Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mimi Kwa majina naitwa G.

Nilifanya interview ya utumishi nakuingia oral mwezi wa nane.

niseme neno Moja.

Kuanzia leo tar moja sitajishughulisha tena na masuala ya kutafuta mkeka.


NIMEACHA NIMECHOKA.

AMEN

Placement zinaweza chukua 3 months. Mimi pia tumefanya mwezi wa nane, hadi leo bado hatujaitwa. Ni uvumilivu, roho ngumuu, na Kumuomba Mungu roho ya subira.

In TID’s voice “Stamina, Pumzi”
 
Mimi Kwa majina naitwa G.

Nilifanya interview ya utumishi nakuingia oral mwezi wa nane.

niseme neno Moja.

Kuanzia leo tar moja sitajishughulisha tena na masuala ya kutafuta mkeka.


NIMEACHA NIMECHOKA.

AMEN
Yani navokuona humu kutwa na malalamiko yako basi me nadhania oral ulipiga ata mwezi wa 3 huko kumbe ni mwezi 8 tu Mkuu...!

Kuna raia zilipiga oral tangu mwezi wa 2 na hadi hivi sasa zinaskilizia placement kimya kimya

Sasa wewe miezi 2 tu ushaongea maneno yote umemaliza seriously? Na ata wakianza kutoa placement na ukachelewa kupata bado utaendelea kulaumu tu

Mfano, Mimi nilipiga oral mwezi wa 2, ulipofika mwezi wa 3 placement zikaanza kutoka, kila mwezi majina yanatoka, washkaji wanapata me holaaa, katika kundi langu la washkaji 8 nilibakia mwenyewe tu

Nikaendelea kufanya mambo yangu Tu, kwa sababu najua interviews ni mashindano na ni vigumu kushinda wote, sasa unapodhania wewe ndio una haki ya kupata kuliko wengine hilo linakuwa tatizo la Akili sasa

Nilipotezea issue za placement hadi nilipopigiwa simu mwezi wa 10 napewa hongera, na katika hao washkaji 8 hakuna ata mmoja aliepata kazi kwa connection

We fanya interview kisha endelea kuishi maisha yako uliyokuwa unaishi kabla hujafanya, amini kuwa kila Mtanzania ana haki ya kupata kazi ya utumishi ila sio lazima awe wewe
 
mbona unatutisha.yaani mwezi wa 2 mpaka wa kumi mmmhhh twafa.....🤣🤣
 
Hongera sana mkuu, ni uvumilivu mkubwa sana, finally you made it, ukawe mtumishi mwema, utuwakilishe vijana
 
Maisha unayoishi wewe usitake wengine tuyazoee .

Kiukweli psrs wamekwama na inabidi wajitathimini vya kutosha.

Yaani ufanye interview mwezi wa 2 ajira uoate wa 8 na ukute sio database halfu use me kawaida.

Kiukweli inabidi wajitafakari vya kutosha na wajitathmini sana .

Mimi silalamiki na nimejiandaa kwa lolote lile
 
Sema mwana na ww unanichanganya 😁 mara Psrs hawana makosa, mara Psrs wanazingua!

Sema humu watu wanatumia Id fake, kuna baadhi ya shuhuda humu zinatia mashaka na kujiuliza maswali kama ni kweli au kunakitu anatetea.
 
kwakweli ni uchoko..
 
Mkuu wewe unalalamika na hujajiandaa kwa lolote lile ndomana kila baada ya dakka kadhaa lazima upost comment humu, waliojiandaa na lolote wanasubiri kupigiwa Kama itatokea

Na kingine issue sio maisha nayoishi Mimi bali ni kukubaliana tu na mazingira, we ata ukeshe humu unawasagia kunguni utumishi haibadirishi chochote na wala haikupi faraja yoyote

Na issue sio Tu kutoa placement issue ni wewe kupata katika hizo placement, kama unalalamika placement hazitoki utakuja kulalamika tena kuwa umekosa kazi kisa upendeleo na kusahau kwamba mlikuwa kadhaa mnagombania nafasi kadhaa

Ushaanza Mambo za ohhh utumishi waache kusimamia zoezi la Ajira, yani miezi miwili Tu? Kuna mwenzio tulikuwa nae humu tangu January alikuwa na campaign ya kupinga utumishi kusimamia mchakato wa Ajira kwa sababu hawako Fair

Matokeo yake alipata kazi, na akapote jumla humu ata salamu Tu hataki kutoa, ila ilikuwa anashinda humu kama ulivo wewe, kwahiyo ubaya au uzuri wa utumishi inategemea unwaangalia kwenye Angle ipi, utakuja Tu kuwasifia siku Moja
 
Bora taasisi ziajiri zenyewe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…