Kwanini usukani wa gari haukuwekwa katikati na badala huwekwa kushoto ama kulia?

Kwanini usukani wa gari haukuwekwa katikati na badala huwekwa kushoto ama kulia?

ankai

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2017
Posts
3,282
Reaction score
4,251
Ivi ni sababu zipi za kisayansi ama za kawaida zilizo na zinazosababisha mpaka leo uskani (sterling) ya gari isiwekwe pale katikati bali huwekwa pembeni kushoto ama kulia mwa gari

Wakati kwa kawaida mtu ukiangalia unaona labda ungekaa pale katikati ingekuwa ni rahisi zaidi kwa dereva kuendesha kwa usahihi zaidi na uenda labda ili lingeweza kupunguza ajali za magari barabarani

Kwa yeyote anayejua sababu za kisayansi zinazozuia uskani kukaa katikati karibu atujuze wengine tusio jua izo sababu
 
Usukani kukaa kulia au kushoto ni salama zaidi kuliko katikat. Kwanza inamsaidia dereva kuona MTU alinyuma yake, inamsaidia kuzuia ajali kwa kuwa dereva anajua umbali sahihi pindi kipishana na chombo kingine. Sasa ukikaa katikati lazm utafanya makadirio tu ha ha ha
 
Hili dereva aweze kuwa huru zaid bila kusumbuliwa au kugusana anapo piga kona zozote.

Usukani ukiwa kati, maan dereva atakuwa amewekwa katikati ya abiria, hapa anaweza asiwe flexible au comfortable sana, kinyume na hapo kuwe kuna gape kubwa kati ya siti ya dereva na abiria hao wawili kwa kila upande, na kufanya gari liwe pana zaidi

Niwazavyo.
 
Wakati kwa kawaida mtu ukiangalia unaona labda ungekaa pale katikati ingekuwa ni rahisi zaidi kwa dereva kuendesha kwa usahihi zaidi na uenda labda ili lingeweza kupunguza ajali za magari barabarani

Pale ulipo ndipo unamfanya dereva aendeshe kwa usahihi zaidi kuliko kama ungekuwa katikati kama bajaji, dereva kuwa kulia mwa gari kunamfanya aone inamoishia lane yake kwa usahihi zaidi na kutosababisha ajali kwa sisi tunaopita kushoto mwa barabara
 
Back
Top Bottom