Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hivi hii kozi yangu ya BACHELOR OF SCIENCE IN PHYSICS haina hata matangazo ya ajira za kutengeneza mitego ya panya. Mbona nimepigwa na kitu kizito vibaya sana wajemeni.
Tatizo Bongo hamna scientific research and development institutions
So watu kama wewe kazi zenu ni za maabara na kudevelop scientific ideas na kufanya research mbalimbali na vumbuzi au kufanya kazi za maabara
Ninyi ni kama wale wenye bachelor's of science in Chemistry au Biology
Ingawa watu wengi wamezoea kuwaita walimu ila si sawa ,ninyi ni experts katika hiyo field .
Ingawa hata kufundisha inawezekana ingawa sio specialty yenu .
Wa Chemistry na Biology naona ndio wanapata pata kwenye institutions kama NIMR , TARI ,TAFIRI nk ila kwa Physics sijui wakuajili wapi aisee .
Kuna dogo mmoja rafiki yangu alisomea hiyo course DUCE na akaajiriwa mwaka jana kule IRINGA kama mwalimu ,ila ile ilikuwa ni special case kwa zile nafasi za kipekee za watu wasio na fani ya ualimu kuomba kazi za ualimu kupitia Tamisemi ,nadhani zile nafasi ilikuwa ni mwaka 2021 au 2022 ndio zilitolewa
 
mmmhh lkn sasa mbona ww huach kaz au unatudanganya majobless??
Kama ni jobless kafanye hata hizo za Halmashauri,au kama kazi unayofanya kwa sasa ina kipato kidogo sana au kama mishe zako ni za kuunga unga sana kafanye kazi hata Halmashauri,hela ipo. Pia neno langu sio sheria,so kila mtu ana nafasi ya kuchagua kipi ni sahihi kwa muda na muktadha upi vile vile malengo yake ni yapi.
 
kwan ni halmashauri zote au inategemea na halmashauri??
Halmashauri zote mambo ni yaleyale tu,ingawa zipo baadhi ambazo wanasaini saini vijiposho posho. Inategemea pia position yako ni ipi,na hiyo halmashauri yenu ina mapato kiasi gani. Ila hizi ambazo zinategemea OC ya serikali kujiendesha ni changamoto sana.
 
Uko sahihi kabisa Mkuu,ila kwa huku ambako nipo fursa pekee labda uwe Mganga wa Kienyeji.
 
Sawa Mkuu,ila changamoto unakuta unasota miaka 8 katika hiyo halmashauri.
 
Sawa Mkuu,ila changamoto unakuta unasota miaka 8 katika hiyo halmashauri.
Kama ushamaliza probation anza kufight kwa kuomba kazi ajira portal upya ila utakuwa unaambatanisha barua zako kwa mwajiri. Kidogo kidogo unachomoka kimtindo
 
Mkuu,baadhi tulibahatika kulamba hiyo vijana tunaita asali,ila mazingira tuliyolamba hiyo asali imegeuka shubiri. Kuna Baadhi ya Wilaya katika hii nchi ukipangwa kwenda kufanya kazi unatamani bora ungebaki kwenu Chalinze ulime nanasi.
🤣🤣🤣🤣 Mwenetu wapi Buhigwe nini.

Ofisini unakutana na kiti cha mbao mguu mmoja mfupi.

Ofisini hapo nje zimepaki baiskeli na pikipiki za Watumishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…