Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Mkuu nasisitiza, shukuru umepata hiyo kazi, unavoendelea kushuhudia hapa unaanza kuwavua nguo utumishi.
Maswali mawili hukujibu, na hata uliyojibu hukumbuki ulijibu nini na bado ukachomoka kwa database "best loser".
Ndio ujue kuwa kufauru oral kuna vitu vingi, nimeorodhesha hapo . Na hawataki ujifanye much know... Hata wao wana vitu vyao wanaangalia haiwezekani mtu apate written 80, practical 80+ ...thn oral ashindwe basi wam cancel ...so kuna vitu vingi wanaangalia zaidi ya unachokijibu....maana wakitaka uende jino kwa jino....wataanza kuicheck hata hiyo english yako 🤣 na grammar zake ..
 
Wakuu Utumishi Connection hakuna wewe make sure unafanya vizuri...thn tulia unaweza ukaa hata database ikapita mwaka , kidogo vuuup Kwenye dimbwi la asali
Jitahidi kutumia muda mwingi KUMSHUKURU Mungu kwa kukupa hiyo kazi.

Kuliko kutumia muda mwingi kuitetea utumishi.

Mimi namfaham mtu niliyefanya kazi nae na kila Siku alikuwa anatuambia ajira za utumishi zikija lazima apate kazi.

Mimi nakadhani anatania lakini tulienda dodoma kufanya nae interview tukapiga oral na written majina ya kazi kutoka jina lake la kwanza.

Kiukweli jamaa alikuja kunuchana alitengenezewa mazingira name hadj maswali ya oral na written alikuwa nayo.

Utumishi connection ipo ila kwa asilimia hazifiki kumi.
 
Ila kupata wewe kazi.

Kusikufanya ukawa mjinga kuwasifia utumishi na kuwasahau kuna kundi kubwa la watu linahitajika kutiwa moyo na kupewa faraja.

Unajiita chawa wa mama inakusaidia nini?
 
Ndio ujue kuwa kufauru oral kuna vitu vingi, nimeorodhesha hapo . Na hawataki ujifanye much know... Hata wao wana vitu vyao wanaangalia haiwezekani mtu apate written 80, practical 80+ ...thn oral ashindwe basi wam cancel ...so kuna vitu vingi wanaangalia zaidi ya unachokijibu....maana wakitaka uende jino kwa jino....wataanza kuicheck hata hiyo english yako 🤣 na grammar zake ..
Kwa ulichokiandika hapa, hupaswi kuwa na imani hiyo ya kuwa utumishi wako fair na wala usiamninishe tena watu kuwa wako fair.
 
Ndio ujue kuwa kufauru oral kuna vitu vingi, nimeorodhesha hapo . Na hawataki ujifanye much know... Hata wao wana vitu vyao wanaangalia haiwezekani mtu apate written 80, practical 80+ ...thn oral ashindwe basi wam cancel ...so kuna vitu vingi wanaangalia zaidi ya unachokijibu....maana wakitaka uende jino kwa jino....wataanza kuicheck hata hiyo english yako [emoji1787] na grammar zake ..
Mzee tulia ukale ulale unaongea pumba sana na umekuwa kama mwehu fulani
 
Sasa unamkuta mtu mwengine anaulizwa swali anaona hapa hajui thn anaakaa kimya ..wakimwambia twende swali jengine...anasema ooh Noo... wait .thn aanaanza kuunga point anaitafuutaaa anapata moja anakaa kimya , huku anafikiria wanamwangalia tu ...wanasema tena twende anakataa..mpka wenyewe wanauliza swali linalofuata . Sasa anakuwa kama anawaletea ubishi flani hivi. Wakati kuna kijiji nje na wao wanatakiwa wasailiwe.

Mimi niliingia oral moja na hiyo ndio niliyotoboa , niliingia youtube nikaangalia jinsi gani unatakiwa ujibu alooo kwanza sauti inatakiwa itoke ,🤣 usmile , uwaangalie usoni, usijipigilee sana mpka mtu akikuona ajue aaahh huyu mbona kama hana shida kivile... Usikae bila kuambiwa ,usinyanyuke bila kuambiwa.. tia huruma. Fata maelekezo.
Kutia huruma tena mkuu?? Unafanyaje kutia huruma?
 
Mkuu umeongea sahihi kwa asilimia 100% ,ila swala la kupiga chabo hapo au kuingia na supportive material utumishi wakikudaka wanafungia na account yako huwezi omba kazi serikalini tena...

