Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hivi hii kozi yangu ya BACHELOR OF SCIENCE IN PHYSICS haina hata matangazo ya ajira za kutengeneza mitego ya panya. Mbona nimepigwa na kitu kizito vibaya sana wajemeni.
Tatizo Bongo hamna scientific research and development institutions
So watu kama wewe kazi zenu ni za maabara na kudevelop scientific ideas na kufanya research mbalimbali na vumbuzi au kufanya kazi za maabara
Ninyi ni kama wale wenye bachelor's of science in Chemistry au Biology
Ingawa watu wengi wamezoea kuwaita walimu ila si sawa ,ninyi ni experts katika hiyo field .
Ingawa hata kufundisha inawezekana ingawa sio specialty yenu .
Wa Chemistry na Biology naona ndio wanapata pata kwenye institutions kama NIMR , TARI ,TAFIRI nk ila kwa Physics sijui wakuajili wapi aisee .
Kuna dogo mmoja rafiki yangu alisomea hiyo course DUCE na akaajiriwa mwaka jana kule IRINGA kama mwalimu ,ila ile ilikuwa ni special case kwa zile nafasi za kipekee za watu wasio na fani ya ualimu kuomba kazi za ualimu kupitia Tamisemi ,nadhani zile nafasi ilikuwa ni mwaka 2021 au 2022 ndio zilitolewa
 
mmmhh lkn sasa mbona ww huach kaz au unatudanganya majobless??
Kama ni jobless kafanye hata hizo za Halmashauri,au kama kazi unayofanya kwa sasa ina kipato kidogo sana au kama mishe zako ni za kuunga unga sana kafanye kazi hata Halmashauri,hela ipo. Pia neno langu sio sheria,so kila mtu ana nafasi ya kuchagua kipi ni sahihi kwa muda na muktadha upi vile vile malengo yake ni yapi.
 
kwan ni halmashauri zote au inategemea na halmashauri??
Halmashauri zote mambo ni yaleyale tu,ingawa zipo baadhi ambazo wanasaini saini vijiposho posho. Inategemea pia position yako ni ipi,na hiyo halmashauri yenu ina mapato kiasi gani. Ila hizi ambazo zinategemea OC ya serikali kujiendesha ni changamoto sana.
 
Usemacho ni kweli kabisa mkuu, na hasa kama unafanya kazi za Desk, kitendo cha kuingia job asubui na kutoka jioni alafu mwisho wa mwezi usubiri laki 8 ni kasheshe kama mtaani ulikuwa unaingiza zaidi ya hiyo au inayoendana na Salary

ila kwa ambao wanafanya kazi za field ni unyama sana Mkuu, km utafika ofisini asubui ukasaini unasepa zako ndo imetoka hiyo, hadi kesho tena au siku ingine utakayoamua kwenda ofisini

So unaweza kukaa ata siku 3 hujakanyaga ofisini, ila kama una viongozi wakuda we ni kuingia na kusaini kisha safari, hapo ata km unalipwa laki 5 we fresh tu kwa sababu unautumia muda wako vizuri sana kiasi kwamba unaweza ukawa unafanya kazi Singida ila unafata biashara mwanza kila week

Na una fursa ya kukopa na kuongeza kwenye mtaji wako ili kuongeza mzunguko, kwahiyo kazi za Halmashauri inategemea na nature ya kazi yako, kuna raia waga hazionekani job ata mwezi mzima kwa sababu yeye ni mtu wa field
Uko sahihi kabisa Mkuu,ila kwa huku ambako nipo fursa pekee labda uwe Mganga wa Kienyeji.
 
Aise nimefatilia maongezi ya watu wengi humu asa wadau wenzangu wa Halmashauri, lakin chakushauri tu washikaji tusikate tamaa, mungu yupo na bado anapambania ndoto zako.
Nina ndugu yangu mmoja alianzia kazi Halmashauri tena kigoma vijijini ila kakomaa kipindi kirefu kidogo saivi yupo TRA, na mfano mwingine kuna watumishi wamehamia kutoka halmashauri kuja uku nilipo na wanalalamika kweli walipotoka hali sio nzuri lakini walipambana pasipo kutoa chochote na wameshatoka uko.
Ushauri wangu ni kwamba tusichoke kupambana hapo ulipo ni mungu kapanga uanzie apo kwaiyo omba mungu pia akupeleke unapopatamani na ukiwa bado unapambana.
Sawa Mkuu,ila changamoto unakuta unasota miaka 8 katika hiyo halmashauri.
 
Sawa Mkuu,ila changamoto unakuta unasota miaka 8 katika hiyo halmashauri.
Kama ushamaliza probation anza kufight kwa kuomba kazi ajira portal upya ila utakuwa unaambatanisha barua zako kwa mwajiri. Kidogo kidogo unachomoka kimtindo
 
Mkuu,baadhi tulibahatika kulamba hiyo vijana tunaita asali,ila mazingira tuliyolamba hiyo asali imegeuka shubiri. Kuna Baadhi ya Wilaya katika hii nchi ukipangwa kwenda kufanya kazi unatamani bora ungebaki kwenu Chalinze ulime nanasi.
🤣🤣🤣🤣 Mwenetu wapi Buhigwe nini.

Ofisini unakutana na kiti cha mbao mguu mmoja mfupi.

Ofisini hapo nje zimepaki baiskeli na pikipiki za Watumishi.
 
Back
Top Bottom