Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Sekretarieti ya ajira wasipo tenda haki watakua wameyakanyaga maana majobless hadi neno la Mungu wanalijua
 
Ni kweli mkuu unachokisema lkn waongezee nguvu kazi wapo slow sana sijui kama wao ni ng'ombe wa nyuma. Sasa hivi sio kuchelewa kuita watu job bali ni hata kuita watu interview pia. Waongezewe nguvu kama ni chombo kinaweza handle graduants wote nchi nzima watumishi wawe wengi na wapunguze urasimu pia
 
PSRS huwa wanaajiri wanachukua kutoka database.

Sijawahi kuona watangaze nafasi za kazi ila nimeshuhudia placement kadhaa zimepangia watu kazi PSRS.

Kwenye huu uzi kuna jamaa alilamba asali huko PSRS kupitia database
Mkuu thibitisha ww ulilamba asali kwa connection au juhudi binafsi mkuu
 
Hahahaa, ila huu uzi unapitia vipindi tofauti tofauti sana.

Kuna watu wa aina tofauti tofauti pia, wenye hasira wanaonekana kuwa ni wengi lakini kinachofurahisha, pindi wakipata placement huwa wanajirudi na kuwa watu poa hatimaye kupotea hapa na kwenda kuendelea na mambo mengine.

Hivyo kuwa na hasira sio vibaya maana ni njia mojawapo ya kurecover kutokana na hali uliyonayo.

Mwisho wa siku tunarudi kule kule kwenye uvumilivu na muda wako ukiwadia unaingia kundini.

Kama una kijiwe ulichojishikiza komaa hapo hapo na kuwa mtiifu fanya kazi kwa bidii, ipo siku utashangilia na kusherehekea, mtaani ni pa moto asikwambie mtu.
 
Mkuu thibitisha ww ulilamba asali kwa connection au juhudi binafsi mkuu
Tunaposema enzi zetu uzi ulikuwa bora, wenye kutia matumaini, hamasa, faraja ilikuwa namna hii.

Hiyo comment itabaki kuwa comment bora zaidi kuliko zote nilizowahi kupost kwenye huu uzi
 
Tunaposema enzi zetu uzi ulikuwa bora, wenye kutia matumaini, hamasa, faraja ilikuwa namna hii.

Hiyo comment itabaki kuwa comment bora zaidi kuliko zote nilizowahi kupost kwenye huu uzi
Mkuu nipe connection nitoke huku mabonde kuinuka PSRS ilikonileta 😁
 
Tunaposema enzi zetu uzi ulikuwa bora, wenye kutia matumaini, hamasa, faraja ilikuwa namna hii.

Hiyo comment itabaki kuwa comment bora zaidi kuliko zote nilizowahi kupost kwenye huu uzi
Uko MDAs/ LGAs?
 
PSRS huwa wanaajiri wanachukua kutoka database.

Sijawahi kuona watangaze nafasi za kazi ila nimeshuhudia placement kadhaa zimepangia watu kazi PSRS.

Kwenye huu uzi kuna jamaa alilamba asali huko PSRS kupitia database
kweli aisee kuna muda niliona kwenye pdf watu wameajiliwa tu lakini sjawahi kuona tangazo lolote
 
Subra yavuta kheri, sema kwa mimi ninavoona hizi taasisi ndo zinataka kutupambanisha majobless na Utumishi kwa sababu mpaka Utumishi wanatoa Tangazo la kazi lazima wanakua wamepokea barua ya kuhitajika kwa watu kadhaa, na Utumishi wakiipokea ndo wanatutangazia sisi sasa naona shida ipo kwenye hizo taasisi kuita watu kazini hapa ndo unakuja uchonganishi kati yetu na utumishi na kabla hujawalaumu Utumishi jiulize swali kwamba JE UNAFIKIRI HIZI TAASISI ZINAPENDA KUONA UTUMISHI ANAZIDI KUENDELEA KUFANYISHA SAILI KWA HAKI? maana yake wameziba mianya ya viongozi fulani kwenye taasisi hizo kupitisha watu wao, kwahiyo nadhani jibu ni kwamba hizo taasisi hazipendi hiki kitu kuendelea (kwa mawazo yangu lakini😁)lakini pia hili la baadhi ya taasisi kujitoa tusilishabikie saana maana kama wakiendelea kuajiri wenyewe sisi tusio na watu huko tutateseka sana, tena zaidi ya sana kama huamini jaribu kuomba nafasi TRA na taasisi nyingine zinazoajili zenyewe, mwisho utaishia kusonya tu😅 SIKU ZOTE HUWA NAAMINI SERIKALI INA MIPANGO MIZURI, ILA KUNA WATU WACHACHE WANAKWAMISHA HIYO MIPANGO KWA FAIDA ZAO WENYEWE.

GOOD MORNING JOBLESS 💥🤗
 
Wanaowaingiza kazini kupitia mlango wa nyuma mpaka wanafanya training wao fedha za kuhandle wanazipata wap?...
 
Nmesoma comments za member wa mwaka jana sion hata mmoja active lately ni ww tu umebaki basi ikawe kheri na sisi jobless 💯
 
tanapa kuna pdf lingine uko
Kama kuna raia hapa wa tanapa na amelamba asali na alikuwa akilalamika kuhusu ucheleweshaji wa pdf, sasa hv ukimuuliza hawezi kukumbuka kama kulikuwa na ucheleweshaji.

Guys, mm naona kwenye mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu hasa hapo kwenye kutoa pdf tuzidi kuwa wapole huku kumuomba Mungu mana pdf zinaweza kutolewa kila siku na bado haupo, n bora zichelewe then siku wakitoa bc na ww uwepo.
 
sio kwamba zikiwa zinawahi probability ya kutokea mapema inakua kubwa..?
 
Ni kweli mkuu ila tusiwe wapole sana, tusiwe wanyonge kihivyo lazima tuwafokee fokee kidogo ili wawahishe mambo. Wengine tunasubiri check number ili tulipe madeni mtaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…