Kuna jamaa wao walitumia mbinu ya kufanyiana bahati mbaya wakadakwa .walifungwa miaka 3 na kuzuiwa kuomba kazi utumishi tena .na tangazo lilitoka. Cheating is prohibited.

Ila vyengine vyote umeongea ni sawa .
Shukrani kwa feedback mkuu, ila sidhani kama kuna sehemu nimeongea uingie na materials ndani ya chumba cha mtihani

Ukiigilizia hakuna ushahidi wowote ule ambao utumishi watautumia kukupa adhabu yoyote ile, Sana sana watakubadirishia eneo la kukaa
 
Wakuu I mean a battle between innojembe na ITpersonal hawa watu niliinjoi bifu Lao.

Ila ndo hivyo It katuacha sisi jobless.

Natangaza Rasmi bifu na bwana anajiita Utumishi wako fair.

Ili bifu litadumu hadi mimi nitakapopata placement
🤣🤣 Boss nakuahidi kazi utapata, hakuna connection wewe omba Mungu kapige interview yani huwezi piga interview 3 mfululizo ukakosa lazima upate... Mimi nina shuhuda rafiki zangu asilimia kubwa wamekula vitengo ,tena wao ndio walikuwa wakwanza kuingia utumishi wakawa wananiambia RAJABU kaza unatoboa...Na kweli....So hata wewe mkuu kaza unatoboa wallah.

Mimi kuanzia january Nitakuwa sichart humu sababu nitabanwa na majukumu ya kazi yangu mpya,.

Nitakuwa nafanya kazi kama punda, nitalala offcn mara moja moja🤣🤣
Pia nitakuwa nakuja kuwatia moyo vijana wenzangu, cz i know ujobless sio kitu kizuri kabisa ,yani bora jobless awe mtoto wa kike ila sio mshkaji cz unakuwa ile thamani yako haipo yani hata simu za washkaji huoni....

Mimi dua zangu, Mama samia suruhu aendelee kubakia madarakini naamini vijana wengi watatoka kwenye hili dimbwi... Wewe kaangalie trend ya ajira alizotoa since amekuwa madarakani.. yani Mheshimiwa alimwaga ajira mpka watu wakaanza dharau za kuchagua kazi ,yani mtu anapangiwa Halmashauri anasema siendi, nasuburia nyengine ndio uone uhakika wa kazi ulivyo mkubwa, cz haiwezekani leo uletewe ugali useme huu sitaki nataka wali kama huna uhakika wa wali.

So naomba matangazo ya kazi yawe mengi kuanzia january, ili watu waombe...

Pia all in all nawaombea wote humu ,mpate kazi before mwaka 2024 kuisha... Amiiin .
 
Unakuta raia ananyuka Suti ,yani ile yenyewe kabisa. Sio suit kachumbari zile za karume pale...Yani Suit yenyewe kabisa.. ananukia unyunyu saa moja kaliiiii 🤣. Bro pendeza ila usipendeze sana mpka waone mambo safi ....
😂Ila hii nchi yetu bado ngumu sana aisee kwahyo mtu usipendeze kisa?? Kwenye mavazi labda usivae kihuni ila kama umevaa vizuri na unajua unachofanya kwenye interview i think its okay!
 
😂Ila hii nchi yetu bado ngumu sana aisee kwahyo mtu usipendeze kisa?? Kwenye mavazi labda usivae kihuni ila kama umevaa vizuri na unajua unachofanya kwenye interview i think its okay!
Hiyo nimeweka chumvi tu Mkuu, ila katika kupitia pita Maandiko ya Joel Nanauka..... Kuna siku niliona Article hiyo.' akatolea mfano; wakija watu wawili hapo wakakuomba mfano kitu fulani, Basi kuna mmoja utampa either kingi au kidogo ya mwenzake with no reason' ...
 
Boss wangu ,kuna kuandika kiswahili kweli?? thn wala hazinipi shida ila siwezi kuwa carefully to that extent kwenye sehemu ambayo haihitaji hicho kitu... Yani nianze kucheck spelling error humu, wakati naandika sifaidiki chochote just for fun..tu.

