Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Acheni kuwaogopa hao viazi wanaojifanya wanatoa misaada.

Msaada uko katika bwana aliyeziumba mbingu na nchi.

Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na amfanyae kinga yake.

Zab 23 BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Wafilipi 4;13.Naweza kufanya mambo yote katika yeye anipaye nguvu

Zab 56;11

Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
Sekretarieti ya ajira wasipo tenda haki watakua wameyakanyaga maana majobless hadi neno la Mungu wanalijua
 
Psrs ndo sehemu pekee ambayo kunakua na uwazi kwa asilimia kubwa sana katika mchakato wake wa ajira.

Kuna siku BOT walitoa post ya kada yangu niliomba ili sizani hata kama ile barua yangu ilisomwa.

Ila uku psrs ww ukifuata maelekezo yao tu una 99.9%ya kuitwa mengine ukayapambanie mwenyewe.

Mimi kuna watu wengi sana wamepata ajira kupitia psrsbila kufaamiana na mtu yeyotee. Ila vip uko kwenye masekta mengine wanao ajili wenyewe??

Mimi bado naona kuna namna psrs wanakutana na lawama zetu sisi ma jobless ila wao sio wa kulaumiwa.
Ni kweli mkuu unachokisema lkn waongezee nguvu kazi wapo slow sana sijui kama wao ni ng'ombe wa nyuma. Sasa hivi sio kuchelewa kuita watu job bali ni hata kuita watu interview pia. Waongezewe nguvu kama ni chombo kinaweza handle graduants wote nchi nzima watumishi wawe wengi na wapunguze urasimu pia
 
PSRS huwa wanaajiri wanachukua kutoka database.

Sijawahi kuona watangaze nafasi za kazi ila nimeshuhudia placement kadhaa zimepangia watu kazi PSRS.

Kwenye huu uzi kuna jamaa alilamba asali huko PSRS kupitia database
Mkuu thibitisha ww ulilamba asali kwa connection au juhudi binafsi mkuu
 
Moja ya jambo naloshukuru Maisha yangu nimepambana sana na ujobless.

Kwa sasa nimeajiriwa tena serikalini japo sio ya kustaafu kama wengine.

Ila nafanya saili nikiwa nimerelax tofauti na mwanzo hivyo Mengine nimemwachia Mungu tu.

Sio wapuuzi wa kunitisha.

Mwifwa kaka Una mbingu yako achana na hawa wapuuzi wanaojifanya wanaamsaada kisa wametukwana kwanini hawajatusaidia tukiwa cool
Hahahaa, ila huu uzi unapitia vipindi tofauti tofauti sana.

Kuna watu wa aina tofauti tofauti pia, wenye hasira wanaonekana kuwa ni wengi lakini kinachofurahisha, pindi wakipata placement huwa wanajirudi na kuwa watu poa hatimaye kupotea hapa na kwenda kuendelea na mambo mengine.

Hivyo kuwa na hasira sio vibaya maana ni njia mojawapo ya kurecover kutokana na hali uliyonayo.

Mwisho wa siku tunarudi kule kule kwenye uvumilivu na muda wako ukiwadia unaingia kundini.

Kama una kijiwe ulichojishikiza komaa hapo hapo na kuwa mtiifu fanya kazi kwa bidii, ipo siku utashangilia na kusherehekea, mtaani ni pa moto asikwambie mtu.
 
Mkuu thibitisha ww ulilamba asali kwa connection au juhudi binafsi mkuu
Finally I made it!

Kutana na Mwifwa- From three times defeat to Champion

Hii ndio ilikuwa safari yangu ya kusaka mrija wa Asali.

Mwaka 2021, safari hii ilishika kasi kwa kuapply mara 8( Sekta binafsi, Wizarani na Tamisemi). Kote niliangukia pua, Sekta binafsi sikubahatika hata kuitwa kwa usahili.

Mwaka 2022, kasi ikaendelea kushika kasi nilipoapply Wizarani na Tamisemi kabla ya kutimkia PSRS, mara hii niliangukia pua pia Wizarani na Tamisemi.

PSRS nilifanya application 5, 4 nikawa shortlisted, moja sikuwa shortlist kwa sababu isiyokuwa ya msingi maana hiyo sababu wangeizingatia nisingekuwa shortlist zile zingine 4.

Kwenye shortlist 4, tatu nikakandwa mfululizo hadi nikakata tamaa, ila wadau wa humu wakanipa moyo na nikapata nguvu ya kwenda kupambana.

Baada ya kwenda kwenye battle nikaingia oral kimasihara. The rest is history, what a joyful in my life history, my eyes are filled with joyful tears.

Join me in celebrating this remarkable history!!
Tunaposema enzi zetu uzi ulikuwa bora, wenye kutia matumaini, hamasa, faraja ilikuwa namna hii.

Hiyo comment itabaki kuwa comment bora zaidi kuliko zote nilizowahi kupost kwenye huu uzi
 
Tunaposema enzi zetu uzi ulikuwa bora, wenye kutia matumaini, hamasa, faraja ilikuwa namna hii.

Hiyo comment itabaki kuwa comment bora zaidi kuliko zote nilizowahi kupost kwenye huu uzi
Mkuu nipe connection nitoke huku mabonde kuinuka PSRS ilikonileta 😁
 
Tunaposema enzi zetu uzi ulikuwa bora, wenye kutia matumaini, hamasa, faraja ilikuwa namna hii.

