Wakati sisi tunaajiriwa halmashauri 2014, jamaa yangu mmoja tulisoma nae Pugu A level kisha tukawa wote UDSM ila kozi tofauti. Sasa wote tulipata halmashauri ila yeye hakwenda kumbe kuna contract ya Jhpiego. Sisi tukajiona tumepata maisha tumeingia serikalini. Baada ya miaka 3 ya contract yake kajenga nyumba, kanunua na gari ingawa alimvua mtu. Mkataba ulipoisha kakaa mtaani mwaka na miezi kadhaa kadhaa kadaka mkataba shirika jingine. Sasa hivi nyumba ya pili imebaki vioo/aluminium tu kukamilika na gari ile kabadilisha kachukua Rav4 new model mwaka juzi kamaliza Masters ya Project Management. CV inazidi kupanda. Tulioingia halmshauri nyumba zetu zimeishia njiani either kwenye lenta au imepauliwa ila imebaki pango la popo tena tumefika hapo baada ya kukopa sana na kutop up.