Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Walimu mna kimuyemuye. Subirini saa 3 usiku wanabandika pdf lenu la kuitwa machinjoni. PSRS ni ubaya ubwela
 
Katibu wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma Bw.Mick Lutechura Kiliba amewashukuru watumishi wa ofisi hiyo kwa kumkaribisha kwa mapokezi mazuri.

Bw.Kiliba ametoa shukrani hizo alipokutana na watumishi hao kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza ofisi hiyo.

"Nawashukuru sana kwa mapokezi makubwa tangu niliporipoti na kupokelewa na Menejimenti na leo hii ninyi watumishi mmenipokea vizuri sana" alisema.

Katika hatua nyingine Katibu wa Sekretarieti ya Ajira amepokea mrejesho kutoka kwa watumishi kuhusu utekelezaji wa zoezi la usaili kwa kada za afya na kuwapongeza watumishi hao kwa kusimamia zoezi hilo kwa weledi.

"Nawapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri ya kusimamia zoezi la usaili kwa kada za afya ambalo limefanyika vizuri nchi nzima".

Aidha, Bw.Kiliba amewataka watumishi hao kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza Katika zoezi hilo ili kuboresha zaidi uendeshaji wa mchakato wa ajira.

"Kuna zoezi kubwa la usaili kwa kada za ualimu linakuja hivyo tunapaswa kutatua changamoto zilizojitokeza katika usaili uliotangulia ili kufanya vizuri zaidi" alisema.

Bw.Kiliba amewataka watumishi wa Sekretarieti ya Ajira kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

"Ajira ni eneo nyeti sana na vyuo vinazalisha wahitimu wengi ambao wanatarajia kupata ajira serikalini hivyo tujitahidi kutekeleza majukumu yetu kwa weledi wa hali ya juu na niwaombe tuizingatie ile misingi ambayo tumejiwekea katika utendaji kazi wetu" alisisitiza
 
Karibu Sana Katibu naamini mchakato utakuwa mzuri na placement zitatoka kwa wakati, jobless tunaimani na nyie
 
Wakuu Tiwasamehe watu.

Nadhani sehemu ya PLACEMENT WAMEISAHAU.

Tuendelee kukesha kwa mwamposa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…