Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Naona yangu ya heslb ba naot ziko vile vile tu?

Ahsante sana mkuu.

Wazoefu msituangushe kwenye hii kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi
Oral interview tips:
1. Omba Mungu

2. Confidence, ukijibu swali jitahidi kujibu kwa utulivu na chukua muda kidogo kutafakari swali linataka nini kabla ya kujibu kwa pupa na kisha kuishia njiani na kutokujua jinsi ya kuendelea na kuonekana hujui kitu kumbe unajua!

3. Kujiandaa, hakiksha unasoma taarifa muhimu za taasisi unayoenda kufanyiwa usaili
unapojibu maswali hakikisha unaunganisha matarajio na maono ya taasisi na majibu yake

4. Usaili wa oral huwa mara nyingi huwa na maswali matano
swali la kwanza huwa ni tell us about yourself, mengine yataendana na kada/fani yako mengi huangalia general knowldege uliyo nayo.
swali hili la kwanza kila kada lazima uulizwe

ushauri: jibu kuanzia elimu yako, na nenda kwenye uzoefu wa kazi huku ukiainisha zile job descrption (jd) na uzoefu wako. Yaani onyesha uzoefu wako unavoendana na kazi unazotarajiwa kuzifanya
kisha elezea kitu/vitu vya ziada vinavokupa faida zaidi kwenye hio kazi.

5. Vaa vizuri, nguo zinazoendana kiofisi.

6. Wahi sehemu ya usaili nusu saa kabla

7. Beba nyaraka zako zote zinazohitajika.

8. Sema asante baada ya usaili kwa wasaili.

9. Unapofika sehemu ya usaili utakuta watu wengi, wasalimie unaowafahamu na usiowafahamu. Mtu akikuuliza kitu na unakijua usiwe mchoyo mueleweshe, mpe moyo. What goes around comes around. Mtakutana sehemu nyingine anaeza kuwa msaada kwako.

10. Ukimaliza usaili basi Omba Mungu tena na zaidi zaidi.
 
Wakuu naomba kukazia hapo kwenye kusalimia kila mtu aseeh salimia kila mtu pale atakaekuwa karibu nawewe lakini usiogope hasa hizi oral zinazofanyika kwenye taasisi interview ya juzi nilifika pale kwenye taasisi mapema sana tukawa tumekaa na jamaa nayeye anaendakufanya oral sasa akaja mama mmoja akatuuliza vipi mbona mmekaa hapa tukamuelezea tu kilichokuleta tukasalimia nae akatuelekeza pakukaa lakini alikuwa kavaa tu kawaida yani ukimcheki unaona aah huyu hana kitengo chochote labda sasa tumeanza oral yeye ndo akawa anaekuja kutuchukua kutupeleka kwenye panel yetu ya interview ,nikajisemea huyu mama tusingemsalimia sijui ingekuaje leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…