Upo sahihi sana, lakini ulipaswa kuongezea kuwa wizara ya afya ina ngazi tofauti ya hospitali na pia ina taasisi na mamlaka zilizo chini yake.
Watumishi wote wa kada za Afya waliopo wizarani (makao makuu), hospitali za mikoa, na wale waliopo Tamisemi wanalipwa mishahara yao kwa ngazi za TGHS, wote wanafanana mishahara yao.
Watumishi wa kada za Afya waliopo katika hospitali za kanda, hospitali maalum za kitaifa (Mirembe, Kibong'oto etc), na hospitali ya taifa wanalipwa kwa ngazi za mshahara za PGMSS ambazo zipo juu kuliko zile za TGHS.
Watumishi wa kada za afya waliopo katika taasisi na mamalaka zilizo chini ya wizara ya afya (NHIF, TMDA, MSD, NIMR etc) wanalipwa kwa scale za mishahara maalum kutegemeana na taasisi ama mamlaka husika, mara nyingi zipo juu kuliko za hospitali za hapo juu.