Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hongereni wote mnaoendelea kuingia kundini.

Naendelea kusisitiza, HAKIKISHA UNAAPPLY HATA KAMA NAFASI NI 1, HAKIKISHA UNAFANYA USAHILI HATA KAMA NAFASI NI 1 NA HAKIKISHA UNAPAMBANA HADI ORAL.

Tangu niaapply nafasi zinazotagazwa na PSRS mwaka 2022 hadi sasa, nimekuwa nikifuatilia Job advertisements, Call for Interview(hii sio sana) na Placements.

Nimeona nafasi zinatangazwa zikiwa zinataka watu 2, lakini wakati wa placements wanachukuliwa ama hao 2 au zaidi, au wanakuja kuchukua tena kutoka database watu kadhaa zaidi wa nafasi hiyo hiyo. Kwa hiyo wale waliofika oral na kukaa bench wanaingia kundini kiulaini.

Kuna watu wangu wa karibu huwa kila mara nawashauri wafanye hizo sahili ila wanapuzia lakini wengine wanazozipambania tayari wanapata nafasi kiulaini.

Hatupangiani juu ya kufanya maamuzi ila ushauri hatuachi kutoa. Maamuzi atabaki nayo Mshauriwa.
 
Hili wengi hawazingatii sana, nna watu kadhaa wa karibu kwa strategy km hii wamebahatika kulamba asali
 
Hili wengi hawazingatii sana, nna watu kadhaa wa karibu kwa strategy km hii wamebahatika kulamba asali
Mimi nimefikia hatua ya kukaushia mtu.

Nimekuwa natanguliza neno KAMA UNA INTEREST ili akipenda afanye asipopenda aache.

Ile nafasi ya Registration Officer ya NECTA iliwahi kutangazwa mwaka jana ilihitaji watu 2. Lakini hadi sasa wanachukua watu kutoka database, ambao hawakuzembea imekuwa bahati yao
 
ila mfifwa mungu akupe maisha marefu aisee endelea na moyo huohuo wa kutukumbuka majobless..
 
Muhim sana hili la interest, kuna dogo pia aliona zile post za ASA Walika agricultural engineer kwenye tangazo nakumbuka hazikuzidi watu 20 akawa anapuuzia kuomba ila walipokuja kuchukua walizoa balaa watu wa civil walikuchukua km 100, wa maji walichukua km 60 na wa agriculture engineer nao walikua wa kutosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…