Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kuna kozi yangu kwa assistant lecturer mpaka sasa vyuo kama 8 vimeshatangaza kazi na hakuna hata mmoja nimewahi kuona anaomba sasa najiuliza si wachukue tutorial assistant tu wakienda huko wasome badae wawe assistant lecturer.
 
Wadau mambo Vip? Naomba mwenye link ya group ya Trade officer na Customer service officer anitumie. Thanks
 
Sawa asiende!Ila after years asirudi analia lia baada ya mfumo wa placement kuwa unamtema kila akiomba kazi maana utakuwa unakumbuka kuwa keshapangiwaga.
 
Nilikuwa nasuburia advertisement karibia mwaka mzima..
Leo na nasuburia call for interview inaenda miezi mi nne😀😀
Then nitaanza kusubiria placement tena ya database mwaka mzima😀
Mungu atutie nguvu jobless
Call for interview yaan unaweza ukasahau
Mwezi wa 7
Mwezi wa 8
Mwezi wa 9
Mwezi wa 10
Mwezi wa 11

Unaelekea mwezi wa 12 hakuna kuitwa interview kuna watu wameapply TCRA mwezi wa 10 mwezi wa 11 wamepiga interview hawa wengine kuna nini mboni inachukua muda mrefu kuitwa interview au lundo la watu wanashindwa kuwapanga?
 
Lakini uzuri waliomba wenyewe hizo za LGAz hivyo hakuna shideeer
 
Niliituma maombi ya kazi ajira portal toka mwezi wa nane mpaka Sasa sijapata majibu yoyote... Ndugu zangu au nitakuwa nimetemwa? Mwenyewe experience na hili anidodose nisije nikawa nasubilia embe kwenye mnazi
 
Kuwa mvumilivu Mkuu kama ungekuwa umetemwa ungeona notification ambayo ingekuambia nini sababu ya wewe kutemwa ivyo mchakato bado unaendelea
 
Hawa jamaa nahisi wamzidiwa
 
Sema ingekuwa ukiomba kazi ndani mwezi moja unaitwa kwa interview. Ingekuwa poa sana. Nahisi hata ratio ya jobless ingepungua
 
Sema ingekuwa ukiomba kazi ndani mwezi moja unaitwa kwa interview. Ingekuwa poa sana. Nahisi hata ratio ya jobless ingepungua
Interview zinavuuutwa saaaaana sijui wanafanya michongo gani huko sasa hio interview tu kuitwa utasugua lami sio mchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…