Hebu angalia maandiko yangu ya nyuma kipindi nipo jobless kama niliwahi changanya spelling ...Boss kuna ka hali fulani ukiwa una uhakika unakuwa dont care
- unataka tujue maandiko yako nyuma tutajie ID yako ya zamani
 
Mkuu nasisitiza, shukuru umepata hiyo kazi, unavoendelea kushuhudia hapa unaanza kuwavua nguo utumishi.
Maswali mawili hukujibu, na hata uliyojibu hukumbuki ulijibu nini na bado ukachomoka kwa database "best loser".
Mkuu usiwe serious kiivyo wacha watu waonyeshee Furaha zao.
 
Wakuu Naendelea Vizuri ,Sijawatupa wadau... Nikipata nafasi ya kutulia nitajibu pongezi ya Mtu mmoja mmoja, na kutoa ushauri...

Ila nilifanikiwa kuchukua barua utumishi na nilipeleka kituo cha kazi, Napenda nimshukuru Mungu sana, Pamoja na utumishi wa umma kwa kutoa kazi pila Upendeleo hata kidogo, yani wanafanya haki 100% ...

Nitatoa briefly njia niliyotumia mpka nikafanikiwa kupata kazi, Serikalini...Pia baada ya kufika huku nimeshuhudia zile process wanazojadiri wadau humu almost ndio zile ..zile, yani ukifika automatically unaona process zina flow. Pia kuhusu mshahara wa Taasisi na tamisemi kutofautiana ni kweli. Diploma wa taasisi anamwacha mbali mtu wa Tamisemi au wizara tena HQ. Yani Wewe ukiwa na bachelor ya Account na mwenzako. Wewe upo wizara yeye taasisi anakupiga bonge la Gap.

So wadau nitashare experience ,since nimeona jina mpka kufika kituo cha kazi.[emoji120]
Na jina umebadilisha utumishi [emoji3]
 
Mkuu hakuna ukweli wowote na hizo Mambo z kuaga au kutokuaga, ila kwa Akili ya kawaida tu unaaga watu ili iweje ilhali unaenda kubeti?

Aga kama kitu una UHAKIKA nacho, ila unaaga alafu baada ya muda watu wanaendelea kukuona tena uraiani ni wazi utaonekana ulifeli interview, sasa Kwanini uwape watu vitu vya kusema

We Sepa kimya kimya na lengo ni kukaa kwa Amani kitaa pindi utakaporudi kuskilizia ili ata ukizingua watu hawajui kama ulienda interview

Huwa inakera watu wanapojua ulienda interview na bado unaonekana kitaa Tu ata kama utumishi watachelewa kukupangia kituo wao hawajui hayo, wao wanajua ulifeli Tu na kuonekana Mzigo kitaa

Turudi kwenye point ya msingi nini ufanye utoboe, Kwanza inaonekana Kada yenu inatoa Ajira chache ndomana hadi Written wanaanza kuchukua 75, it means nawewe inabidi uset standard ya kuanza kupata kuanzia at least 75

Written ya Kwanza hukufika 50, ila ya pili ukafika 65, that means ya pili uliongeza juhudi katika kujiandaa, ndo kitu unachotakiwa kukifanya kwenye interview inayofata, kwenye Written jitajihidi uwe miongoni mwa best performer kisha kwenye Oral acha Lucky ichukue mkondo wake

Na kingine cha muhimu kabisa, mitihani ya Utumishi sio necta, jitajihidi kwa mbinu yoyote ile uhakikishe unapata mark's za kutosha, unapoingia kwenye pepa chagua watu ambao unajua wako vizuri, na hasa wale fresh from school vichwa waga bado viko fresh, au jamaa zako ambao unajua walikuwa visomo sana ndio ukae nao

Na ukiona swali halitembei Kwa uwezo wako fanya juu chini usaidiwe, muache utoto wa shule kwamba utaonekanaje ukiomba majibu, hapo upo unatafuta future ambayo inaweza ikaamliwa na Makaratasi Tu, kwahiyo jibu swali ambalo Una uhakika nalo Tu na kama sio sumbua watu wakupe majibu

Ukipita Oral hapo waga ni 50/50 haijarishi ulifanya vizuri au ulifanya vibaya, Siri ya oral wanaijua hao hao utumishi, tupo watu ambao tulitoka kwenye oral tumefanya hovyo ila tukapata kazi, ila kazi inaanzia kwenye Written not otherwise
Asante kwa ufafanuzi mkuu, japo pia wakati mwingine unakuta mshapanga formula nje namna ya kukaa mkiingia mle ndani jamaa wanapangua hapo ndio panaanza kuwa pagumu na unakuta zile dk 40 zao hazitoshi, ila yote kwa yote la muhimu hapo ni kujiandaa vizuri tuu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom