Yani navokuona humu kutwa na malalamiko yako basi me nadhania oral ulipiga ata mwezi wa 3 huko kumbe ni mwezi 8 tu Mkuu...!
Kuna raia zilipiga oral tangu mwezi wa 2 na hadi hivi sasa zinaskilizia placement kimya kimya
Sasa wewe miezi 2 tu ushaongea maneno yote umemaliza seriously? Na ata wakianza kutoa placement na ukachelewa kupata bado utaendelea kulaumu tu
Mfano, Mimi nilipiga oral mwezi wa 2, ulipofika mwezi wa 3 placement zikaanza kutoka, kila mwezi majina yanatoka, washkaji wanapata me holaaa, katika kundi langu la washkaji 8 nilibakia mwenyewe tu
Nikaendelea kufanya mambo yangu Tu, kwa sababu najua interviews ni mashindano na ni vigumu kushinda wote, sasa unapodhania wewe ndio una haki ya kupata kuliko wengine hilo linakuwa tatizo la Akili sasa
Nilipotezea issue za placement hadi nilipopigiwa simu mwezi wa 10 napewa hongera, na katika hao washkaji 8 hakuna ata mmoja aliepata kazi kwa connection
We fanya interview kisha endelea kuishi maisha yako uliyokuwa unaishi kabla hujafanya, amini kuwa kila Mtanzania ana haki ya kupata kazi ya utumishi ila sio lazima awe wewe