Kwanini usukani wa gari haukuwekwa katikati na badala huwekwa kushoto ama kulia?

Kwanini usukani wa gari haukuwekwa katikati na badala huwekwa kushoto ama kulia?

Hili dereva aweze kuwa huru zaid bila kusumbuliwa au kugusana anapo piga kona zozote.

Usukani ukiwa kati, maan dereva atakuwa amewekwa katikati ya abiria, hapa anaweza asiwe flexible au comfortable sana, kinyume na hapo kuwe kuna gape kubwa kati ya siti ya dereva na abiria hao wawili kwa kila upande, na kufanya gari liwe pana zaidi

Niwazavyo.
Sio gari linabeba abiria mbele wakiwa siti moja na dereva
 
Kuna gari ya Muingereza ilitengenezwa kipindi cha nyuma ilikuwa inaitwa Vanguard ilikuwa na usukani(Sterling) upande wa kulia na kushoto kwa wakati mmoja.
 
Niliwaza utotoni, mawazo yakapotea kusikojulikana...
 
Ivi ni sababu zipi za kisayansi ama za kawaida zilizo na zinazosababisha mpaka leo uskani (sterling) ya gari isiwekwe pale katikati bali huwekwa pembeni kushoto ama kulia mwa gari

Wakati kwa kawaida mtu ukiangalia unaona labda ungekaa pale katikati ingekuwa ni rahisi zaidi kwa dereva kuendesha kwa usahihi zaidi na uenda labda ili lingeweza kupunguza ajali za magari barabarani

Kwa yeyote anayejua sababu za kisayansi zinazozuia uskani kukaa katikati karibu atujuze wengine tusio jua izo sababu
Ukikaa kati utawezaje kuovertake mzee baba
 
Kwanini bajaji, tractor, excavator na grade sterling zao zipo katikati??? Ukipata jibu utakuwa umejinjibu swali lako
Hii inaweza kuwa ni mojawapo kati ya sababu lakni vip kwa gar za LHD nazo unaziweka wapi kwa hii point yako ndugu ama zenyewe ni vice versa zinapata ajali sana mkuu??
 
Je unajua kwanini kitanda hakiwekwi katikati ya chumba?

Ukijua hilo hata la gari utakuwa umemaliza. Utakua umepata jibu.
Hakiwekwi katikati ya chumba uswahilini.. Watu wenye mijengo na room zwnye nafasi wanaweka kitanda katikati
 
Ina maana dreva wa trekta yeye waga haoni inapoishia lane yake kweli kiongozi na pia hii haiwezi kuwa sababu ya kisayansi

Ukitazama tractor ni jembamba zaidi katika eneo la uendesheaji, hata abiria wake hukalia vizuizi vya matope huku eneo la kupandia likiwa wazi na lina uwazi mkubwa kati ya gurudumu ya mbele na nyuma kiasi kwamba alama za lane zinaonekana kwa urahisi kuliko gari ambalo huwa limefungwa na driver huona nje kupitia vioo/madirisha, tazama hata greda la kusembulia barabara lina umbile la kufanana na tractor kama lina vioo utaona vimeshuka mpaka chini zaidi ya vile vya magari
 
Kati kati kuna raha nyingi ina jiwe's voice

Hapo watengenezaji wa majeneza wangetajirika
 
Ivi ni sababu zipi za kisayansi ama za kawaida zilizo na zinazosababisha mpaka leo uskani (sterling) ya gari isiwekwe pale katikati bali huwekwa pembeni kushoto ama kulia mwa gari

Wakati kwa kawaida mtu ukiangalia unaona labda ungekaa pale katikati ingekuwa ni rahisi zaidi kwa dereva kuendesha kwa usahihi zaidi na uenda labda ili lingeweza kupunguza ajali za magari barabarani

Kwa yeyote anayejua sababu za kisayansi zinazozuia uskani kukaa katikati karibu atujuze wengine tusio jua izo sababu
Sababu ni MOJA tuu......kioatikane nafasi ya mtu mwingine kukaa vizuri mbele.....ki swahili tunaita proper utilizationi ofu lisosezi!
 
Back
Top Bottom