa ukusanyaji wa data kijiolojia katika ulinganishi wa carborn 14 kama walivyo chagua ndio ikapatika umri wa mwamba uo.

Upande wa mwanadamu uwezi kulinganisha mwanadamu na umri wa dunia sababu wakati dunia inaelekea kuwa kwenye maisha kulikuwa hakuna mazingira ya daraja pa viumbe ambavyo ni sisi sote vingeweza kustahimili mazingira yale ya mwanzoni.

Someni sana nchi za watu achana na kukalia michezo ya simba na yanga
Na vipi kwa binadamu yeye aliumbwa na mungu baada ya mda gani. Tiririka mkuu
 
Evolution
Kwenye hili kidogo linanitatiza kwasababu kwenye biblia hakuna maelezo mengi yanayohusu dunia zaidi ya kuelezea uumbaji katika kitabu cha mwanzo
 
Kwenye hili kidogo linanitatiza kwasababu kwenye biblia hakuna maelezo mengi yanayohusu dunia zaidi ya kuelezea uumbaji katika kitabu cha mwanzo
Soma kitabu cha enoki ndio kinaeleza mengi na kwa nini kilitolewa kwenye biblia.
 
Tafiti bado zinaendelea kufanyika na sisi bado tunaendelea kufuatilia kwa sababu sayansi inakuja na fact pamoja na evidénce ukilinganisha na dini ambayo mara nyingi inaonekana na wéngi kuwa ni vitu vya kufikirika
Sayansi haina facts wanakuaminisha wanachotaka kuamini ,sayansi inabadilika kulingana na muda ...
 
Tatizo lako linaanzia hapa
Kwa mujibu wa wanasayansi
Hapa umetumia dhana ya kisayansi
Hatujui Mungu alikaa mda gani
Halafu ukatumia dhana ya uumbaji
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mafumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi haï.(mwanzo2:5-7).
Ukamalizia kwa bible
Hapo umeongelea kitu kimoja lkn kwa nadharia mbili tofauti halafu unataka jibu lifanane never ever.
Sayansi inautazama ulimwengu(universe) na utokeaji wake tofauti na nadharia za uumbaji na kwenye nadharia ya uumbaji pia ina tofauti ndogo ndogo baina ya imani moja na nyingine
 
Sayansi haina facts wanakuaminisha wanachotaka kuamini ,sayansi inabadilika kulingana na muda ...
Na vipi dini kwenye hili limekaaje maana dini ni maandiko tu ila sayansi ni ushahidi
 
Kama tukiangalia kwa mtazamo wa sayansi, Zinjanthropus ni miongoni mwa viumbe wa mwanzo wanaofanana na binadamu. Lakini kwa mtazamo wa kiimani/kidini, Adam ndiye binadamu wa kwanza halisi aliyeumbwa na Mungu kwa mfano wake (in His image).

Hivyo basi, jibu linategemea na mtazamo wako uko wapi:
Science says: Zinjanthropus was among the earliest hominids.
Faith says: Adam is the first true human created by God.
 
Tatizo lako linaanzia hapa

Hapa umetumia dhana ya kisayansi

Halafu ukatumia dhana ya uumbaji

Ukamalizia kwa bible
Hapo umeongelea kitu kimoja lkn kwa nadharia mbili tofauti halafu unataka jibu lifanane never ever.
Sayansi inautazama ulimwengu(universe) na utokeaji wake tofauti na nadharia za uumbaji na kwenye nadharia ya uumbaji pia ina tofauti ndogo ndogo baina ya imani moja na nyingine
Nimejaribu kulinganisha tu kupata uhalisia maana bible first human ni adam na sayansi ni ZINJATHROPUS
 
Na vipi dini kwenye hili limekaaje maana dini ni maandiko tu ila sayansi ni ushahidi
Hakuna ushahidi ,sayansi imebase kwenye kuteteq jambo hilo : Sawa ukisema wale wa dunia duara na flat wote wana hoja ...Sayansi inakufanya uweze kuteteq kile kitu kwa kuwaaminisha watu ,huo ndiyo msingi mkubwa wa sayansi ..

Inawez kesho wakaja na idea mpya tena na ushahidi na ikakubalika..Kuhusu umri ni maamuzi kama huamini vitabu vya kale watu walikuwa wanaishi muda mrefu hiyo sio sayansi ...Kuhusu umri na masimulizi ya zamani hayatokani na sayansi kabisa ni mambo yalikuwepo ila sayansi inaendea kutoa evidences ..


Suala la umri naona upungue mpaka miaka 10 ,mtu unaishi miaka mpaka 50 ili ugundue nn?
 
Kwakifupi sana .. nenda Soma kitabu cha mwanzo.
Utaona ulimwengu uliumbwa .... Kisha ukawa upweke kiza na maji vikiijaza.

Mungu akasema na iwe mwanga (thus akaumba Juan na mwezi)

Akaona nuru ni njema , akatenga na akaiita nuru mchana na giza usiku.

Akaja akaumba mimea, samak, Wanyama na kila kilichopo. ....

Siku ya Sita akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu ...

SASA tafuta maandiko utaona siku moja mbinguni (kwa MUNGU ni sawa na myaka elfu ngapi kwetu Wana Adam.

### usisahau kuwa Dunia iliumbwa ikawa na Giza na upweke Kabla hata ya Hilo wiki la uumbaji wa vitu vingine viujazavy omkuu.
 
Back
Top Bottom