Kwanini umri wa dunia unatofautiana sana na wa binadamu wa kwanza

Ukitaka kuelewa ulichouliza usichanganye mambo,umeuliza "lini binadamu aliumbwa" Nani kakwambia aliumbwa??tukienda na nadharia hiyo tutasema ADAM aliumbwa karibu miaka 5000 iliyopita,je vipi kuhusu mafuvu ya kale yaliyopata kuwako miaka 500,000 nyuma??
Tutakosa jibu,tusimame na dhana moja uumbaji au Mageuzi,

Ila ukitaka jibu la JUMLA nitasema hao kina zinja walikuwapo kabla ya Adam ila hawakua binadamu, Adam ndio binadamu wa Kwanza na habari zake zimeanza kuandikwa katika Bible,aliishi Mashariki ya kati

Ila mafuvu ya watu wa kale(sio binadamu) yanapatikana kila mahala na wanasema kila yanayopatikana yakiwa mbali from Africa,yanakua na umri mdogo tofauti na yanayopatikana Africa,means maisha yalianza hapa,then wakahamia Australia na kwingine
 
Vp bustani ya edeni kwa sasa iko wapi
 
Sayansi haina facts wanakuaminisha wanachotaka kuamini ,sayansi inabadilika kulingana na muda ...
Sasa kama sayansi hakuna fact kulikua na haja gani kutumia teknolojia zao na ukiumwa unakwenda kutubiwa na wao.
Mfano hiyo simu unayotumia na mpaka JF umeipata ukiambiwa kitaalamu unaweza kubisha kwa kutumia vifaa vyao.
 
Inaonyesha kwenye tafiti za wanasayansi kuwa wanadamu walikuwepo kabla ya adamu hata walipotimuliwa kwenye maelezo inaonyesha walikuta watu wengine ambao mungu hakutaka wachangamane nao.

Kuna maelezo kwenye biblia unasema alimuumba kwa mfano wake.
Ila wengine walikuwa sio mfano wake ndio maana kuona watu wenye tabia za kenge,chura viziwi na wanyama wengine.
 
Sasa kama sayansi hakuna fact kulikua na haja gani kutumia teknolojia zao na ukiumwa unakwenda kutubiwa na wao.
Mfano hiyo simu unayotumia na mpaka JF umeipata ukiambiwa kitaalamu unaweza kubisha kwa kutumia vifaa vyao.
Umenielewa lakini? Sayansi ni endelevu inakuwa hai kutokana na muda husika ,hata simu hazikuanzia hapa ; kulikuwa na za batani na hazina mambo mengi ,kulikuwa na simu ambayo hauwezi kuweka mfukoni ila sasa wako mbali sana so hapa simu ya zamani hauwezi kutumia kwa ulimwengu wa sasa .

Unachoamini kwa sasa ukienda kununua simu : iwe touch ,kamera nzuri ,internet , muonekano labda nyembamba sana na makokoro mengine.
 
Sasa hao wengine waliumbwa na nani mkuu
 
Usikimbie kuruka mada.Shida yetu sisi wa afrika unajibu kuwa sayansi hakuna fact.
Wewe hiyo uliyo approve kuwa sio fact hiko wapi?.
Shida mnajua sayansi ni kama easy check.
Nikurudishe nyuma kama miaka ambayo watu wanatumia barua xa kawaida walivyoelezwa barua pepe walifikiri itawezekana.
Mbona imewezekana we sasa unafikiri miaka ya nyuma kulikuwa na Hard disk yenye ukubwa kilo 500 yenye uwezo wa MB 1 leo unatembea nayo mfukoni ikiwa na 1TB
 
Naona shule tatizo kuna facts na opinion basi kasome vizuri !

Sayansi unayoongelea hata theories zilikuwepo nyingi za kutokea kwa mabara ,zilitamba kwa muda husika na watu walizisoma ila baadaye zilibaki kama opinion tu basi .

Sayansi waliamini kifo hakiepukiki na watu wameishi hivyo karne kwa karne ila leo wamekuja na mpango wa kusema mtu anaweza kuepuka kifo ...Sayansi inabaki na fact kwa muda husika ila inaweza kuwa ni opinion tofauti na vitabu vya dini ,hazijawahi kubadili misimamo yake tangu awali
 
Sayansi ipo sahihi na biblia ipo sahihi. Hapo mwanzo Mungu aliumba dunia ikiwa nzuri tu. Hiyo ni mwanzo 1:1 na vitabu vingine utaenda kutafuta. Baadaye, dunia ikiwa nzuri, Shetani akatupwa chini, dunia ikaharibika maana popote alipo Shetani pana uharibifu. Ikapita miaka mingi sana (billions of years) , ndipo Mwanzo mstari wa 2 ikaendelea na Mumbai ukafanyika upya ikiwemo Mumbai wa mwandamu. Cha kushika ni kati ya mwanzo 1:1 na mwanzo 1:2 kuna bilions of years ambayo biblia haijasema ni miaka mingapi ila ni miaka ya kutosha. Tafuta expository study bible inayochambua mstari kwa mstari utaelewa vizuri.
 
Kati ya Shetani na Adam nani alikuwa wa kwanza kuishi humu duniani?

Na hatujui ilimchukua miaka mingapi kufikiria kumuumba mwanadamu.

Historian Wanasema shetani alipofukuzwa huko mbinguni, Mungu alimtupa duniani.

Hatujui Adam aliishi miaka mingapi kabla Mungu hajamuumba Hawa.

Shetani alimrubuni Hawa, na Hawa akamrubuni Adam.

Kisha wakatimuliwa wote, na wanaume ndio huwa tunakufa kabla ya wake zetu, hahaha.

Au ni fuvu la Abel aliye uwawa na Kaini.

Au ndilo fuvu la shetani wa kwanza.
 

Inafikirisha sana maana hata Adam mwenyewe haijulikani alizikwa wapi
 
Inafikirisha sana maana hata Adam mwenyewe haijulikani alizikwa wapi
Huyo Dr.Leakey na mkewe waongo tu, kwani binadamu wa kwanza hakuwa anaoza?

Yani Miaka yooote hiyo fuvu liwe linamsubiri yeye aje alivumbue?
 
Hakuna "binadamu wa kwanza", fanya jitihada ujielimishe zaidi.

Hakuna mahali hata huyo Dr. na mkewe wamewahi kusema wamegundua mabaki ya "binadamu wa kwanza".

The very idea eti kuna binadamu yeye ndio alikuwa wa kwanza is stupid! Kwamba yeye ali evolve peke yake mpaka kuwa binadamu?
 
Sio 1935 ni 1959. Rekebisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…