Hiyo comment itabaki kuwa comment bora zaidi kuliko zote nilizowahi kupost kwenye huu uzi
Uko MDAs/ LGAs?
 
PSRS huwa wanaajiri wanachukua kutoka database.

Sijawahi kuona watangaze nafasi za kazi ila nimeshuhudia placement kadhaa zimepangia watu kazi PSRS.

Kwenye huu uzi kuna jamaa alilamba asali huko PSRS kupitia database
kweli aisee kuna muda niliona kwenye pdf watu wameajiliwa tu lakini sjawahi kuona tangazo lolote
 
Subra yavuta kheri, sema kwa mimi ninavoona hizi taasisi ndo zinataka kutupambanisha majobless na Utumishi kwa sababu mpaka Utumishi wanatoa Tangazo la kazi lazima wanakua wamepokea barua ya kuhitajika kwa watu kadhaa, na Utumishi wakiipokea ndo wanatutangazia sisi sasa naona shida ipo kwenye hizo taasisi kuita watu kazini hapa ndo unakuja uchonganishi kati yetu na utumishi na kabla hujawalaumu Utumishi jiulize swali kwamba JE UNAFIKIRI HIZI TAASISI ZINAPENDA KUONA UTUMISHI ANAZIDI KUENDELEA KUFANYISHA SAILI KWA HAKI? maana yake wameziba mianya ya viongozi fulani kwenye taasisi hizo kupitisha watu wao, kwahiyo nadhani jibu ni kwamba hizo taasisi hazipendi hiki kitu kuendelea (kwa mawazo yangu lakini😁)lakini pia hili la baadhi ya taasisi kujitoa tusilishabikie saana maana kama wakiendelea kuajiri wenyewe sisi tusio na watu huko tutateseka sana, tena zaidi ya sana kama huamini jaribu kuomba nafasi TRA na taasisi nyingine zinazoajili zenyewe, mwisho utaishia kusonya tu😅 SIKU ZOTE HUWA NAAMINI SERIKALI INA MIPANGO MIZURI, ILA KUNA WATU WACHACHE WANAKWAMISHA HIYO MIPANGO KWA FAIDA ZAO WENYEWE.

GOOD MORNING JOBLESS 💥🤗
 
😂😂😂
Tusubilini mpka taasis ziwaambie waiteni vijana wetu sasahv tunauitaji nao, kwan wao si ku print na ku sign tu.. Tahasi bado zinajipana namna ya kukuhandle mkuu,

Wengine uko mtalipiwa nyumba, usafiri bado na maposh kibao. Lazima tahasis ikuandalie mzingira mkuu.
Wanaowaingiza kazini kupitia mlango wa nyuma mpaka wanafanya training wao fedha za kuhandle wanazipata wap?...
 
Finally I made it!

Kutana na Mwifwa- From three times defeat to Champion

Hii ndio ilikuwa safari yangu ya kusaka mrija wa Asali.

Mwaka 2021, safari hii ilishika kasi kwa kuapply mara 8( Sekta binafsi, Wizarani na Tamisemi). Kote niliangukia pua, Sekta binafsi sikubahatika hata kuitwa kwa usahili.

Mwaka 2022, kasi ikaendelea kushika kasi nilipoapply Wizarani na Tamisemi kabla ya kutimkia PSRS, mara hii niliangukia pua pia Wizarani na Tamisemi.

PSRS nilifanya application 5, 4 nikawa shortlisted, moja sikuwa shortlist kwa sababu isiyokuwa ya msingi maana hiyo sababu wangeizingatia nisingekuwa shortlist zile zingine 4.

Kwenye shortlist 4, tatu nikakandwa mfululizo hadi nikakata tamaa, ila wadau wa humu wakanipa moyo na nikapata nguvu ya kwenda kupambana.

Baada ya kwenda kwenye battle nikaingia oral kimasihara. The rest is history, what a joyful in my life history, my eyes are filled with joyful tears.

Join me in celebrating this remarkable history!!
Nmesoma comments za member wa mwaka jana sion hata mmoja active lately ni ww tu umebaki basi ikawe kheri na sisi jobless 💯
 
tanapa kuna pdf lingine uko
Kama kuna raia hapa wa tanapa na amelamba asali na alikuwa akilalamika kuhusu ucheleweshaji wa pdf, sasa hv ukimuuliza hawezi kukumbuka kama kulikuwa na ucheleweshaji.

Guys, mm naona kwenye mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu hasa hapo kwenye kutoa pdf tuzidi kuwa wapole huku kumuomba Mungu mana pdf zinaweza kutolewa kila siku na bado haupo, n bora zichelewe then siku wakitoa bc na ww uwepo.
 
sio kwamba zikiwa zinawahi probability ya kutokea mapema inakua kubwa..?
 
Kama kuna raia hapa wa tanapa na amelamba asali na alikuwa akilalamika kuhusu ucheleweshaji wa pdf, sasa hv ukimuuliza hawezi kukumbuka kama kulikuwa na ucheleweshaji.

Guys, mm naona kwenye mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu hasa hapo kwenye kutoa pdf tuzidi kuwa wapole huku kumuomba Mungu mana pdf zinaweza kutolewa kila siku na bado haupo, n bora zichelewe then siku wakitoa bc na ww uwepo.
Ni kweli mkuu ila tusiwe wapole sana, tusiwe wanyonge kihivyo lazima tuwafokee fokee kidogo ili wawahishe mambo. Wengine tunasubiri check number ili tulipe madeni mtaani
 
Back
Top Bottom